Mwandishi Ansbert Ngurumo apewa hifadhi kwa usalama wake nchini Finland

Ni habari mbaya kwa nchi yetu inaendelea kuwa na hadhi mbaya ndani /nje ya mipaka yake. Maisha ya waandishi wa habari, wanasiasa na wanaharakati yamekuwa ya mashaka.

Mwanahabari Ansbert Ngurumo aliyewahi kuwa mhariri wa Magazeti ya Tanzania Daima na Mwanahalisi, amekimbilia nchini Finland na kupewa hifadhi huko, kwa muda alikuwa akisema anatishiwa kuuawa.

Habari zaidi soma=> Ansbert Ngurumo: Muda wowote naweza kufa maana natishiwa kifo

UPDATE:

Mwandishi wa Habari mwandamizi nchini, Ansbert Ngurumo amepata hadhi ya kupewa ulinzi nchini Finland, baada ya kudai amekimbia aliowaita "wauaji" wake.

Ngurumo ambaye amewahi kuwa mhariri wa magazeti kadhaa nchini; Mtanzania, Tanzania Daima na MwanaHalisi, ameiambia JamiiForums kuwa amekiepuka kifo kilichopangwa na wale aliowaita "wasiojulikana."

Akizungumza na JamiiForums, Ngurumo alisema ni kweli amekimbia Tanzania ili kuulinda uhai wake baada ya kuanza kuwindwa na watu wasiojulikana.

"Tangu mwaka jana nimekuwa nikipokea vitisho vingi na vyenye kuogofya kufuatia makala zangu kwenye gazeti la MwanaHalisi. Nimenusurika kuuawa mara kadhaa, lakini nashukuru Mungu hadi leo niko hai," anasema Ngurumo.

Anasema ili kunusuru uhai wake, alilazimika kujificha Mwanza tangu mwaka jana na baadaye kupata kwenda Kenya, kabla ya kwenda Sweden na sasa Finland, ambako amepewa hifadhi.

Ngurumo anasema hadhi aliyopewa Finland, siyo ya ukimbizini, bali ni "hifadhi ya kimataifa," kuunusuru uhai wa mtu ambaye yuko katika hatari ya kuuawa nchini mwake.

Vyombo vya Habari vya Finland na mitandao ya kijamii, imeandika habari ya Ngurumo kukimbia Tanzania kwa hofu ya kuuawa.

"Nimezungumzia mkasa wangu wa kunusurika kudakwa na watu wasiojulikana, ambao wamekuwa wakipanga kuniua na wamejaribu mara kadhaa bila mafanikio, sasa nikaona niwakimbie, kwani kufa kijinga ni dhambi kubwa," anaongeza Ngurumo.

JamiiForums inatambua kuwa Ngurumo alianza kuhofia maisha yake baada ya kudai kupokea vitisho kwa alichodai ni kufuatia kuandika makala kwenye gazeti la MwanaHalisi ikiwa na kichwa cha habari; “Tumuombee Rais Magufuli au Tundu Lissu?”
Wengine tulidai kuna raia tu watafuata mkumbo..


Ebu tufuatilie thread za Ansbert Ngurumo..zaleta picha za kuchanganya, anasifu, anaponda, anasifu, anaponda, mwisho anahofia maisha yake! Duh...

Ansbert Ngurumo amchana Kikwete live... Ansbert Ngurumo amchana Kikwete live... via JamiiForums
Ansbert Ngurumo anauliza: Maamuzi magumu? Mbona tuko gizani? Ansbert Ngurumo anauliza: Maamuzi magumu? Mbona tuko gizani? via JamiiForums
Ngurumo acha kumchafua JK baada ya kukunyima nafasi Ikulu Ngurumo acha kumchafua JK baada ya kukunyima nafasi Ikulu via JamiiForums
Ansbert Ngurumo: Muone, kichwa kama CCM Ansbert Ngurumo: Muone, kichwa kama CCM via JamiiForums
Ansbert Ngurumo endorses lowassa for presidency 2015? Ansbert Ngurumo endorses lowassa for presidency 2015? via JamiiForums
Ansbert Ngurumo: Roma 1,300, CCM 50 Ansbert Ngurumo: Roma 1,300, CCM 50 via JamiiForums
Ngurumo avuruga ziara ya Slaa Kagera! Ngurumo avuruga ziara ya Slaa Kagera! via JamiiForums
Ansbert Ngurumo awamwagia Pongezi za ushindi kwa Makamanda wa CHADEMA! Ansbert Ngurumo awamwagia Pongezi za ushindi kwa Makamanda wa CHADEMA! via JamiiForums
Swali la Ngurumo kwa Rais Kikwete ... nani wa kumsaidia kumjibu? Swali la Ngurumo kwa Rais Kikwete ... nani wa kumsaidia kumjibu? via JamiiForums
Ansbert Ngurumo: Kikwete anajua CCM bingwa wa udini? Ansbert Ngurumo: Kikwete anajua CCM bingwa wa udini? via JamiiForums
Ansbert Ngurumo: Lowassa Mpya Amenikumbusha Makubwa Ansbert Ngurumo: Lowassa Mpya Amenikumbusha Makubwa via JamiiForums
Ngurumo ampongeza Rais Magufuli Ngurumo ampongeza Rais Magufuli via JamiiForums
Daniel Ngogo, Ansbert Ngurumo kupigania ubunge Mahakamani Daniel Ngogo, Ansbert Ngurumo kupigania ubunge Mahakamani via JamiiForums
Ansbert Ngurumo aonya maamuzi ya Rais na kutoshaurika Ansbert Ngurumo aonya maamuzi ya Rais na kutoshaurika via JamiiForums
Ansbert Ngurumo: Taifa linaelekea pabaya sana Ansbert Ngurumo: Taifa linaelekea pabaya sana via JamiiForums
Ansbert Ngurumo: Muda wowote naweza kufa maana natishiwa kifo Ansbert Ngurumo: Muda wowote naweza kufa maana natishiwa kifo via JamiiForums
 
Hovyooo
emoji83.png
emoji379.png
emoji61.png
emoji218.png
emoji196.png
Jenga hoja acha attacks
Mumeo aliekushindisha njaa ndio mwenye njaa
Kumbe umeolewa jamaa,tunza mji wako acha kuparamia wanaume
 
Back
Top Bottom