Mwandishi aliyechinjwa na IS

Mwandishi aliyechinjwa na IS

Status
Not open for further replies.

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
33,569
Reaction score
53,583
140820234200_sp_steven_sotloff_304x171_reuters_nocredit.jpg

Mwandishi aliyechinjwa na IS, Steven Sotloff


Wapiganaji wa dola ya Kiislam IS wamesambaza picha za video katika mitandao kwa lengo la kuonyesha kuchinjwa kwa mwandishi wa habari raia Marekani Steven Sotloff ambaye ni mmoja wa mateka wanaoshikiliwa na wapiganaji hao.

Mwandishi huyo Sotloff, mwenye umri wa miaka 31 ambaye alitekwa na wapiganaji hao mwezi August mwaka jana.

Mwezi uliopita Sotloff alionekana mwishoni katika picha za video zilizoonyeshwa kuhusiana na kuchinjwa kwa mwandishi mwingine wa Marekani James Foley.

Wapiganaji hao wa katika picha hizo pia wameonekana wakimtishia kumuua mateka mwingine anayedhaniwa kuwa ni raia wa Uingereza.
Baada ya mauaji ya mwandishi wa awali Foley, mama mzazi wa mwandiashi wa Sotloff alitoa ombi maalumu kwa kiongozi wa wanajeshi hao Abu Bakr al-Baghdadi kutoa muua mtoto wake.

Msemaji wa Ikulu ya White House Josh Earnest amesema kuwa maofisa wa Marekani wanaendelea na uchunguzi wa ripoti hiyo.
Marekani hivi karibuni ilifanya mashambulizi ya anga dhidi ya IS nchini Iraq.

Mwandishi wa masuala ya usalama wa BBC Frank Gardner amesema hatua hiyo ya wapiganaji wa IS ni kulipa kisasi kwa Marekani.

Chanzo:BBC

http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2014/09/140902_hostage_death.shtml
 
Nimeogopa kuangalia hiyo video. Imani za kuchinja watu kama kuku.
 
God have mercy waarabu wakianza kumalizana ukichangia na ma evil spirits watachoka tu bure maana kila nafsi itaonja mauti
 
Hawa ISIS ni mbwa pori. Lakini itabidi turudi nyuma, nani aliwaachia hawa mbwa pori walipoanza kushambulia Syria? Si waliitwa wapigania uhuru?
Usidaganyike, isingewezekana kwa maelfu ya waovu hawa kuvuka mipaka bila ya kusaidiwa na mataifa hayo hayo yanayotoa machozi ya mamba. Huu ndio mwisho wa ubaguzi wa rangi. Anapouawa Msyria sawa, sasa mkuki kwa binadamu.
 
Dawa ni kuwachimbua kama Hiroshima tuu maliza mpaka kuku labda wataelewa
 
Wamarekani washenzi sana,wao ndio waliosababisha iraq,syria,libya na ht afghanistan kuishi kwa kupigana wenyewe kwa wenyewe,alimuua saddam bure kwa kisingizio eti ana silaha za nyuklia,wako wapi walibya waliokuwa wakiishi kwa raha nchini kwao kiliko nchi yoyote duniani unayoijua wewe,leo mmarekani anawapiganisha na kuwaua raia bila kosa lolote,mbona hajawahi kuinua mdomo kwa kuwaonya waisrail kuwaua watoto na wanawake wasio na hatia huko gaza,haya ndio malipo yenu tunakusubirini na huku iran mje mtugombanishe muone km mtaishi tena nje ya nchi yenu,wasiojua wataona waislam wanawachinja bila kosa lkn kosa limefanya nchi yao kwa kumwaga damu ndani ya nchi za watu,yuko wapi sadam na wanawe leo hii?yuko wapi gadafi na wanawe leo hii?yote hayaonekani wanaonekana hao wenye machungu ya kuvamiwa na kupiganishwa ndani ya nchi yao kuwa wao ndio wahalifu,wamarekani msipojirekebisha mtamalizwa kidogo kidogo,ajenda ya siri ya obama imejulikana na sasa ni kuwalipiza kisasi tu,haihusiani na dini na hata ukiwasikiliza ISIS wanaeleza wazi wanachowachinjia wamarekani.
 
Obama kichwa kinamuwanga masikini.wamewafunza,wakawapa silaha sasa wanawageuka.na hao wanaouawa ni mashushushu wao,maana mwandishi wa kawaida kwenda nchi kama syria ni kujitakia balaa.
 
ISIS released a brutal video today showing the beading of a second U.S journalist, 31 year old Steven Sotlof. Sotloff had appeared in another video where U.S Journalist James Foley was killed two weeks ago (left. Sotloff pictured right at the execution scene). And it looks like Sotloff was killed by the same executioner who killed Foley on August 19th. He had same British accent and before beheading Sotloff, the terrorist said;
"I'm back Obama, and I'm back because of your arrogant foreign policy towards the Islamic State, because of your insistence on continuing your bombings on Mosul Dam, despite our serious warning. So just as your missiles continue to strike our people, our knife will continue to strike the necks of your people."
Sotloff disappeared while reporting in Syria a year ago. He worked for Time, Foreign policy & others
 
Ni hatari sana kuamini kuwa Mungu ana kiu ya damu za watu.....What kind of God do these people worship?
Obviously the kind of God who is blood thirsty, mbona ushajibu mwenyewe mwanzo wa comment yako???!!
 
Mbwa waliyemfuga wenyewe sasa kawageuka, walimpa siraha syria wakampamba sasa leo hii ndo kawa mbaya.
Wakati anaua watu syria na kushambulia kule walidai ni majeshi yanayo muunga mkono raisi leo imewageukia wanahaha.
Nasema acha wakome hawa Wamarekani na Waingereza wanafiki sana..
Ila kumchinja binadamu mwenzio kama kuku nako kwahitaji uwe na roho ngumu kweli sijui wanapata wapi huo ujasiri
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom