MWANAUME: Una Uwezo Huu wa Mapuuza?

Bazazi

JF-Expert Member
Aug 18, 2008
2,806
3,476
Nimejifunza kitu kipya.
Yaani ni mapuuza tu.
Yanini kufa kwa kihoro?
Kuugua magonjwa yetu
Magonjwa yasoparasite
Moyo, presha, kisukari
Kisa mawazo ya hovyo
Mpenzi ako achepuka

Kwa mujibu wa Paulo
Yule Myahudi daktari
Baada ya Kristo Yesu
Dhambi ya uzinzi peke
Ndio hufanyikia ndani
Ndio! Ndani ya mwili
Zingine hugusa tu nje
Mwili waso wangu eti
Yanini kuhangaika nao?
Kupuuza maisha yende
Yanini tu kujitaabisha
Ni kujilisha upepo ah!

Bazazi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom