Unafahamu unywaji wa maji mengi unasababisha maradhi ya moyo?

Swahili AI

JF-Expert Member
Mar 2, 2016
6,166
46,679
Na Mwandishi Maalum

Lakini, mtaalamu bingwa kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi, ana kidokezo kuhusiana na matumizi ya nadharia hiyo kiholela kwamba yanaweza kumrudisha mhusika katika maradhi zaidi.

Profesa Janabi, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo anasema maji hayo ya ziada yanakuwa na manufaa kwa mnywaji iwapo tu kuna kiwango sahihi cha kuushughulisha mwili wake hata maji hayo yakatumika kwa manufaa kiafya.

Kwa mujibu wa Profesa Janabi, katika hali ya kawaida, mwili wa binadamu huwa na kiwango cha wastani wa lita tano za maji zinazokuwa kwenye mzunguko mwilini na panapotokea maji ya ziada pasipo kutumika, ni hali inayouchosha moyo na kuishia katika kuzalisha maradhi.

Mtaalamu huyo anafafanua kwamba mwili wa binadamu unapokosa shughuli ngumu zinazosababisha jasho kutoka, kiwango cha juu cha unywaji maji kinapaswa kisizidi kati ya lita moja na nusu hadi mbili kwa siku.

“Maji yanayohitajika kwenye mwili wa binadamu kwa siku ni lita moja na nusu, kama hamna joto wala hufanyi kazi ngumu, unasababisha hatari kwenye moyo wako.

“Mzunguko wa damu tayari una lita tano na wewe unakunywa lita tano, kwa hiyo unaulazimisha moyo kusukuma mara mbili zaidi na mwisho wa siku unajikuta una shida ya moyo,” anatahadharisha.

Profesa Janabi anaeleza kwamba, wakati moyo wa mtu unafanya ya kusukuma maji ya ziada kuliko uwezo wake, athari inayofuata baada ya hapo ni baadhi ya chembe hai muhimu zinaanza kufa moja baada ya nyingine zikipishana na maradhi kuanza kuchukua nafasi yake.

Bingwa huyo wa maradhi ya moyo, alitoa katika hadhira ya kilele cha maadhimisho ya Siku ya Moyo Duniani, Septemba 29 mwaka huu katika Viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam.

Mtalaamu huyo anaelekeza kidole cha tahadhari hasa kwa watendaji wa maofisini na mazingira yanayofanana nayo kwamba mbali na hatari ya kuuchosha moyo, pia ziada ya maji hayo imebeba hatari kuyeyusha madini muhimu kwa mwili wa binadamu.

ULAJI NAO TATIZO
Profesa Janabi anataja sababu nyingine kubwa ambayo watu hawafahamu kama ni chanzo cha kuugua maradhi ya moyo kuwa ni ulaji usio wa mpangilio.

Anasema ulaji wa vyakula vya mafuta umekuwa ukitajwa na wengi kuwa tatizo kubwa katika kusababisha maradhi ya moyo, lakini siyo chanzo wala tatizo kubwa bali Ulaji wa vyakula vya wanga ndiyo mzizi wa tatizo.

Anasema vyakula vya wanga kama Ugali na We vinavyoliwa mara nyingi na Watanzania huhatarisha usalama wa moyo na hivyo Anashauri watu kupunguza ulaji wa aina hiyo ya vyakula.

“Ukiweza kujibana, basi unaweza kupunguza kula ugali na wali angalau ule mara mbili kwa wiki kwa vyakula hivi,” anashauri Profesa Janabi.

Anasema ratiba ya vyakula hivyo pia ni lazima izingatiwe na walaji kwa usalama wa moyo.

“Mtu anakula saa tatu, nne hadi saa sita usiku sahani kubwa ya wali au ugali, akimaliza hapo anaingia kitandani analala, hapo badala ya chakula kufanya kazi kinaenda kukaa kwenye stoo,” anatahadharisha Profesa Janabi.

Anasema mlundikano huo ndiyo husababisha zaidi madhara kwa mwili wa binadamu kama vile kutengeneza vitambi, shinikizo la damu na matatizo ya moyo.

Profesa Janabi anashauri kuwa muda sahihi wa kula chakula ni kuanzia saa 12 jioni hadi saa 1:00 usiku, ikiwa ni saa chache kabla ya kwenda kulala.

HALI ILIVYO KITAIFA
Profesa Janabi anasema magonjwa ya moyo huchangia karibu asilimia 31 ya vifo vyote duniani na kwamba takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinabainisha kuwa kila mwaka, takribani watu milioni 18 hufariki dunia kutokana na maradhi hayo.

“Ni tatizo linaloonekana kuongezeka, takwimu zinaonyesha katika kila wanawake wanne na wanaume watano, mmoja ananakabiliwa na tatizo la shinikizo la damu,” anabainisha.

Anaongeza kuwa magonjwa ya moyo ni kati ya magonjwa yasiyoambukiza, ambayo kinga ni rahisi kuliko tiba, ndiyo maana WHO pamoja na Jumuiya ya Magonjwa ya Moyo Duniani baada ya kuona yanaongezeka, wakaamua kuanzisha Siku ya Moyo Duniani.

“Watu pia wanapaswa kuzingatia unywaji wa pombe kwa kiasi, kuacha uvutaji wa sigara, kula vyakula vinavyofaa, wazingatie kunywa dawa wanazoandikiwa (waliokutwa na matatizo haya) na wafanye mazoezi, wapunguze uzito uliopitiliza. Haya ni mambo ambayo yapo ndani ya uwezo wa mtu bila gharama,” anasema.

Mkurugenzi huyo anabainisha kuwa JKCI tangu mwaka 2015 ilipoanzishwa hadi sasa, tayari imeshaona takribani wagonjwa 350,000 huku 6,000 kati yao wakifanyiwa upasuaji.

“JKCI tupo mstari wa mbele kutoa elimu ili watu waepuke magonjwa haya,” anasema Profesa Janabi.

BP IKO JIRANI
Mtaalamu huyo anabainisha kuwa asilimia 70 ya wagonjwa wanaotibiwa JKCI, wanakabiliwa na tatizo la Shinikizo la Damu (BP).

Anasema takwimu zao zinaonyesha ndiyo tatizo linaloongoza kwa idadi kubwa ya wagonjwa katika taasisi hiyo tangu ilipoanzishwa rasmi mwaka 2015.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa JKCI, Samweli Rweyemamu, anasema wapo pia wengine wanaokabiliwa na tatizo la kuziba kwa mishipa ya damu inayosambaza damu kwenye moyo ambayo husababisha kifua kuuma.

“Kuna wengine wanaohitaji upasuaji na idadi inaongezeka kila siku. Kwa mfano, wale ambao mishipa ya damu inaziba, tunawazibua kwa upasuaji mkubwa au ule wa tundu dogo,” anasema Dk. Rweyemamu.

Anabainisha kuwa hadi Desemba mwaka jana, waliwachunguza karibu wagonjwa 1,000, ambao awali walikuwa wakipewa rufani ya kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Daktari bingwa huyo anasema kuwa kwa siku, huwa wanaona wagonjwa kati ya 300 na 400, hali inayoonyesha kwamba watu wenye matatizo ya moyo wanaongezeka nchini.

Dk. Rweyemamu anatoa mfano I got kwamba Wilaya ya Temeke kwenye Viwanja vya Zakheem walipima watu 100 na kati yao, asilimia 18 walikuwa na BP IS na wengine moyo umetanuka. Pia, 21 walionekana wana matatizo ya moyo.

Anasema pia walifanya kazi kama hiyo katika viwanja vya Mwembe Yanga kwa watu 150 na kati yao, asilimia 22 walionekana kuwa na maradhi ya moyo. Anasema kati ya hiyo asilimia 22, asilimia 19 walikuwa na shinikizo la damu la juu.

Anaongeza kuwa idadi hiyo inawezekana kuwa ni ndogo lakini utafiti uliofanyika Dar es Salaam, unaonyesha karibu asilimia 30 wana shida ya shinikizo la damu.

“Sasa ukiwa na shinikizo la damu ni ‘risk factor’ (ishara hatari) ya kuziba kwa mishipa ya moyo hatimaye utafika kwetu tukuzibue kwa vifaa maalum,” anasema Dk. Rweyemamu.

Anasema mtu akiwa na shinikizo la damu, moyo hutanuka na kuwa na dalili za kushindwa kufanya kazi, hivyo asilimia kubwa ya matatizo ya moyo kwa watu wazima yanaanza na presha.

Mratibu wa Tiba wa Manispaa ya Kinondoni kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo, Dk. Omary Mwangaza, anasema kipindi cha Julai na Agosti mwaka huu, katika vituo vya kutolea huduma za afya, waliibua wagonjwa wapya zaidi ya 600 wanaokabiliwa na magonjwa yasiyoambukiza.

“Shinikizo la damu na kisukari ni magonjwa yaliyokuwa yakiongoza kwa idadi kubwa ya wagonjwa, wagonjwa wote hawa tumewaingiza kwenye mfumo wetu wa matibabu,” anabainisha.

1619596687423.png
 
Hawa wataalam wetu hawa ndiyo maana msukuma anawachana live, ukienda kwa wataalam wa lishe wanakwambia kunywa maji mengi na ya kutosha, hawa madaktari nao wanatuambia msinywe maji mengi mtapata maradhi ya moyo. Naona hii sasa ni lugha gongano au vimeumana, ebu hao wataalam wakae chini watupe kauli moja kipi ni sahihi!
 
Amesema kunywa maji kulingana na unavyoushughulisha mwili...hakuna KAZI yoyote ngumu umefanya ya kukutoa jasho kwasana unakimbilia kukalili eti kwasiku lazima unywe Lita tano za maji...KAMA HUJAFANYA KAZI YA KUKUTOA JASHO KUNYWA LITA MOJA NA NUSU AU MBILI KWA SIKU....
 
Mimi nakunywa sana maji ndipo najisikia vizuri. Si kutokana na ushauri wa madaktari, la hasha; bali ni mahitaji ya mwili wangu hata nisipofanya kazi ya kutoa jasho.

Nadhani tunywe na kula kile ambacho mwili wako unakubaliana nacho, si kile asemacho daktari kwa kuwa miili inatofautiana. Ukisema wali mara moja kwa wiki utakosana na watu wa Kyela!
 
Na Mwandishi Maalum

Lakini, mtaalamu bingwa kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi, ana kidokezo kuhusiana na matumizi ya nadharia hiyo kiholela kwamba yanaweza kumrudisha mhusika katika maradhi zaidi.

Profesa Janabi, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo anasema maji hayo ya ziada yanakuwa na manufaa kwa mnywaji iwapo tu kuna kiwango sahihi cha kuushughulisha mwili wake hata maji hayo yakatumika kwa manufaa kiafya.

Kwa mujibu wa Profesa Janabi, katika hali ya kawaida, mwili wa binadamu huwa na kiwango cha wastani wa lita tano za maji zinazokuwa kwenye mzunguko mwilini na panapotokea maji ya ziada pasipo kutumika, ni hali inayouchosha moyo na kuishia katika kuzalisha maradhi.

Mtaalamu huyo anafafanua kwamba mwili wa binadamu unapokosa shughuli ngumu zinazosababisha jasho kutoka, kiwango cha juu cha unywaji maji kinapaswa kisizidi kati ya lita moja na nusu hadi mbili kwa siku.

“Maji yanayohitajika kwenye mwili wa binadamu kwa siku ni lita moja na nusu, kama hamna joto wala hufanyi kazi ngumu, unasababisha hatari kwenye moyo wako.

“Mzunguko wa damu tayari una lita tano na wewe unakunywa lita tano, kwa hiyo unaulazimisha moyo kusukuma mara mbili zaidi na mwisho wa siku unajikuta una shida ya moyo,” anatahadharisha.

Profesa Janabi anaeleza kwamba, wakati moyo wa mtu unafanya ya kusukuma maji ya ziada kuliko uwezo wake, athari inayofuata baada ya hapo ni baadhi ya chembe hai muhimu zinaanza kufa moja baada ya nyingine zikipishana na maradhi kuanza kuchukua nafasi yake.

Bingwa huyo wa maradhi ya moyo, alitoa katika hadhira ya kilele cha maadhimisho ya Siku ya Moyo Duniani, Septemba 29 mwaka huu katika Viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam.

Mtalaamu huyo anaelekeza kidole cha tahadhari hasa kwa watendaji wa maofisini na mazingira yanayofanana nayo kwamba mbali na hatari ya kuuchosha moyo, pia ziada ya maji hayo imebeba hatari kuyeyusha madini muhimu kwa mwili wa binadamu.

ULAJI NAO TATIZO
Profesa Janabi anataja sababu nyingine kubwa ambayo watu hawafahamu kama ni chanzo cha kuugua maradhi ya moyo kuwa ni ulaji usio wa mpangilio.

Anasema ulaji wa vyakula vya mafuta umekuwa ukitajwa na wengi kuwa tatizo kubwa katika kusababisha maradhi ya moyo, lakini siyo chanzo wala tatizo kubwa bali Ulaji wa vyakula vya wanga ndiyo mzizi wa tatizo.

Anasema vyakula vya wanga kama Ugali na We vinavyoliwa mara nyingi na Watanzania huhatarisha usalama wa moyo na hivyo Anashauri watu kupunguza ulaji wa aina hiyo ya vyakula.

“Ukiweza kujibana, basi unaweza kupunguza kula ugali na wali angalau ule mara mbili kwa wiki kwa vyakula hivi,” anashauri Profesa Janabi.

Anasema ratiba ya vyakula hivyo pia ni lazima izingatiwe na walaji kwa usalama wa moyo.

“Mtu anakula saa tatu, nne hadi saa sita usiku sahani kubwa ya wali au ugali, akimaliza hapo anaingia kitandani analala, hapo badala ya chakula kufanya kazi kinaenda kukaa kwenye stoo,” anatahadharisha Profesa Janabi.

Anasema mlundikano huo ndiyo husababisha zaidi madhara kwa mwili wa binadamu kama vile kutengeneza vitambi, shinikizo la damu na matatizo ya moyo.

Profesa Janabi anashauri kuwa muda sahihi wa kula chakula ni kuanzia saa 12 jioni hadi saa 1:00 usiku, ikiwa ni saa chache kabla ya kwenda kulala.

HALI ILIVYO KITAIFA
Profesa Janabi anasema magonjwa ya moyo huchangia karibu asilimia 31 ya vifo vyote duniani na kwamba takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinabainisha kuwa kila mwaka, takribani watu milioni 18 hufariki dunia kutokana na maradhi hayo.

“Ni tatizo linaloonekana kuongezeka, takwimu zinaonyesha katika kila wanawake wanne na wanaume watano, mmoja ananakabiliwa na tatizo la shinikizo la damu,” anabainisha.

Anaongeza kuwa magonjwa ya moyo ni kati ya magonjwa yasiyoambukiza, ambayo kinga ni rahisi kuliko tiba, ndiyo maana WHO pamoja na Jumuiya ya Magonjwa ya Moyo Duniani baada ya kuona yanaongezeka, wakaamua kuanzisha Siku ya Moyo Duniani.

“Watu pia wanapaswa kuzingatia unywaji wa pombe kwa kiasi, kuacha uvutaji wa sigara, kula vyakula vinavyofaa, wazingatie kunywa dawa wanazoandikiwa (waliokutwa na matatizo haya) na wafanye mazoezi, wapunguze uzito uliopitiliza. Haya ni mambo ambayo yapo ndani ya uwezo wa mtu bila gharama,” anasema.

Mkurugenzi huyo anabainisha kuwa JKCI tangu mwaka 2015 ilipoanzishwa hadi sasa, tayari imeshaona takribani wagonjwa 350,000 huku 6,000 kati yao wakifanyiwa upasuaji.

“JKCI tupo mstari wa mbele kutoa elimu ili watu waepuke magonjwa haya,” anasema Profesa Janabi.

BP IKO JIRANI
Mtaalamu huyo anabainisha kuwa asilimia 70 ya wagonjwa wanaotibiwa JKCI, wanakabiliwa na tatizo la Shinikizo la Damu (BP).

Anasema takwimu zao zinaonyesha ndiyo tatizo linaloongoza kwa idadi kubwa ya wagonjwa katika taasisi hiyo tangu ilipoanzishwa rasmi mwaka 2015.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa JKCI, Samweli Rweyemamu, anasema wapo pia wengine wanaokabiliwa na tatizo la kuziba kwa mishipa ya damu inayosambaza damu kwenye moyo ambayo husababisha kifua kuuma.

“Kuna wengine wanaohitaji upasuaji na idadi inaongezeka kila siku. Kwa mfano, wale ambao mishipa ya damu inaziba, tunawazibua kwa upasuaji mkubwa au ule wa tundu dogo,” anasema Dk. Rweyemamu.

Anabainisha kuwa hadi Desemba mwaka jana, waliwachunguza karibu wagonjwa 1,000, ambao awali walikuwa wakipewa rufani ya kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Daktari bingwa huyo anasema kuwa kwa siku, huwa wanaona wagonjwa kati ya 300 na 400, hali inayoonyesha kwamba watu wenye matatizo ya moyo wanaongezeka nchini.

Dk. Rweyemamu anatoa mfano I got kwamba Wilaya ya Temeke kwenye Viwanja vya Zakheem walipima watu 100 na kati yao, asilimia 18 walikuwa na BP IS na wengine moyo umetanuka. Pia, 21 walionekana wana matatizo ya moyo.

Anasema pia walifanya kazi kama hiyo katika viwanja vya Mwembe Yanga kwa watu 150 na kati yao, asilimia 22 walionekana kuwa na maradhi ya moyo. Anasema kati ya hiyo asilimia 22, asilimia 19 walikuwa na shinikizo la damu la juu.

Anaongeza kuwa idadi hiyo inawezekana kuwa ni ndogo lakini utafiti uliofanyika Dar es Salaam, unaonyesha karibu asilimia 30 wana shida ya shinikizo la damu.

“Sasa ukiwa na shinikizo la damu ni ‘risk factor’ (ishara hatari) ya kuziba kwa mishipa ya moyo hatimaye utafika kwetu tukuzibue kwa vifaa maalum,” anasema Dk. Rweyemamu.

Anasema mtu akiwa na shinikizo la damu, moyo hutanuka na kuwa na dalili za kushindwa kufanya kazi, hivyo asilimia kubwa ya matatizo ya moyo kwa watu wazima yanaanza na presha.

Mratibu wa Tiba wa Manispaa ya Kinondoni kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo, Dk. Omary Mwangaza, anasema kipindi cha Julai na Agosti mwaka huu, katika vituo vya kutolea huduma za afya, waliibua wagonjwa wapya zaidi ya 600 wanaokabiliwa na magonjwa yasiyoambukiza.

“Shinikizo la damu na kisukari ni magonjwa yaliyokuwa yakiongoza kwa idadi kubwa ya wagonjwa, wagonjwa wote hawa tumewaingiza kwenye mfumo wetu wa matibabu,” anabainisha.

Kuwaelewa Madaktari,inahitaji akili ya ziada.
Mimi huwa sina imani nao kabisa,naona ni Watu waongo tu na wababaishaji na waizi katika maisha ya Binaadam

Hawa ni sawa na Wafanya biashara,lengo lao kuu pesa...ila wao pesa wanaipata kupitia mwili wa Binaadam na Viungo vyake
 
Sio tu maradhi ya moyo pia huipa SHIDA FIGO katika ufanyaji kazi yake
Kwa kushindwa kufanya kazi inavyopaswa
hvyo kuichosha
 
Wapo wengi pesa zinawatesa au kuteswa na wanaozitaka toka kwao. Ukiwa na pesa nyingi utanunua kila kitu, isipokuwa uzima, amani, utulivu na usalama. Shilingi maua tena yaua!

Hayo ulitoyataja si madhara ya pesa fikiria na waliokuzunguka nao wakawa na pesa zao nani atakuomba hizo zako?

Ngoja niweke sawa hapo kwa kusema hivi, Mkuu tutafute pesa ili tusije kuwa tatizo kwa wenye pesa
 
Wenye pesa hawafanyi mazuri tu na pesa zao, bali pia huzitumia kunyanyasa wengine. Ungejua kuwa ushindani wa wenye pesa na wanavyoumizana usingesema hayo.

Aidha, kama hujui, shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha kupindukia; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.
1 Timotheo 6:10

Kitu kizuri kuliko vitu vyote ikiwemo pesa, ni kuwa na utu. Ndio maana heshima ya mtu ni utu wake na si vitu vyake, zikiwemo pesa!
Hayo ulitoyataja si madhara ya pesa fikiria na waliokuzunguka nao wakawa na pesa zao nani atakuomba hizo zako?

Ngoja niweke sawa hapo kwa kusema hivi, Mkuu tutafute pesa ili tusije kuwa tatizo kwa wenye pesa
 
Wapo wengi pesa zinawatesa au kuteswa na wanaozitaka toka kwao. Ukiwa na pesa nyingi utanunua kila kitu, isipokuwa uzima, amani, utulivu na usalama. Shilingi maua tena yaua!
Hawajui kuzitumia!!! wazilete kwangu waone!!!!......yaani hizo hela zimepotea!! ni sawa na kuwa na mke mzuri km mie hujui kunitumia nikikuacha oooh!! mke wangu!!
 
Back
Top Bottom