Silivian
Member
- Nov 13, 2022
- 90
- 218
Ipo tafiti inasema mwanaume hutumia wastani wa masaa 7 kila mwaka kujificha chooni ili apate "Amani, Utulivu na Ukimya"
Tunapitia mengi sana badala ya kuendeleza hii kampeni mliyoificha kwenye utani wa "kila siku msisahau kumuogopa Mwanaume", mngetenga muda wenu kutuombea..
Dunia ni kama ina kiwango tulichoshindwa kufikia ukomo wake wa changamoto.. Kazini boss anakuhesabia siku kwamaana tayari kikao cha kufukuzwa kazi kimepata muafaka.. Baba mwenye nyumba anadai kodi yake mbele ya watoto tena kwa ukali usio mithilika.. Kijijini kile kitenge cha mama alichopewa kwenye kampeni za uchaguzi kimechakaa..
Baba anaumwa na shambani haendi tena.. Wadogo zetu wamekosa sare ya shule na madaftari.. hakuna future. Ghetto moja, masela kibao. Tunalala ili pambazuke, sio tupumzike. Mzigo wote upo kwetu, kosa ni kuja mjini kwa maelezo kuwa tumekuja kutafuta..
Maisha yetu ni kijiweni tu, ambapo hakuna cha maana zaidi ya mabishano ya mpira na siasa.Marafiki ukiwaambia huna, wanakuita fake friend au snitch. Wadada wa mjini usipotimiza mahitaji yao na upendo hupati tena. Ni kama biashara iliyokosa leseni tu.
Tuombeeni jamani,
Hivi hivi tulivyo, watu wana chuki
Huko vilingeni kuna majina mpaka ya mama zetu, tunarogwa sisi na ukoo mzima..
Ila sawa, msisahau kuwaogopa wanaume, kama mnavyoambiana na kucheka kwa kejeli.
Ni mtu gani mwenye uwezo wa kuishi na tabasamu mbele yako na kazi kafukuzwa bila wewe kujua na home hamlali njaa?
Ni kiumbe gani anaweza kucheka mbele yako, na wakati huo nyumba mnayoishi tayari benki inayowadai mkopo ishaipiga mnada?
Ni binadamu yupi anaweza kuishi na watoto uliomdanganya ni wake, bila kupunguza huduma?
Tulivyo wachache hivi na bado kuna wenzetu wameisaliti jinsia na kwenda kuolewa.
Dunia ina watoto sio rizki kibao.. Kuwa mwanaume ni kazi jama!
Endeleeni na utani wenu wa "Don't forget to fear men."
Mngejua tunayopitia, kila siku mngetupokea kwa magoti stendi kila tunapotoka vibaruani na majasho yetu.. Ni Mateso.
Ukitaka kukosana na wamama wa kibongo
Mseme vibaya MWAMPOSA
[emoji23][emoji23][emoji23]
Sent from my TECNO KE5 using JamiiForums mobile app