Mwanaume kuwa mbobezi wa mapishi kuliko mwanamke

SIPIYU30

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
1,621
2,015
Hii kitu inanifikirisha sana.
Katika maisha yangu nimeishi katika mapito ya kuhustle sana kwa mbinde mpaka nimetoka kimaisha.
Mara nyingi nimeishi maisha ya kujitegemea tangu utotoni.
Sasa nimejikuta najua mapishi mengi sana. Alafu hulka yangu huwa napenda kila ninachokifanya nifanye katika ubora uliotukuka. Nikiona siwezi kufanya kitu kwa ubora ninaotaka bora niache.

Sasa kwenye mapishi maisha yangu yamekuwa gumzo kwa akina dada wananikwepa sana.
Ikitokea akaja msichana kunitembelea kwangu basi menu nitakayopika kwanza hataamini macho yake kama ni mimi nimepika. Wengine mpaka wanakiri kusema siwezi kuwa naye kwa sababu nitakuwa nakosoa mapishi yake kila wakati. Mwingine anasema hatakaa anipikie maana hawezi kupika level yangu.

Sasa akina dada mnakwama wapi? Kweli nikukose kwa sababu nakuzidi kupika?
Kwani mnalelewa kwenye jokofu kiasi hata usiweze kupika?
Sio fresh, badilikeni buana
 
Ndio vzr ili akiwa na wewe a-step up her game kwenye cooking.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ila kupikiwa na mtu anaejua nini maana ya kukaa jikoni unaenjoy saaana,.hata mimi pamoja na ufundi wangu kuna mtu/watu wakinipikia nakifurahia chakula na nakula mpaka mwisho😋...

Hao uanaokutana nao hawajui kupika wanabaki kujishtukia tuu,kama wako tayari kujifunza wangekuelewa...au naww unawachamba sana kuwa hawajui kupika???😃
 
Umeandika pumba mwanamke mwenzangu
 
Pole sana aisee,.sio lazima tuelewane shogaa,.wewe mama debora mimi Mother Confessor hatuwezi fanana hata theluthi,. kama umeona pumba mie kwangu mchele..

Assalam alaykhum!!!

Kumbuka hujajiandikia wewe.
Umeandika ili watu wasome, na watu hao sio wewe bali ni sisi, sasa kama umetuandikia pumba lazima tukwambie!!
 
Kumbuka hujajiandikia wewe.
Umeandika ili watu wasome, na watu hao sio wewe bali ni sisi, sasa kama umetuandikia pumba lazima tukwambie!!
Hiyo ni comment sio THREAD,.jua hilo pia..halafu ni mawazo yangu,.wewe unaweza weka hayo yako ya maana dear..
 
Hiyo ni comment sio THREAD,.jua hilo pia..halafu ni mawazo yangu,.wewe unaweza weka hayo yako ya maana dear..

Kwahiyo comment huwa watu wanaandika ili wasome wenyewe ama watu wengine wasome. Point iko palepale. Umeandika pumba ingawa kwako unaona ni "mchele"
 
Kwahiyo comment huwa watu wanaandika ili wasome wenyewe ama watu wengine wasome. Point iko palepale. Umeandika pumba ingawa kwako unaona ni "mchele"
Kwani mwenzangu vipi mbona kama comment yangu inakuumiza sana kichwa,.kama imekuuma basi pole,.ila "hatuwezi fanana".
 
Hoa wadada wanaokutembelea bado hawajakomaa kiakili
hawajui nini maana ya maisha

kwani nani alizaliwa anajua??
kila kitu tunajifunza hapahapa duniani

Au wao wanataka waendelee na ujinga hawataki kujifunza?

Wanapaswa kuyatazama maisha
kwa jicho la tofauti sana si kwa mtazamo huo

kujifunza kitu kipya ni muhimu ktk maisha

"Never be fenced in"-usikariri tu ulivofundishwa kupika na bi mkubwa

Dada zetu wakiwa na nia wanaweza kuwa ma expert ktk mapishi coz siku hizi kuna makala mbalimbali hutoa elimu juu ya mapishi kupitia social media kama vile redio,tv,machapisho mbalimbali,youtube channels,etc

Tatizo hao waliokutembelea hawajafikiria tu nje ya box

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom