Tuache ushamba, kujifunga kitenge au kanga kiunoni, wakati wa kwenda kuoga wala siyo ushamba. Maeneo ya pwani tunakabiliwa na joto, kipindi kirefu cha msimu kuliko baridi, hivyo tunajifunika nguo nyepesi kanga au kitenge. Na wanaojifunga hivyo wengi ni wanaume, walio owa nasisitiza walioa, na wengi wanaishi maisha ya chini kiuchumi.
Huko kwenu kama mnatoka na shuka au blanketi kwenda kuoga, hatuwapangii, tokeni tu. Ila vazi la kitenge si ndo tulichagua Tanzania, kama vazi la Taifa, kuvaa shati la kitenge kwa anaelewa siyo tatizo wala barakoa ya kitenge, na kwa mwanamme kitenge kujifunga kiunoni. Maana hakuna mwanamke anaejifunga kitenge kiunoni, hapo ndipo tofauti inapo onekana.