Mwanaume Kumpenda Mwanamke Maana Yake Nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanaume Kumpenda Mwanamke Maana Yake Nini?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by RaiaMbishi, Feb 14, 2012.

 1. RaiaMbishi

  RaiaMbishi JF-Expert Member

  #1
  Feb 14, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 252
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Nimekuwa najiuliza, wanaume tunaposema tunampenda msichana/mwanamke, tuna maana gani hasa? Nimebaini kwamba wanaume tuna maana nyingi sana juu ya hili. Kwa mfano, je ukiambiwa uchague kitu kimoja tu kati ya hivvo hapa chini, halafu mwanamke utakayemchagua utapelekwa nae kwenda kuishi katika kisiwa cha mbali na kukaa nae huko kwa miaka mitatu bila ya wewe kukutana na mwanamke mwingine katika kipindi chote hicho, utapendelea mwanamke huyo awe na sifa zipi kazi ya hizi? Kumbuka, ukichagua sifa moja kati ya hizi 20, ina maana kwamba, sifa nyingine 19 zilizobakia, mwanamke uliyemchagua hatokuwa nazo. Pia assumption ni kwamba wote mtapimwa ukimwi na kuwa swaaaafi kabisa.


  1. Mwili/umbile kama vile saizi ya mwili, urefu/ufupi, matiti na booty?
  2. Mvuto wa sura/sura ya kuvutia?
  3. Ngozi uipendayo wewe - mweupe/mweusi/maji ya kunde?
  4. Tabia Nzuri/heshima iliyotukuka?
  5. Manyago mazuri Kitandani na anayetoa huduma zote unazohitaji?
  6. Mwanamke mselamsela?
  7. Mwanamke mcheshi, mzungumzaji, mchekeshaji/kampani?
  8. Mwanamke mkimya na asiyekuwa mzungumzaji?
  9. Anayependa Kudeka?
  10. Asiyekuwa na tamaa/gharama?
  11. Anayejitegemea kiuchumi/mwenye ajira au biashara yake?
  12. Anayejua kutunza mwanaume kwa gharama zote?
  13. Anaetoka familia Bora/wenye mali kwao?
  14. Aliye na elimu nzuri/ana Akili/intelligent?
  15. Aliye wahi kuishi nje ya nchi kwa muda mrefu?
  16. Ambae ametokea kijijini na asiyejua maisha ya mjini?
  17. Mwanamke mwenye umri mkubwa sana zaidi yako/sugar mami?
  18. Mwanamke bikra?
  19. Mwanamke ambae ameshatumika sana na kaamua kutulia?
  20. Mwanamke jike dume/tom boy?

  Kumbuka, unatakiwa kuchagua sifa moja tu, na ukichagua hiyo sifa, nyingine ina maana huyo mwanamke automatically hana sifa zilizosalia. Na utaishi nae kwenye kisiwa mkiwa wawili tu bila ya kukutana na wanawake wengine kwa miaka mitatu, na mtakuwa mnaletewa mahitaji yenu kwa helikopta pale tu mtakapokuwa mnahitaji kitu. Jitahidi kutoa maelezo kwanini umechagua sifa uliyoichagua.


  Nia yangu ni kujaribu kubaini, je, kwa mwanaume walio wengi, ipi ni sifa muhimu zaidi? Mimi nimechagua sifa namba '14', najali zaidi mwanamke kichwa, akikosa mengine ntamzoea tu mapungufu yake, na mambo yatakuwa swaaaaafi.
   
 2. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #2
  Feb 14, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Ngoja kwanza nikutakia Valentine njema kabla sijaja kwenye huu uzi!!

  [​IMG]
   
Loading...