Mwanaume kumgharamia mwanamke(kuhonga) ni amri ya mwenyezimungu,ni haki yao kuhongwa

mwekundu

JF-Expert Member
Mar 4, 2013
21,859
19,700
MWANAUME KUMGHARAMIA MWANAMKE(KUHONGA) NI AMRI YA MWENYEZIMUNGU
Kutokana na ugumu wa maisha wanaume tumegeuka kuwa walalamikaji linapofika suala la mpenzi wake kuwa very dependant sana kwako na badala yake tumewageuza na kuanza kuwaita majina(inferiority complex) kama vicheche,wachunaji,ruba hata muda mwingine kuwaita Malaya n.k
Na wao kwa kutokufahamu au kutokana na pressure kutoka kwa wanaume ya kuogopa kusemwa vibaya tumepachikwa majina na kuanza kuitwa Mabuzi,ATM n.k lakini ukweli wa mambo ulishawekwa/ulishapangwa bayana na Mkuu wa viumbe vyote,Muumbaji (Creator),Mwanasheria Mkuu,Mtabiri Mkuu Mwenyezimungu by the way dini zote uumbaji na mwanzo wa binadamu unatoa maelezo yanayofanana(katika andishi langu napenda nitumie reference ya biblia)
Mwenyezimungu aliitoa amri hii ukisoma Biblia GENESIS(MWANZO) aya 3:1-24 hapo ndipo utabiri na utaratibu wa miasha ya binadamu ,ulipangwa upya mara baada ya Hawa kushawishiwa na Nyoka(shetani) kula mti wa tunda la katikati naye akamgawia Adam ale pia , ndipo walipoanza kujua mema na mabaya katika bustani ya Eden
Nanukuu katika aya ya 3 mstari wa 16 GENESIS(mwanzo) 3:16 mwenyezimungu anatoa assignment/task "Akamwambia mwanamke hakika nitakuzidishia uchungu wako,na kuzaa kwako,kwa uchungu utazaa watoto na tamaa yako itakua kwa mumeo,naye atakutawala" -(kumbuka wenzetu hawajawahi kulalamika hata siku moja kuhusu kusaidiwa uchungu,kuzaa na tunawatawala they know its NATURE/amri kutoka kwa Mwenyezimungu)NB;mtawala siku zote ndo mpangaji wa mambo yote refer serikali katika suala la budget ,budget kama haitoshi/finyu wananchi watalalamika bila kujua fedha utapata vipi?

Ndipo anapomgeukia Mwanaume na kumpa adhabu/assignment-basic task(ambayo wengi wetu tunalalamika) yake Genesis(mwanzo) 3; 17-19 "akamwambia Adamu kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako ,ukala matunda ya mti ambao
nilikukataza,ardhi imelaaniwa kwa ajili yako;kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako;18 michongoma na miiba itakuzalia nawe utakula mboga za kondeni 19;kwa jasho la uso wako utakula chakula hata utapoirudia ardhi ambayo katika hiyo ulitwaliwa"

Katika maelezo hayo hapo juu utagundua kuwa shughuli za ufanikishaji wa kimaisha ya binadamu(MAJUKUMU) katika ngazi ya familia zilishagawanywa(assigned) na Mwenyezimungu katika makundi mawili yaani ya kiuchumi ambayo alikabidhiwa mwanaume so we are responsible to provide Money,rent,shelter ,clothing and other expenses like shopping,Manicures,pedicures Voucher,M-pesa,Tigo-pesa etc na yale ya Uzazi kama kuzaa ,kutunza na kulea watoto wa
familia alikabidhiwa mwanamke

Hivyo basi sio busara na ni kinyume na mafundisho ya imani ya dini mwanaume kulialia pale your girlfriend,wife,Mlupo etc anapodai haki yake ya kutunzwa na kukukumbusha umgharamie kwa sababu wewe ni mtawala wake tena unapaswa utii amri ya mwenyezimungu ambayo aliitoa Hapo MWANZO 3:1-24 ,Na hata upande wa UISLAM umeeleza bayana mwanamke akishaolewa hata kama anakazi she isn't responsible katika gharama zozote za maisha(hata kuosha vyombo tu) labda aamue mwenyewe ,jukumu lake yeye ni uzazi na kulea(basic task zile…..)

Nawasilisha tulijadili
,changamoto zinakaribishwa pia
copy to watu8(ulinikumbusha majukumu finally nimechimba nimepata ukweli-kulialia hakutakiwi) Mentor Kaizer Mndengereko isumbiro Nicas Mtei Mashaxizo Madame B(mama la mama) Lady doctor Munkari charminglady lara 1(igweeeeeeee) angelita Bishanga Judgement jamiif Malaika mimi KakaKiiza Asprin Kongosho Zinduna miss neddy miss chagga miss strong Preta Mshinga ,mkuu zinc(umeitoa ile unatakiwa uigharamie)@Eiyer Tutor B King'asti BADILI TABIA TIMING Sangarara Heaven on Earth Rogie kobun Mapi Mtambuzi Bujibuji tinna cute Mzee Kipaji Halisi Smile mwallu @Ruttashobolwa waiting for your facts brother etc etc
 
tatzo umekurupuka kutoa threads bila kutumia mawazo chanya.mkeo pekee ndo unaweza beba majukumu yote na siyo mwanamke unayekutana naye ghafla tu useme uwe unamgharamia kwa lipi ? anakaa kwa baba yake na mama yake .ULITAKIWA USEME KUOA KUNA MAJUKUMU AMBAYO HAYAKIMBIWI NA HAKUNA MWANAUME ANAYEPINGA MAJUKUMU YA NDOA
 
kinachowaunganisha ni nini?hapo ndo ilipo haki yake
 
Majibu mazuri hapo juu - LIKE; Kwa nyongeza, wao wenyewe (wanawake) wanataka haki sawa labda ukutane na mwanamke mwenye mlengo usio wa kimapinduzi, wao wanasema "WANAWAKE TUKIWEZESHWA TUNAWEZA" hawasemi wakiwezeshwa na nani ndo waweze, Binafsi najua mwezeshaji ni mmoja tu - MUNGU.
 
MWANAUME KUMGHARAMIA MWANAMKE(KUHONGA) NI AMRI YA MWENYEZIMUNGU
Kutokana na ugumu wa maisha wanaume tumegeuka kuwa walalamikaji linapofika suala la mpenzi wake kuwa very dependant sana kwako na badala yake tumewageuza na kuanza kuwaita majina(inferiority complex) kama vicheche,wachunaji,ruba hata muda mwingine kuwaita Malaya n.k
Na wao kwa kutokufahamu au kutokana na pressure kutoka kwa wanaume ya kuogopa kusemwa vibaya tumepachikwa majina na kuanza kuitwa Mabuzi,ATM n.k lakini ukweli wa mambo ulishawekwa/ulishapangwa bayana na Mkuu wa viumbe vyote,Muumbaji (Creator),Mwanasheria Mkuu,Mtabiri Mkuu Mwenyezimungu by the way dini zote uumbaji na mwanzo wa binadamu unatoa maelezo yanayofanana(katika andishi langu napenda nitumie reference ya biblia)
Mwenyezimungu aliitoa amri hii ukisoma Biblia GENESIS(MWANZO) aya 3:1-24 hapo ndipo utabiri na utaratibu wa miasha ya binadamu ,ulipangwa upya mara baada ya Hawa kushawishiwa na Nyoka(shetani) kula mti wa tunda la katikati naye akamgawia Adam ale pia , ndipo walipoanza kujua mema na mabaya katika bustani ya Eden
Nanukuu katika aya ya 3 mstari wa 16 GENESIS(mwanzo) 3:16 mwenyezimungu anatoa assignment/task "Akamwambia mwanamke hakika nitakuzidishia uchungu wako,na kuzaa kwako,kwa uchungu utazaa watoto na tamaa yako itakua kwa mumeo,naye atakutawala" -(kumbuka wenzetu hawajawahi kulalamika hata siku moja kuhusu kusaidiwa uchungu,kuzaa na tunawatawala they know its NATURE/amri kutoka kwa Mwenyezimungu)NB;mtawala siku zote ndo mpangaji wa mambo yote refer serikali katika suala la budget ,budget kama haitoshi/finyu wananchi watalalamika bila kujua fedha utapata vipi?

Ndipo anapomgeukia Mwanaume na kumpa adhabu/assignment-basic task(ambayo wengi wetu tunalalamika) yake Genesis(mwanzo) 3; 17-19 "akamwambia Adamu kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako ,ukala matunda ya mti ambao
nilikukataza,ardhi imelaaniwa kwa ajili yako;kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako;18 michongoma na miiba itakuzalia nawe utakula mboga za kondeni 19;kwa jasho la uso wako utakula chakula hata utapoirudia ardhi ambayo katika hiyo ulitwaliwa"

Katika maelezo hayo hapo juu utagundua kuwa shughuli za ufanikishaji wa kimaisha ya binadamu katika ngazi ya familia zilishagawanywa(assigned) na Mwenyezimungu katika makundi mawili yaani ya kiuchumi ambayo alikabidhiwa mwanaume so we are responsible to provide Money,rent,shelter ,clothing and other expenses like shopping,Manicures,pedicures Voucher,M-pesa,Tigo-pesa etc na yale ya Uzazi kama kuzaa ,kutunza na kulea watoto wa
familia alikabidhiwa mwanamke

Hivyo basi sio busara na ni kinyume na mafundisho ya imani ya dini mwanaume kulialia pale your girlfriend,wife,Mlupo etc anapodai haki yake ya kutunzwa na kukukumbusha umgharamie kwa sababu wewe ni mtawala wake tena unapaswa utii amri ya mwenyezimungu ambayo aliitoa Hapo MWANZO 3:1-24 ,Na hata upande wa UISLAM umeeleza bayana mwanamke akishaolewa hata kama anakazi she isn't responsible katika gharama zozote za maisha(hata kuosha vyombo tu) labda aamue mwenyewe ,jukumu lake yeye ni uzazi na kulea(basic task zile…..)

Nawasilisha tulijadili
hili
copy to watu8(ulinikumbusha majukumu finally nimechimba nimepata ukweli-kulialia hakutakiwi) Mentor Kaizer Mndengereko isambwiro Nicas Mtei Mashaxizo Madame B(mama la mama) Lady doctor Munkari charminglady lara 1(igweeeeeeee) angelita Malaika mimi KakaKiiza Asprin Kongosho Zinduna miss neddy miss chagga miss strong Preta Mshinga ,mkuu zinc(umeitoa ile unatakiwa uigharamie) Rogie Mtambuzi Bujibuji tinna cute Mzee Kipaji Halisi Smile mwallu @Ruttashobolwa waiting for your facts brother etc etc
malalamiko yako mengi na hayafanani kabisa.

wanaume wengi hawalalamiki kutaka kukwepa majukumu yao,wanaume wengi wanapenda kuonekana wanajali sana.

tatizo linakuja kuwa badala ya majukumu ya kawaida na ya lazima sasa yamekuwa ni majukumu ya starehe na mambo mengine ambayo hayana maana sana katika maisha ya mwanadamu na kibaya zaidi ukishindwa kutekeleza hayo ya starehe ujue unanyang'anywa mke ama mchumba ama demu kisa anataka vitu vidogovidogo.

mfano.
leo gharama za mwanamke kutunza nywele ambazo nazo si zake ni kubwa kushinda gharama ya nguo alizovaa, ni kubwa kushinda bajeti ya chakula nyumbani.

kwa nini tusilalamike wakati hayo si mambo ya msingi na sudhani kama ni sahihi kusema ni mgawanyo wa majukumu toka kwa Mungu.

mwanaume unaweza kumpa mpenzi wako hela ya kununua unga,mafuta ya kupikia,mafuta ya taa,mchele,ngano,jiko la gesi pia na nguo nzuri nk lakini kama usipompa hela mara kwa mara za kwenda saloon kununu nywele bandia,kwenda saloon kusukwa hizo nywele,usipompa hela ya kununua simu za smartphone ujue yote unayofanya ni kazi bure.

na hapo si kwamba hukutimiza majukumu ya kula kwa uchungu,umekuwa umetimiza majukumu hayo lakini unaelemewa na majukumu yanapoingia mambo ya starehe.

nywele mama zetu walifuga za kwao,wakazitunza kwa gharama ndogo,walisuka kwa nywele zao halisi lakini leo ni wachache tu wanakubali kutumia nywele zao halisi na hapa ndio tunasema inferiority complex kwa maana hawajiamini
 
Kumbuka imeandikwa kwa mke na siyo hawara au girl frend na sidhani kama kuna mwanaume analalamika kuwa maisha magumu pale mke wake anapoomba pesa ya matumizi, kumbuka hapo mwanamke unapompa hela siyo ya kwake ni ya familia ukitoa hela utakuta chakula ndani na wewe utakula watoto watakula kama mnao hata ndugu wakija nadani hapakuwa na njaa,akivaa akapendeza ndo raha ya mke hiyo na mungu alikusudia hivyo hata akizaa kwa uchungu anajua atahudumiwa,atafarijiwa,hata mue jasho linapomtoka atapewa faraja na kutiwa moyo na mke wake maana wote walitende dhambi pamoja kwa kushawishiana,sasa shida inakuja kwa huyu girl frend au hawara ndiyo malalamiko yanapotokea huyu yuko kwa ajiri ya matumizi yake tu,na demand lazima ziwe nyingi maana anakuwa amekufanya source ya income yake, ukuona una girl frend amekuomba hela umempa then baadaye anakuletea japo hata boxa tu shukuru sana!
 
Mmmmmmmmmh!

NIAKULA VYA WATU WITH PLESURE!!!!!!!!!!!! Sina wasi wasi mie!
 
Majibu mazuri hapo juu - LIKE; Kwa nyongeza, wao wenyewe (wanawake) wanataka haki sawa labda ukutane na mwanamke mwenye mlengo usio wa kimapinduzi, wao wanasema "WANAWAKE TUKIWEZESHWA TUNAWEZA" hawasemi wakiwezeshwa na nani ndo waweze, Binafsi najua mwezeshaji ni mmoja tu - MUNGU.

mkuu tumepewa utawala(serikali/mamlaka) Genesis 3;16 hivo basi tusitumie nafasi yetu vibaya-remember elements of good governance including caring and sharing
 
Kumbuka imeandikwa kwa mke na siyo hawara au girl frend na sidhani kama kuna mwanaume analalamika kuwa maisha magumu pale mke wake anapoomba pesa ya matumizi, kumbuka hapo mwanamke unapompa hela siyo ya kwake ni ya familia ukitoa hela utakuta chakula ndani na wewe utakula watoto watakula kama mnao hata ndugu wakija nadani hapakuwa na njaa,akivaa akapendeza ndo raha ya mke hiyo na mungu alikusudia hivyo hata akizaa kwa uchungu anajua atahudumiwa,atafarijiwa,hata mue jasho linapomtoka atapewa faraja na kutiwa moyo na mke wake maana wote walitende dhambi pamoja kwa kushawishiana,sasa shida inakuja kwa huyu girl frend au hawara ndiyo malalamiko yanapotokea huyu yuko kwa ajiri ya matumizi yake tu,na demand lazima ziwe nyingi maana anakuwa amekufanya source ya income yake, ukuona una girl frend amekuomba hela umempa then baadaye anakuletea japo hata boxa tu shukuru sana!

uchumba,u girlfriend is a way to last stage ya Marriage
 
well said my dear!

usemayo ni kweli mwekundu
wengi huwa wanasahau hilo agizo
wanatamani kila kipatikanacho kiwe pasu wanasahau kuwa mwanamke ameshatimiza wajibu wake wa kuzaa kwa uchungu na ataendelea na wajibu wake wa kuhakikisha watoto wanakuwa katika maadili mema

kuna mmoja amesema et hayo majukumu yatimizwe kwa mke tu
je huyo binti ulienae sasa ambaye hujamuoa ni nani yako si mpenzi ukishataja neno MPENZI lazima umtunze hata kama hujamuoa hii itamuondelea mashaka binti juu yako na itamuonyesha kuwa wewe ni REAL MAN ambae utaweza kutimiza majukumu yako hata ndani ya ndo MAANA DALILI YA MVUA NI MAWINGU
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom