figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,485
Heshima kwenu wakuu,
Wanawake siku hizi wameibua tabia ya kutuonea wanaume. Utakuta anataka kukukunja au mara akupige kofi eti ana hasira, ukifanya hivyo unakosea.
Wengine wanajifanya kumpiga mwanaume kwa maneno makali na matusi, ukifanya hivyo utaletewa nyumba ndogo.
Nini cha kufanya?
Kwanza tambua ukiwa na mwanaume, haina tofauti na kuwa na mtoto mdogo. Kwa ufupi wanaume ni kama watoto tu, wanapenda kusikilizwa na kudekezwa kwa kukandwa kandwa viungo vya mwili.
Hata pale anapokuudhi, usimuonee aibu kumpiga kwa Boxer ya kuvaa ndani au Koti kubwa na tai. Nakuhakikishia utapendwa hadi utakuja kuuliza ni aina gani ya limbwata umempa mume wako.
Nawatakia Jumamosi njema.
Salamu nyingi sana kutoka kwa My wife Heaven on Earth. Anawasalimia sana na anasema kawamiss. Anawapenda pia