Mwanaume' - Aukata Mdomo Wa Mkewe ili asiweze kubusu tena

lutayega

JF-Expert Member
Feb 29, 2012
1,288
552
Daktari huyo bingwa mwenye umri wa miaka 52 aliwaambia polisi kuwa alichukua uamuzi wa kuukata mdomo wa mke wake mwenye umri wa miaka 32 kwakuwa mke wake huyo alikuwa aking'ang'ania kudai talaka.

Daktari huyo alichukua uamuzi huo baada ya mkewe kurudi nyumbani kutoka kwenye tripu ambayo inahisiwa alienda na mpenzi wake wa nje ya ndoa.

"Sikutaka kumuua, nilitaka ataabike maisha yake yote kwa haya aliyonifanyia", alisema daktari huyo bingwa anayeheshimika sana katika tafiti za kitabibu katika taasisi ya Karloinska Institute ya jijini Stockholm.

"Awali nilichukua kisu lakini hakikuwa na makali ya kutosha ndipo nilipochukua kisu chenye ncha kali kinachotumika kwenye upasuaji mahospitalini".

Daktari huyo aliongeza kuwa mkewe alikuwa macho wakati wa shambulio hilo na alimwambia kuwa anataka kumuadhibu sio kumuua.

"Niliuvuta mdomo wake na kuukata kwa kisu na kisha niliutafuna tafuna", alisema daktari huyo katika mahojiano na polisi.

"Awali nilifikiria kuwa kwa kuukata tu mdomo wake, madaktari wanaweza wakauunganisha tena ndipo nilipoamua kuutafuna na kuumeza ili kuzuia kutokea kwa hali hiyo", aliongeza dakatari huyo.

Magazeti ya Sweden yalisema kuwa daktari huyo aliwaambia polisi kuwa uamuzi huo aliuchukua ghafla na kuamua kuondoa udhia.

"Mimi ni mwanasayansi na nina IQ kubwa sana, nina uwezo wa kutatua matatizo ndani ya sekunde chache", alijigamba daktari huyo ambaye jina lake liliwekwa kapuni.



 


"Mimi ni mwanasayansi na nina IQ kubwa sana, nina uwezo wa kutatua matatizo ndani ya sekunde chache", alijigamba daktari huyo ambaye jina lake liliwekwa kapuni.




Ana IQ kubwa ya ukichaa......
 
madaktari wote akili zao na maamuzi yao yanafanana.

...ndio maana walijitahidi kumsaidia mama yako akuzae wewe salama toka tumboni mwake.
...wakahakikisha unapata chanjo zote stahili.
...lakini leo unawaona wapumbavu, haya bwana.
 
...ndio maana walijitahidi kumsaidia mama yako akuzae wewe salama toka tumboni mwake.
...wakahakikisha unapata chanjo zote stahili.
...lakini leo unawaona wapumbavu, haya bwana.
saloot muheshmiwa!!
narekebisha kauli kidogo,asilimia kubwa ya madoctor ndio hivyo kama nilivyosema awali!nikimaanisha 92%
 
Back
Top Bottom