Mwanaume aua familia yake kisa wivu wa mapenzi

mtu watu

JF-Expert Member
Dec 10, 2017
2,123
1,616
Mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Ammy Lucas Lukule ambaye ni Mhasibu wa Hospitali ya Rufaa Mbeya, amechukua uamuzi wa kuua familia yake kutokana na wivu wa mapenzi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Benedict Kitalika amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la mauaji, na kusema kuwa muuaji alifanya tukio hilo usiku wa jana huko nyumbani kwao Kimara jijini Dar es salaam, na kisha kutokomea kusikojulikana.

“Ni kweli mwanaume mmoja ambaye anafanya kazi ya uhasibu katika hospitali ya rufaa ya Mbeya, aliyejulikana kwa jina la Ammy Lucas Lukule, ameua mke, mtoto na shemeji yake, inasemekana kulikuwa na ugomvi ambapo mwanaume alikuwa akimtuhumu mkewe kuwa huyu mtoto mdogo sio wake na anajihusisha na mapenzi na wanaume wengine, hivyo aliamua kuwaua kwa jembe na kukimbia”, amesema Kamanda Kitalika.

Kamanda Kitalika ameendelea kwa kueleza kuwa baada ya kufanya tukio hilo marehemu aliacha ujumbe kuwa polisi wasihangaike kwani yeye ndiye kafanya mauaji.
Jeshi la Polisis limesema taarifa za tukio hilo walizipata kutoka kwa majirani baada ya kugundua hakuna dalili ya kuwepo watu kwenye hiyo nyumba na kuanza kuchunguza, ndipo walipogundua hayo na kuita polisi kuvuja mlango.

Waliouawa kwenye tukio hilo wametajwa kuwa ni Upendo Lukule ambaye ndiye mke, Magreth Samuel ambaye ni shemeji mtu na mtoto mdogo ambaye umri wake ni chini ya mwaka mmoja.
 
Ila wanawake wa miaka hii ni majeuri na vichwa ngumu.

Mimi ninamlaumu sana huyu jamaa.

Ila wanawake jerekebisheni, Uwezi kumwambia Mume wako, kwamba kuna wanaume tele huko mitaani halafu unakuja na kimimba cha mashaka mashaka kwa mume wako.
 
Amefanya uamuzi mgumu sana, tusipende kuwachunguza wenzi wetu na watoto wetu, hata yeye huenda sio wa babake fikria mzee yule angechukua uamuzi kama huo wake.
 
Angeshauriwa vizuri, wangepata vipimo vya DNA na shida ingekuwa imetatuliwa. Hivi hawa vijana wa siku hizi wamelelewa wapi? Mbona wanashindwa kutatua changamoto ndogo ndogo tu kama hizi?


Baba anafanya kazi Mbeya, mama anakaa Dar, usaliti utakosekanaje hapo sasa? Maana ya ndoa ni kuishi pamoja...
 
Angeshauriwa vizuri, wangepata vipimo vya DNA na shida ingekuwa imetatuliwa. Hivi hawa vijana wa siku hizi wamelelewa wapi? Mbona wanashindwa kutatua changamoto ndogo ndogo tu kama hizi?


Ukipima Dr akaona ni -ve akaona hutaweza kustahimili majibu unaambiwa +ve ni wako huyoo
Unaseli zako zote.


Lasi hivyoo mauaji na ndoa kuvunjika hakutaisha.

Watoto wengi sana tunalelea sio wakwetu.
 
Dah inatia uchungu sana kwa waliopetezewa uhai wao.
Mbeya sijui kuna nini maana ukatili ndio nyumbani kwake kule khaaa.......!
 
Mapenzi yana nguvu sana sana na wanawake huwa wanarahisisha sna mambo
Embu fikiria wakati mwingine maisha ni magumu alafu unamsingizia mtu mimba analea mimba mpaka mtoto labda miaka mitatu alafu anakuja kujua mtoto si wake
Ukiwaza vizuri inaumiza sana sana

Kama mimi nilikuwa na mpenzi wangu aliwahi kuja kukaa kwangu alikuwa anafuatilia mambo ya kazi alikaa kama mwezi mmoja na nusu hivi wakati anakaribia kuondoka alijigundua kuwa ana mimba
Nilimuuliza una uhakika ni ya kwangu astaajabu hilo swali lakini lengo lilikuwa ni kupata uhakika kutoka kwake kwa kuwa hawa watu sio wa kuamini sana
Alinijibu ni yakwangu ndio
,nilichomwambia ni kwamba kama mimba ni yakwangu niko tayari kumlea mwanangu na sio yakwangu asiogope kuniambia mapema tujue tunaachana vp
Mpaka akawa kanuna

Usijaribu kumwambia mtu mwingine kuwa una mimba yake mi sitaki migogoro na huyo mtoto
Imeenda imeenda kaenda kwao kakaa kama wiki mbili akawa ananipigia sm mara naumwa ukucha mara kidole mara naumwa kiuno mara chini ya kitovu
Siku moja nikaota ndoto kuwa mimba inetolewa nilivyoamka nikauliza nkapiga cm nikauliza vipi unaendeleaje akaniambia poa ila tumbo bado linasumbua nikamwambia fanya ufanyavyo usitoe hiyo mimba akasema poa

Baada ya kama siku mbili napigiwa simu kwa namba yake naambiwa huyu mtu anaumwa na hawezi hata kuongea tatizo ni tumbo nikaishiwa nguvu nikajua basi tena ile ndoto ndio inaenda kutimia
Kesho yake jion kapiga sm yeye kaniambia mimba imeharibika na amesafishwa
Roho iliuma sana nikaona hili ni picha tu nimechezewa!
Nikaona poa nikawa simzingatii sana

Imeisha kama miezi miwili tangu hilo tukio nikaona picha ya jamaa mmoja fb ambaye niliwahi kuiona picha kama hiyo kwenye watsp ya dem wangu nikamuadi nikamtumia sms
Kesho yake nikaona yuko online tukaanza kuchati sana mpaka akaniambia yule ni demu wake na mi nkamwambia pia akaniuliza vp alishawahi kukwambia kuwa ana mimba nikamwbia ndio na nikamuelezea ilivyokuwa kuwa
Na yeye akanielezea hivyo kwamba na yeye

Alitoa vitisho vya aina yake nikagundua kumbe ndio maana ile mimba ilitolewa na zile za kuumwa ilikuwa ni kutafuta sababu tu ya kuitoa mimba
Imenisikitisha sana hiyo na isingekuwa vile huenda yangekuja kutokea kama ya huyo jamaa wa kimara



Wanawake msiwe kama hivyo jitahidini kusema ukweli wakati mwingine sio kila jambo unaweza kudanganya madhara huwa ni makubwa zaidi
 
Nyie msiwalaumu wanaume me naandika ujumbe uu nikiwa hospital nimechomwa kisu na Mke wangu
IMG_20180104_193343.jpg
kisa nimeoji kwann kachelewa kurud nyumban
 
Back
Top Bottom