Mwanaume apigwa na mkewe

Exaud J. Makyao

JF-Expert Member
Nov 30, 2008
1,518
22
Mwanaume mmoja nchini Kenya ambaye ni kiongozi wa chama cha siasa cha NEW FORD KENYA amepokea kipigo kikubwa kutoka kwa mkewe hadi akalazwa hospitali.
BAADA YA purukushani kubwa, Bwana Robert alipigwa kisu shingoni na mkewe baada ya ugomvi nyumbani kwao.
Kisa hiki kimeripotiwa polisi hivyo Robert anataka mkewe achukuliwe hatua ya kisheria.
Hii imekaaje?

Wives are now beating their husbands in Kenya.

Yes, a significant number of Kenyan men are being battered by their spouses - to the extent of seeking medical attention.
A study carried out by three universities and published in the reputable British Medical Journal of Medicine seems to give credence to claims by a lobby group claiming that about 1.5 million men in Kenya are battered by their wives.
While agreeing with the lobbyists that there is significant violence against men, the study, however, says that men are the main perpetrators of domestic violence and blames alcohol for most of the cases.
The Kenya Demographic and Health Survey of 2003 claimed that more than half of all women in their 30s have experienced domestic violence inflicted by their spouses and cited drugs and alcohol as the main inducers.
Published in March and carried out by Maseno University and the US universities of Brown and Indiana, the new study says that while men still lead in spousal battery, women are giving back almost half of what they get.
The study was carried out at a rural setting in Mosoriot, a small town close to Eldoret. It says that although more women visit the local health centre with injuries caused by their spouses, a significant number of men also do.
In a study that covered 562 violent injury patients between 2002 and 2004 at the Mosoriot Health Centre, more women than men complained of spousal assault.
"Men and women were equally likely to suffer violent injuries, however, women were more likely to suffer injury from domestic violence at about seven per cent compared to about 4.7 per cent for men," it says.
According to another study carried out by the University of South Carolina in the US, women and men perpetrate equivalent levels of physical and psychological aggression, but evidence suggests that men perpetrate sexual abuse, coercive control and stalking more frequently than women and that women are much more frequently injured during domestic violence incidents.
Meanwhile, the government has announced plans to carry out national campaigns on domestic violence in the wake of reports that men are abused by their wives.
Additional reporting by Benjamin Muindi
 
Last edited:
Ukatili majumbani hauwaathiri wanawake na watoto tu.Inasemekana pamoja na kwamba nyumbani ( home) panadhaniwa kuwa mahali pa salama na amani - hakuna mahali hatari kama hapa! Hii ni kwasababu dola haiingilii kati kupeleleza kinachoendelea ndani ya nyumba za watu au familia.Watu wanapigana, wanaumizana na kusameheana kimyakimya.Haijalishi mpigwa ni mwanamke, mtoto au mwanaume.Tena ni hatari zaidi kwa mwanaume maana jamii imeshapitisha kuwa ni aibu mwanaume kukubali kapigwa na mkewe! Mimi binafsi namwona huyu bwana ni shujaa kwa kile kitendo cha kumshtaki mkewe na kutaka achukuliwe hatua stahiki.
Wanaume mnaopigwa na wake/wapenzi wenu jamani jitokezeni kabla makubwa hayajawakuta
 
Mwanaume mmoja nchini Kenya ambaye ni kiongozi wa chama cha siasa cha NEW FORD KENYA amepokea kipigo kikubwa kutoka kwa mkewe hadi akalazwa hospitali.
BAADA YA purukushani kubwa, Bwana Robert alipigwa kisu shingoni na mkewe baada ya ugomvi nyumbani kwao.
Kisa hiki kimeripotiwa polisi hivyo Robert anataka mkewe achukuliwe hatua ya kisheria.
Hii imekaaje?

Duh, inapokuja kupigana kwa kutumia silaha hapo ni hatari sana. Sitaki kufikiria kama kungekuwa na bastola/bunduki karibu ya huyo mwanamke! Huyo mwanamke amepoteza uhalali wa kuwa mke!
 
Duh, inapokuja kupigana kwa kutumia silaha hapo ni hatari sana. Sitaki kufikiria kama kungekuwa na bastola/bunduki karibu ya huyo mwanamke! Huyo mwanamke amepoteza uhalali wa kuwa mke!
SMU,
Ugomvi wa namna hii ni hatari.Ogopa pale watu wawili wenye nguvu tofauti wanapopigana.Unaweza kukuta huyo mwanamke alikuwa hana uwezo wa kupigana na huyo mume na hivyo kuvuta silaha iliyoko karibu -kisu.Ingeweza kuwa silaha yoyote ile.Hivyo jamani watu wajihadhari na ugomvi unaoishia kwenye kupigana.Ikiwezekana ni bora kumaliza tofauti zetu kwa majadiliano zaidi kuliko kuingia kwenye vipigo.

Usisahau kuwa kila leo kuna wanawake wanapoteza maisha kwa sababu ya vipigo vya waume zao na hakuna anayesema kitu.Fikiria ni wanaume wangapi hawana uhalali wa kuwa waume!!
 
Mwanamke naye ni binadamu ananguvu,akili hivyo siyo kila mwanamke hupigwa na mumewe.
 
SMU,
Ugomvi wa namna hii ni hatari.Ogopa pale watu wawili wenye nguvu tofauti wanapopigana.Unaweza kukuta huyo mwanamke alikuwa hana uwezo wa kupigana na huyo mume na hivyo kuvuta silaha iliyoko karibu -kisu.Ingeweza kuwa silaha yoyote ile.Hivyo jamani watu wajihadhari na ugomvi unaoishia kwenye kupigana.Ikiwezekana ni bora kumaliza tofauti zetu kwa majadiliano zaidi kuliko kuingia kwenye vipigo.

Usisahau kuwa kila leo kuna wanawake wanapoteza maisha kwa sababu ya vipigo vya waume zao na hakuna anayesema kitu.Fikiria ni wanaume wangapi hawana uhalali wa kuwa waume!!

Ni wengi zaidi. Ukitizama sana hii imekuwa habari kwa sababu tu ni mwanamke (ni kama vile binaadamu kumng'ata mbwa inavyoweza kuwa habari na si kinyume chake!). Yote hii, nadhani ni athari za mfume dume.

Kwa vyovyote vile inapofikia, mmoja kati ya wanandoa anataka kutoa uhai wa mwingine, bila kujali jinsia, kimsingi anapoteza uhalali wa kuwa katika hiyo ndoa. Ndoa ni watu wawili, sasa kama mmoja ahataki mwingine aendelee kuishi hiyo ndoa inapoteza maana kabisa.
 
inawezekana kabisa matumizi ya kisu ilikuwa ndio last "resort" kwa
mwanamama ili aweze kuokoa maisha yake. wataalamu wa mapambano wanasema ukimzingira adui bila kumwachia mpenyo achomoke basi ujue mpambano unabadilika kwani adui atapigana kwa kutumia njia zote kwani anajua fika vinginevyo hatapona.

hata hivyo mambo ya husband na wife kupigana hayana tija aslani.
 
Ila mleta habari hujafafanua chanzo cha kichapo hicho kitkatifu. Unajua akipigwa mwanamke tunasema mila zinaruhusu, akipingwa mwanaume tunasema mila zimevunjwa!!!! Mapinduzi ya Feminism huko China, ni matokeo ya mkutano mkuu wa akina mama huko Beijing!!!! Na sasa kwa utandawazi wanaume tunalo!!!!
 
Mkuu,
Hebu tumwagie facts on this maana kwangu hii ni habari mpya.

Pamoja ma mambo mengine, msisitizo ulikuwa katika ile phrase kuwa "Binadamu wote ni sawa". Hapo haikubeba mantiki ya mahitaji muhimu japo hata kama navaa magome, na kulala ndani ya nyumba ya nyasi na kula mizizi basi utaambiwa umepata basic needs. Inapokuwa swala la rights and sharing ndo akina mama wanataka usawa!! Kwa mantiki hiyo kama unampiga mwenzako basi na wewe akuangushie kichapo basi!!!! Huo ndo usawa ati!!! Akina mama wakitaka kufungua mashtaka dhidhi ya waume zao, na kama kila shitaka ni mahabusi, basi itabidi zijengwe nyingine!!! Tupendane ndiyo silaha pekee ya ushindi katika familia na ndoa.

Ya Beijing sina details nayo sana, maana wengi waliyatafsiri vibaya na matokeo yake ni hatari. Ati least najua kuna mkutano huo wa Bijing na ulikuwa na maazimio ambayo yalitumwa kila nchi duniani kwa tekelezaji!!! Jamani mlioko huko Wizara ya Jinsia, Maendeleao na Watoto tujuzeni zaidi.
 
kWA KIFUPI NI KUWA Mkutano wa Beijing ni moja ya mikutano ya UN. Huu ulikwa wa nne wa UN wa wanawake na kwa vile ulifanyika Beijing ndio ukabatizwa Mkutano wa Beijing.Kumbuka kulikwa na iliyotangulia huko nyuma iliyofanyika Mexico na Nairobi.Kilichofanyika Beijing ni tathmini ya miaka 10 kuanzia Nairobi 1985.Kufuatia tathmini hiyo basi maazimio yaliwekwa katika maeneo 12 ili kukaza buti zaidi katika kuboresha hali za wanawake duniani katika nyanja zote- na Maazimio hayo yakaitwa Beijing Platform of Action.Details ninaweza kukupa ukitaka.

Nilitaka kujua zaidi uliposema "Mapinduzi ya Feminism huko China, ni matokeo ya mkutano mkuu wa akina mama huko Beijing "ndiyo nikataka kujua kama kuna kipya ambacho kimenipita sikua nakijua ndugu yangu nikata unijuze zaidi.

Asante lakini.
 
Kanisani padre aliamrisha wanaume wote wanaoteswa na wake zao wasimame; walisimama wote isipokuwa mmoja tu alibakia amekaa!
Padre: Haleluya! MUNGU umemshirikishaje? Wewe huteswi na mkeo?
Akajibu:Kanivunja miguu yote hata kusimama siwezi!
 
Back
Top Bottom