Zinduna
JF-Expert Member
- Nov 6, 2011
- 2,378
- 3,392
Hebu wanaume leo mnipe ushuhuda, kama hamjawahi kukutana na hiki kizungumkuti cha wanawake.
1. Unakutana na binti anakuchangamkia na kila mnapokutana anakusalimia kwa bashasha huku akikupa tabasamu maridhawa linalokushawishi kumtongoza kutokana na kuvutiwa naye, lakini unapothubutu kumwambia ya moyoni anakutolea nje kifedhuli kiasi cha kukuumiza moyo wako
2. Inatokea kila asubuhi uendapo kazini na urudipo kazini unakutana na binti huyu mnayeishi naye mtaa mmoja na kila mkutanapo anakutupia macho ya mahaba huku akikusalimu kwa heshima na upendo, mara mojamoja mnapata fursa ya kuongea mawili matatu kuhusu maisha na pilika za mjini na anaonekana kuvutiwa na wewe kwa jinsi unavyozungumza naye kwa upendo,anaonekana dhahiri kukupenda na haachi kujipitisha pitisha pale inapotokea uko kibarazani kwako ukipunga upepo, moyo unakulipuka kwa mapenzi unaona huyu ndiye, lakini unapojaribu kumtupia nyavu anachomoa na kukupotezea mazima humuoni tena na anaanza kukukwepa. Unajikuta ukijiuliza huyu mwanamke ni mzima kweli au ana wazimu?
3. Mnakutana kwenye Party au Klabu, wakati wakucheza mziki anakufuata na kukuomba mcheze,unapocheza naye anakuchezea kwa manjonjo ya kimahaba huku akikushika shika nakukugeuzia makalio yake na ma hipps yaliyojazia jazia na wewe ukipata fursa yakuyashika na kuufurahia utukufu wa Muumba kiasi cha kusababisha maumbile yako ya chini kututumka kwa ashki na tamaa ya kimwili huku akili yako ikikwambia,leo lazima nikaufaidi huu utukufu wa Mungu. Mara muda wa kufunga mziki umefika na kwa kuwa ni usiku wa manane kila mmoja sasa anatoka kutafuta usafiri wa kurudi kwake. Ukiwa umefuatana naye kutoka nje ya Klabu huku ukijiamini utamudu kumshawishi uondoke naye kwenye Ki Vitz chako cha mkopo, mara anakuonyesha jamaa aliyepaki Toyota MarkX akimsubirina anakujulisha,
Yule ni mpenzi wangu amenifuata, ahsante kwa kampani, uwe na usiku mwema !
Anakuaga hivyo na kukuacha ukiwa umeduwaa. Unabaki ukisaga meno na kungata midomo kwa hasira
4. Mnafanya kazi katika jengo moja, na mara kwa mara mnakutana kwenye mghahawa kwa chakula cha mchana na wakati mwingine kwa evening coffee, wewe unakuwa ni mtu wa utani mwingi na masighara, na kila unapofanya utani anacheka na anaonekana kuufurahia utani wako na pia anaonekana kuvutiwa na uwepo wako kila mnapokutana, kwa kifupi ni kwamba anaonekana dhahiri kukupenda. Jambo hilo linakufanya utake kumvuta ili awe mpenzi wako, si kajilengesha ! Unapojaribu kumuomba mtoko ili upate wasaa wa kumtongoza anakutolea nje na kukwambia hayuko interested na wewe unabaki unashikwa na mshangao, ni kitu gani hiki kinakutokea
Hebu wanaume nipeni mauzoefu yenu kama mlishawahi kukutana na moja kati ya hivi visirani nilivyovieleza hapo juu
CC:
Kaizer, Asprin Kiranga The Boss, Nyani Ngabu, Mwita Maranya, Preta, snowhite, gfsonwin, King'ast, Ruttashobolwa, lara 1, Mr Rocky
Mkuje mtoe maushuhuda yenyu
Acha hizo zote sasa kuna hii yangu.
Nimekutana na mtoto mahali fulani, mtoto kanichangamkia na mimi bila kupoteza nafasi nikamchangamkia zaidi, tukaongea mengi kwa sababu mimi nilikuwa nimefikia hotel moja kali sana, ilivyofika usiku nikamwambia mimi naenda kulala ila ningependa tuende wote, bila hiyana akakubali. Na ukimcheka mtoto yuko vizuri, choo kipo vizuri, mguu ni tembo style na sio Flamingo style. Basi tulipofika room mimi nikaenda kuoga then naye akaenda kuoga tukapanda kitandani huku tukitaniana maneno ya kimahaba, sasa si mimi nikamvua boxer then ikachukua buti nikavaa, ile nataka kumchojoa kufuli ili niue, si akasema yeye hawezi kuduu na mimi eti it was just a company. Yaani mpaka asubuhi nikatoka patupu, dah siwezi kusahau ile pua niliyoangukia.
Sijawahi kuona mwanamke mwenye roho ya ukatili kama yule mweeee!
Teh Teh Zinduna umenifanya nicheke sana na hii thread yako na umenikumbusha mbali sana..na umenikumbusha hasira nilizo zipata baada yakukumbana na hiyo hasa namba nne!
Muda mwingine sisi wanaume huwa tuna kosea sana tena sana maana huwa tunaamini mwanamke hawezi kukukubali au kukupenda bila kuwepo na hisi za mapenzi ndani yake kumbe sivyo!Na yanayo tudanganya zaidi ni matendo na hisia wanazo onesha muda mwingine zinazo tupelekea tuzichanganye na hisia za mapenzi!
Na kumbuka ilikuwa 2008 kuna binti alitokea kunizoea sana na ilikuwa haiwezi kupita siku bila kunitafuta au kuonana tukapiga story na muda mwingine alikuwa hadi aniletea zawadi na ikifika muda wa chakula cha mchana ananishitua tukale..na uwezi amini mimi mwanzo nilimchukulia kama rafiki wa kawaida kabisa..lakini baadhi ya watu walifikiri nina uhusiano nae.
Huyu binti ilikuwa hawezi kulala kabla hatujaongea au kuchati na kutakiana usiku mwema na alikuwa anaonekana mwenye furaha sana hadi marafiki zake wakawa wanasema huyu lazima umuoe kabisa hapo hata sitamtongoza hata sikuwa na fikiri kufanya hivyo maana nilimuona kama rafiki tuu!
Baadae nilianza kupata hisia za kutaka kumtongoza na nilipata msukumo zaidi kutoka kwa marafiki zangu wakiniambia hatuamini kama huna uhusiano na fulani...na anavyo onekana anakupenda ...acha uongo wewe..haiwezekani..daaa
Baadae nilifikiria nikasema lazima nifunguke sasa na haitakuwa shida maana ni wazi ana nipenda kabisa kwanza ataanzie wapi kukataa? niliangalia mazingira yote nikaona hayampi nafasi kukataa kabisa na haiwezekani!
Sasa kwakuwa ulikuwa ndio mwezi wa Valentine nilisema nitaitumia siku hiyo kumsprise na kumfungukia...nilikwenda dukani nikanunua card,mau na zawadi ya pochi..nikavianda vizuri hii ilikuwa siku tano kabla ya Valentine(nilifanya maandalizi mapema sikujua yatakayo nikuta)
Ilipo baki siku moja kabla ya tukio nikamtumia sms kuwa leo jioni nataka tuka kae sehemu tupige story..akasema "poa tena nitakuwa wa kwanza kufika utanikuta" daa nilifurahi sana na nikajisemea moyoni daa tayari nimepewa ushindi wa mezani.
Ulipo fika muda nilia andaa zawadi zangu nilijongea eneo la tukio na kuanza kunywa soda.. baada ya dakika ishirini alifika na kukaa ..cha kwanza akaniambia "Siamini hujaniletea zawadi nika mwambia usiwe na wasi wasi... nikashika kifurushi nika mkabidhi akachunguliaa akacheka akasema nimezipenda lakini nitaziangalia baadae asante...daaa..nikasema nisichelewe nikaanza kufunguka..duuu nikamweleza kila kitu...
Niliishiwa nguvu alipo niambia ruttashobolwa samahani kakaangu mimi "nilikuwa na kuheshimu na nitakuheshimu na upendo nilio nao kwako ni wadada na kaka tuu na sikutegemea kama tutafika huku na siwezi kabisa maana kweli wewe ni muhimu kwangu lakini si jinsi ulivyo fikiri...na zawadi zako siwezi kuzichukua maana haitakuwa fair..samahani naomba niende" nilijaribu kubembeleza wapi ndio kwanza alibadilika na kuchukia na sikuwai kuona amechukia kiasi kile..aliondoka na kuniachia zawadi zangu duuu..niliishiwa nguvu kabisa na kumbuka pale bar nilikuja kuondoka saa 5 na huwezi amini urafiki ulikufa na akabadili namba kabisa....sikuamini kilicho nitokea na ilikuwa funzo kwangu....
Hakuna kazi iliyo ngumu kama kujua mwanamke anataka nini...kwakweli nilipatwa hasira sana na aibu juu
@zinduna umenifanya nikumbuke mbali sana hii thread yako na umenikumbusha mbali sana na inatukumbusha machungu ambayo unayapata baada ya kuweka too much expectation kwa binti na siku ya siku unakumbana na kituko cha mwaka au aibu ya mwaka au hata kumwagiwa kinywaji au kutukanwa mbele ya kadamnasi kisa ulitegemea jibu positive linatoka negative .
Huwa sometime tunajipa matumaini kuwa hapa nilipo na nilipofika ni kama kumuangusha tembo kwa fimbo yaani sitakataliwa. Kumbe unakuta mwenzako yuko mbali kabisa na wala hana hilo wazo na wewe na tatizo ni ile wanaume tunaamini mwanamke hawezi kukukataa wala kukuaibisha mahali popote au kwa hii hatua niliyofikia mimi na yeye. Na kwamba hapa alipofikia ana asilimia mia ya hisia za kunipenda wala hatanikataa. Na yanayo tudanganya zaidi ni matendo na hisia wanazo onesha muda mwingine zinazo tupelekea tuzichanganye na hisia za mapenzi na unakuta hizi hisia wala sio za mapenzi ni za kukupenda tuu kiurafiki zaidi.
Nakumbuka ilikuwa 2006 kuna binti alitokea kunizoea sana kwenye mazingira ya kazi. Yaani kazini ilikuwa kama kumbikumbi kila swala analopata au analoambiwa lazima anishirikishe na kazi zangu zile ambazo zilikuwa zinahusu labda fani yake alikuwa hasiti kuzifanya kwa moyo hata kwa kuchelewa kuondoka kwenye mazingira ya ofisi. Muda ambao alikuwa free hana majukumu makubwa ofisini kwake ni lazima aje kwangu tunapiga story na muda mwingine anaona kwenda canteen mchana haina maana anaenda analeta msosi tunakula pamoja ofisini. Kwangu mimi niliona kwa kuwa alikuja mgeni ofisini na mtu wa kwanza kumzoea alikuwa mimi niliona ni just a friend na kutafuta kampani ya mtu wa karibu na kumfanya asijione mpweke kwenye mazingira ya ofisi mpya.
Tukitoka ofisi japo tulikuwa na usafiri wa pamoja ni lazima ahakikishe nimefika home kwanza na yeye anakuwa wa mwisho kwenda kushushwa na dereva na akifika lazima anitext kwamba amefika home kwake salama. Usiku baada ya msosi na akishajua na mimi nishamaliza kula ni lazima tunaanza mazungumzo kwa sms au simu na yanachukua muda mrefu sana kuongelea masuala mbalimbali mpaka ya ndani kabisa ya kimapenzi kuulizana mahusiano yetu na wapi tulijikwaa katika mahusiano na wapi tunapaswa kurekebisha katika mahusiano iwapo tutakuwa kwenye mahusiano mapya.
Mahusiano na urafiki huu uliendelea kwa kufikia kutoana out weekend na kupeana zawadi mbalimbali kwenye siku za kuzaliwa au Valentine na yeye alikuw aanaongoza sana kunipa zawadi siku yoyote akijisikia anakuletea zawadi. Kwa ofisi kila mtu alielewa kuwa hapa hawa ni zaidi ya marafiki ila siri ilikuwa ndani ya mioyo yetu. Wakati huo sikuwa kwenye mahusiano baada ya kuachana na mtu wangu wa karibu. Na ofisini walikuwa wamnaelewa kuwa kipindi hicho niko single sina mtu so walipoona ule ukaribu wakajua hapa ni penyewe hawa wameshakubaliana. Japo haikuwepo hisia mwanzoni kuwa anaweza kuchukua nafasi yoyote maishani mwangu nilianza kumpenda kutokana na kujali kwake na namna alivyonichukulia. Alikuwa hafanyi maamuzi yoyote bila kunishirikisha au kwenda mahali popote bila mimi kuwa na taarifa yuko wapi na anafanya nini kwa wakati huo. Mwanaume hisia zikawepo kuwa anaweza kuwa rafiki mzuri na niende zaidi ya hapo kuwa mpenzi wake na mwandani wa maisha yake ya baadae.
Nakumbuka ilikuwa birthday yangu na ni yeye alinifanyia surprise. Alitayarisha kila kitu sehem ambako tulikuwa tunapenda sana kwenda. Aliwaambia baadhi ya marafiki zake na baadhi ya marafiki zangu ambao nilishawatambulisha kwake. Tulipotoka ofisini jioni akaniomba niende home nibadilishe siku hiyo ananitoa out. Nilikubaliana nae na nikaenda nyumbani kujiandaa na wakati nampigia kumuuliza yuko wapi nimpitie yeye alinijulisha sehemu ya kukutana so nisihangaike nimkute sehem ile yeye ameshatangulia.
Kwa kweli alipendeza katika siku ambazo nilikuwa natoka nae out siku hiyo alivunja sanduku. Alikuwakatika ubora wake na bora zaidi ya siku zote. Kukutana tena na ile surprise ya birthday aliyoniandalia nilijikuta moyoni nawaza today will be my date nivunje ukimya au nitajikuta nachelewa kuomba jamvi.
Wakati sherehe inaendelea nilivunja ukimya na kumweleza hisia zangu juu yake............................. to my surprise ilikuwa pigo kubwa sana na sherehe yote iliharibika. Kwanza alipata mshtuko na kuongea maneno ambayo yaliniumiza sana. Alinichukulia kama rafiki yake wa karibu na mshauri wake na kamwe hakutarajia hata siku moja nivuke huo mstari. Machozi yalimtoka na ikawa ni kazi kumbembeleza ili nisije nikaharibu sherehe. Japo alitaka kuondoka nilifanikiwa kumtuliz ana akabaki ila sio katika uchangamfu tena kama wa awali.
Iliishia pale pale kurudi ofisini mazoea yakapungua na ule ukaribu ukatoweka na tukabaki kama friends. Hadi niandikapo ameolewa na ana mtoto mmoja kwa sasa ila still we are friends japo sio tena maana ni mali ya mtu nisije kumtibulia kwa mume wake.