Mwanaume ananipasua kichwa

Kuwakomesha hao familia muoe wewe huyo kulakulala wao ili watie akili kuwa hawana mtu.
Asikutishe na kuachana, mwambie kuachana sawa tu kisha fanya maisha yako na achana nae kbs maana hata akikuoa baadae familia yake itakunyima raha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekushangaaa sana!!!kwani ukiolewa ukarudi kaka na hio familia ndio watakupenda?Kwanini wewe upange chumba yeye anafanya nini?
Pole dada mapenzi ni upofu na ushapofuka...
Komaaa muwe na kwenu habari za kuishi kwa "wakwe"kataa kabisa.
Pili komalia ndoa sio kukuchuja miaka yote.
Kama hawezi kaza roho mwache aende(lakin wewe uwezi).
Sikiliza na moyo wako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari JF..mm ni binti nina boyfriend wa muda km miaka 7 now.

Bahati mbaya sn nilikoseaga nikaenda kuishi nae tena nyumbani kwao kabisa mamamkwe na wawifi wote wapo. Hajanitolea barua wala mahari. Wakati naishi nae familia yake ikawa hainipendi navumilia walikua wananiona km nimemroga mtoto wao kwa jinsi yuko karibu na mm. Tukaja kugombana na huyo mwanaume ugomvi mkubwa tu nikaondoka nikarudi kwetu huku nyuma familia yake ikafurahi kweli bora tumeachana.

Tumekaa miezi 6 mwanaume akanitafuta tukarudiana sasa changamoto ni kua anataka siku ambazo niko off kazini niwe naenda kushinda kwao. Jman nimekataa mwanaume haelewi nimemwambia siwezi kwenda kwao tena apange chumba tuwe free. Na kwao nitaenda atakapokua amenioa au kunitolea mahari..haelewi anasema km siendi kwao basi tuachane...

Je ni sahihi kweli baada ya yote hayo kutokea mm kutoelewana na familia yake niwe naenda kwao jamani? Nilikua nafikiria km yeye hataki kupanga chumba basi mm nipange kwa pesa yangu ili tuwe free je na hilo ni sawa.

Naombeni ushauri jamani mwenzenu nimekwama
mkikuwa mtaacha
 
Huna akili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kosa ulilofanya ni kwenda kuishi kwao my dia ila haina haja ya kupanga chumba kama kweli anakupenda atafata taratibu na utakua mke halali
 
Nahisi hata ukikaa na mashoga zako mkipiga story au mkiombana ushairi wewe na huyo pimbi wako wote mnaonekana hamnazo
 
Yaani uchumba miaka 7, jamaa anakaa kwao haitoshi na wewe ukahamia aisee mna shida mahala nyie.
Alafu kwa maelezo yako mpaka hapo sioni future yoyote kati yenu yaani jamaa anakuambia urudi ukaendelee kuishi nae kwao huko huko kama hutaki muachane yaan kiufupi huyo mwanaume sijui ni mvulana hakufai.
 
Mmmh haupo seriouz mamy ,,maisha ya sasa
Mwanamke lazima uwe na msimamo,,acha kuyumbishwa angalia maisha yako kwanza
Alafu uchukue maamuzi ,,,maana mapenzi kwa upande mwingine ni upofu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabisa yaani hawana future ,,hawapo seriouz hao,,eti miaka 7 na uchumba ume expire
Mi mwenyewe nimetaka kumtukana mtoa mada nikakumbuka si kosa lake
Yaani uchumba miaka 7, jamaa anakaa kwao haitoshi na wewe ukahamia aisee mna shida mahala nyie.
Alafu kwa maelezo yako mpaka hapo sioni future yoyote kati yenu yaani jamaa anakuambia urudi ukaendelee kuishi nae kwao huko huko kama hutaki muachane yaan kiufupi huyo mwanaume sijui ni mvulana hakufai.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom