Samson Ernest
JF-Expert Member
- Aug 28, 2014
- 1,242
- 1,750
“[28] Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe. ”
Efe 5:28 SUV
Kuna watu hawajipendi, hii inaweza kutokea kwa sababu nyingi zinazoweza kumfanya mtu ajichukie na asijipende.
Mtu asiyejipenda mara nyingi huanza kutamani kufa, huona kila kitu hakifai kwake, na anaweza kufanya vitu vibaya na watu wakabaki wanashangaa.
Kutojipenda kwa mtu haiwezi kutokea tu, mtu anaweza asijipende mdomoni, ila ukamwona anakula vizuri, analala vizuri, anaamka na kwenda kufanya shughuli zake vizuri.
Mtu aliye sawa kiakili au akiwa hajaharibiwa ufahamu wake, atakuwa anajipenda, atafanya mambo yanayomfanya awe salama.
Sasa neno linasema mwanaume anapaswa kumpenda mke wake kama anavyojipenda yeye, au anavyoupenda mwili wake.
Aliye tayari kuumiza mwili wake, au kuutesa mwili wake, au kuujeruhi mwili wake, au kuukatakata na visu, atakuwa mtu mwenye matatizo ya akili ya kiwango cha juu sana.
Ukiona mwanaume anamtesa mke wake, au hampendi mke wake, ujue kuna shida ya kiroho na kimwili. Huwezi kuchukia mwili wake ukiwa na akili titamamu.
Penda mke wako, humpendi kwa sababu kuna sheria fulani ngumu kwako, unafanya kama hitaji lako lililo kwenye moyo wako bila kulazimishwa na mtu yeyote.
Kufanya hivyo ndoa yako itasitawi na kukua sana, utamfurahia mke wako siku zote za maisha yako.
Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana