Mwanaume afanye hivi ili mkewe amuone mtenda miujiza kila siku, hatasikia la mtu!

Hahahaha kweli kabisa aisee huwa naitumia Mara kwa Mara si kwamba nakuwa sina kitu la hasha huwa najaribu kujenga matumainj kwa NYONDA wangu kila siku halafu ghafla bin vuuu anapata kile alinichoniomba .

Mwanamke ni kiumbe Wa kuishi nae kwa akili


Huu Uzi umenijenga ngoja niuweke sticky
ha ha ha hoja kuntu, chakula cha ubongo.
 
"Wanawake wote wamejaliwa kipaji cha kutumia hela mpaka ziishe" na zikiishaisha anajitoa na lawama zote kukupa wewe mwanaume...... Hilo ni Neno kuntu
Wakudadavuwa huwa ajishushia personalty kuandika uchafu wake wa sisa kumbe kuna mahala huwa panamfaa, hii statement yake ulyoi quote hapo juu ni very useful to men. Big up sana kwa thread hii
 
Na vipi siku mkeo akigundua kuwa unafichaga hela zote hizo pasipo kumjulisha?

Uaminifu wake kwako utakuwaje?
Je, akihisi hiyo pesa huwa unapelekaga kwa mwanamke mwingine?

USHAURI WANGU.
Ficha pesa ya ziada tu unayopataga nje ya mfumo wa kawaida wa kipato(Kama Posho, deals) lakini kamwe usimfiche kipato chako halisi ambacho kiko kwenye mfumo rasmi(Kama Mshahara). Wanawake ni waerevu sana, akitaka kujua siri zako atazijua tu, kumficha mshahara wako ni kujipalia mkaa wewe mwenyewe. Na kwa jinsi mishahara ya watu wengi ilivyo midogo au kutokutoshea, halafu uchote humo humo na kuficha tena, utaleta tafrani tu. Maana inahitaji Nidhamu ya juu sana kutokuweza kugusa hicho kiasi cha mshahara unachokificha na wakati huo huo mshahara haitoshi.
 
Hili ni fundisho kwa vijana wengi ambao wanataabika, suala la fedha limekuwa mwiba mkubwa na chanzo kikubwa cha mahusiano na ndoa kuyumba. Nimelazimika nije na ushauri huu ambao utawasaidia vijana wa kileo ambao wanataabika na ndoa hususani suala la fedha.

Kinachowaumiza vijana wengi katika fedha na wenza wao ni tabia ya wanaume kuwa wazi kwa kutoa taarifa za pato lake kamili. Jambo la uwazi ni jema lakini muwe na kiasi kwani usipokuwa na akiba ya 'taarifa za kipato chako' utakosa fusra ya kufanya miujiza pale mambo yanapokwama.

Fanya hivi. Mfano kipato chako ni shilingi milioni moja kwa mwezi, mweleze kwamba unapokea shilingi laki 7 na hizo tatu hakikisha unaweka katika sehemu salama ambayo hata ikitokea umekufa familia yako itafaidika, mfano benki kila unapochukua mshahara hakikisha unaacha laki tatu kama akiba asiyoijua. Sasa katika hii laki saba panga matumizi pamoja na akiba ya pamoja.

Wanawake wanapenda 'mshtuko/suprise'..so siku ya siku ukiona kanuna unamtoa shoping lazima ataona umetenda muujiza kwa nia njema. Hapa ndipo pale utasikia mwanamke anasema 'mme wangu ana akili kweli'. Ikitokea una marupurupu fulani kama safari nk hakikisha unatoa kiasi na ziada unaweka chimbo. Hii itakupa upenyo wa kuwasaidia hata wazazi wako na ndugu zako bila kumhusisha mara kwa mara kwani wanawake wengine hawapendi usaidie ndugu na jamaa. Fanya mbinu hii hata kama kipato chako ni laki tano weka hata elfu hamsini chimbo ili uweze kutenda baadhi ya miujiza.

Wanawake wote duniani wamejaliwa karama ya kutumia hela yote ya mmewe, yaani ukimwambia kuna hela hii yeye ataandika orodha ya mahitaji ya familia ni kwani njema ila pesa zikiisha yeye hujitoa na kukulaumu kwanini ulitumia pesa zote. Yaani dharura ikitokea yeye hayupo ni lako hilo na ukishindwa kutatua hapo ndipo dharau inaanza...utasikia 'mme wangu hana msaada kabisa' yaani hajali kabisa matatizo anatumia pesa zote bila uangalifu.

Haya yote yanahitaji ustadi mkubwa na utimamu, kumbuka siku zote mwanaume anatakiwa kuwa mtu wa mshitukizo/surprise kwa kutumia kipato kile kile alichonacho. Yaani tunasema uwe na uwezo wa kutengeneza hela (money creator). Ikitokea dharura unamuangalia usoni huku ukitabasamu, unamwambia 'mke wangu usihuzunike ngoja nifanye mpango nitatue hii shida'.

Hii ndio mbinu tuliitumia sisi na kuweza kuishi na mama/bibi zenu bila bugdha.

Nawakilisha.
ad
 
Mwanamke asiyetaka niwasaidie wazazi wangu apite kushoto na aende kua money creator yeye mwenyewe kama ni rahisi.
 
umeuelimishaaaaaaaaaaa umma
umeongezaaaa kuheshimikaa ndanii ya familiaaa nyingiiii
na mimi nmejifunza kituu
Japo nilikua namuonaga mzee wangu akifanya hivo na hata leo bado anaendeleaaa kutendaaa miujizaaa kwa mazaaaa


SHUKRANI KWA KUNIHAMASISHAAAAAA
 
Wakudadavuwa leo umeongea jambo la msingi kuliko msingi wenyewe. Asante kwa somo.
 
Mshahara ni siri huko kumwambia ni kosa wanawake tunawapenda tu lakini wanatuumiza sasa wewe tumelala wote usiku kucha asubui unaniomba hela inamaana Mimi nilikuwa nafanya kazi ?
 
Back
Top Bottom