Mwanasiasa katika kampeni

MAMMAMIA

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
3,811
0
Siku moja baada ya kumaliza bla-bla zake kijijini, wapiga kura walimweleza matatizo yao kama vile shule, maji, hospitali n.k.

MWANASIASA MKONGWE: Ikiwa mtanichagua, nitafanya kila niwezalo kwa ushirikiano wenu.
Siku nyengine baada ya porojo zake gerezani, wafungwa walimweleza matatizo yao kama vile kila mfungwa awe na chumba chake chenye bafu, kiyoyozi, runinga plain ya 52" na dishi la satelite, mtumishi, wasiamshwe alfajiri, wapatiwe mabinti warembo kila wiki n.k.

MWANASIASA MKONGWE: Bila ya shaka, hili nitalitekeleza hata kabla ya uchaguzi.
Mwanasiasa kijana aliyeambatana naye akashangaa na kumwuliza kwa nini wale walio na mahitaji ya muhimu amewaahidi kama wakimchagua na hawa wanaoomba maraha amewaahidi kuwatekelezea maombi yao mara moja.

MWANASIASA MKONGWE: Kijana usiwe mjinga, mimi sitarajii kurudi shule kusoma, kuishi katika giza wala kutibiwa katika zahanati, lakini hapa gerezani ninajitayarishia maisha yangu ya baadaye. :israel:
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom