Mwanasiasa gani amekushangaza 2015-2017

Mimi yaliyonishangaza ni haya:
1. CCM kwa kuwaimbia wapiga kura wake eti wataisoma namba
2. Mkuu wa Wilaya ya Hai kwa kung'oa miche ya mboga shambani kwa Mbowe
3. Polepole na Kabudi kwa Kuikana Katiba ya Warioba waliyoshiriki kuiandaa ili tu wapate nafasi ndani ya Chama Cha Makinikia
4. Usalama wa Taifa kumnyooshea Nape bastola hadharani bila kufanywa lolote
5. Mkuu wa kaya kuwa ndiye mgawaji wa pesa kwa kila idara
6. Nafasi ya Jaji Mkuu kukaimishwa mtu bila kuthibitishwa hadi leo
7. Fedha za Escrow tukaambiwa si za Umma na leo ' wezi' wanakamatwa kwamba waliiba fedha za umma
8. Mwekyembe kupewa wizara ya habari na kulifungia gazeti la Mawio bila kufuata taratibu
9. ACT-Wazalendo kutuzuga kwamba ni chama cha Upinzani wakati ni Makada wa CCM
10. Bashite kuendelea kuwa Mkuu wa Mkoa wa DSM
11. Ndugai kuwaagiza mawaziri wasipeleke (kodi yetu) fedha za bajeti iliyopitishwa kwenye majimbo ya upinzani
12. Mbunge Lusinde kwa kusema Katiba ya nchi haina uhusiano na raslimali za Taifa kama madini
13. Wassira kung'ang'ania kwenda bungeni na kumsumbua Bulaya kila wakati Mahakamani
14. Kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar
15. Mzee wa kaya kuwateua makada wa chama kushika nyadhifa za utumishi wa umma kama Ukurugenzi, Ukatibu tawala, n.k
16. Mzee kutokwenda msiba wa watoto waliopata ajali ya Lucky Vincent kule Arusha
17. Gambo kula fedha za rambirambi na kuzuia watu wasiende kuwapa pole wazazi na walezi waliofiwa watoto ajalini.
18. Mzee kusema mhimili wake ni bora kuliko mihimili mingine
19. Sheria ya makosa ya mtandao kumhusu mzee wa kaya peke yake
20. Fedha za wahanga wa tetemeko kukarabati miundombinu ya serikali
21. Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Tulia Aksoni kuwa Naibu Spika wa bunge kwa tiketi ya CCM
22. Mzee kuwazira na kuwanyima elimu watoto wake wanaopata ujauzito wakiwa wanafunzi
23. Mzee kuwateua MaKamanda wa JWTZ kushika vyeti vya kisiasa, kama U-DC na U-RC
24. Mwigulu kuendelea kuwa Waziri licha ya mauaji ya Kibiti
25. Mzee kuzuia vyama vya siasa vya upinzani kufanya mikutano kasoro CCM
26. Wananchi kuendelea kuichagua CCM kuongoza nchi licha ya madhaifu na kushindwa kwa sera na ilani ya CCM.
27. Wabunge wa CCM kupitisha mikataba mibovu ya madini na baadaye kuruka kwamba hawakufanya hivyo ila LISSU na wapinzani wengine ndio wabaya.
28. Mzee kununua ndege kwa gharama kubwa na kutelekeza Kilimo na mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu.
29. Nchi kumsikiliza mtu mmoja tu
30. Ma-DC na Ma-RC kuwaweka ndani watu kama wapendavyo
31. Serikali kuingilia uchaguzi wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika, TLS.
32. NECTA kuwa uchochoro na kiwanda cha kutengeneza vyeti feki
33. ACACIA kufanya kazi kinyemela miaka 20 bila kujulikana na serikali yenye majeshi na usalama wa Taifa na uhamiaji.
34. Mwenyekiti wa chama Cha magogoni kuwakataza wabunge wake kwenda kuwajulia hali wenye shida ambao si CCM
35. Bunge kutekwa na serikali na kuzuia mijadala ya bunge kuonyesha mubashara.
36. Yanga kushindwa kumsajili Niyonzima licha ya kujua mkataba wake unaisha na badala yake ikampa fedha zote Ajibu.
37. Bunge kuchagua wabunge wa kutuwakilisha kwenye bunge la Afrika mashariki kwa kigezo cha Urembo.
38.Wapinzani kuzuiwa kukagua miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao ya wanayoongoza.
40. Ben Saa Nane kupotea na mamlaka zetu kukaaa kimya kama hakuna kitu vile.
41. Mke wa Mkuu wa kaya mstaafu kupewa ubunge wa kuteuliwa.
42. Mauaji ya kibiti
43. Wananchi kuandamana kumpongeza Mzee kwa kuliletea maendeleo nchi, wakati maendeleo yenyewe hatuyaoni. hii inaonyesha watanzania hawajui maana ya maendeleo na maana ya nchi kuitwa imeendelea.
44. Kuwadhalilisha mabinti zetu mchana kweupe kwa kuwaamrisha wanengue viuno mbele ya mkuu wa kaya anapofanya ziara huku wababa wakifurahi na kucheka mpaka gego la mwisho. Yaani tumewafanya binti zetu na viuno vyao ni chombo cha burudani.
45. Mkuu wa kaya kushindwa kutofautisha ziara za kichama na za kiserikali.
 
Habari wakuu kama Kichwa cha Habari kinavyojieleza hapo juu ni mwanasiasa gani aliyekushangaza zaidi kuanzia mwaka wa uchaguzi mkuu mpaka leo kwa ndani ya Nchi yetu lakini hata kwa Nje ya Nchi yetu pia itakuwa sawa
Hon. Hussein Mohamed Bashe
Member Type : Constituent Member
Constituent : Nzega Mjini
Political Party : CCM
Phone : +255762138204
P.O Box : P.O Box 106 Nzega
Email Address : h.bashe@bunge.go.tz
Date of Birth : 1975-08-26

Huyu kanishangaza kwa upande wangu, ila bado mapema, tusubiri mwisho..
 
Duh wewe mkuu umekuwa na mengi na ya msingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ