Mwanasheria:Wawekezaji wanaruhusiwa kufanya uchimbaji wa madini kadri wanavyoona inafaa

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,694
149,920
Kupitia kipindi cha Tuongee Asubuhui na mada ikiwa ni Uzalendo kwa Maslahi ya Taifa, mwanasheria wa kujitegemea,Gaspar Mwanalyela amerejea taarifa ya Policy Forum kuhusu mikataba/sheria zetu za madini na kunukuu clause mbili mojawapo ikitamka wazi kuwa, "wawekezaji wanaruhusiwa kufanya uchimbaji kadri wanavyoona inafaa."

Akasoma na kifungu kingine kinachosema kuwa hatuwezi kutaifisha mali za wawekezaji hawa.

Chanzo:Star tv

Hata pale mjengoni huwa tunaona kiti kinavyoweza kufanya maamuzi kadri ya aliekikalia anavyoona inafaa na madhara yake tunayajua na hata yule wa magogoni nae anaweza kuamua kari anavyoona inafaa na tumeyaona matokeo yake.

Naungana na mwanasheria huyu pale anaposema mikataba hii ni mikataba ya "kimangungu".
 
Kupitia kipindi cha Tuongee asubuhui na mada ikiwa ni uzalendo kwa maslahi ya Taifa,mwanasheria wa kujitegemea,Gaspar Mwanalyela amerejea taarifa ya Policy Forum kuhusu mikataba/Nasheria zetu za madini na kunukuu clause mbili mojawapo ikitamka wazi kuwa, "wawekezaji wanaruhusiwa kufanya uchimbaji kadri wanavyoona inafaa."

Akasoma na kifungu kingine kinachosema kuwa hatuwezi kutaifisha mali za wawekezaji hawa.

Chanzo:Star tv

Naungana na mwanasheria huyu pale anaposema mikataba hii ni mikataba ya "kimangungu".
It is a pity Kabudi hawezi kumweleza Rais kuwa Mh. sheria na taratibu ziko hivi, tufanye hivi na hivi! Lisu hatasikilizwa, kisa mpinzani!
Mh. Rais kweli hawa wote ukimwacha Lisu ambaye ni upinzani, hawakutaki au hawaitakii mema nchi yetu?
 
Ukitoka hapo nenda pia ukasome alichoandika Mbunge wa CUF, Mh. Maftah Nachuma.
Kisha ujipime.
 
It is a pity Kabudi hawezi kumweleza Rais kuwa Mh. sheria na taratibu ziko hivi, tufanye hivi na hivi! Lisu hatasikilizwa, kisa mpinzani!
Mh. Rais kweli hawa wote ukimwacha Lisu ambaye ni upinzani, hawakutaki au hawaitakii mema nchi yetu?
Unajuwa watu kuingiza siasa katika mambo kama haya tutaenda kubaya, Rais lazima aambiwe ukweli maana mkataba wa mpangaji tu na mwenye nyumba una terms and conditions sasa mikataba mikubwa kama hii, Mimi wasiwasi wangu tu isiwe kuwa CCM wanajuwa matokeo sasa ili wanataka wapate huruma kwa wengi bila kujua madhara ya kuiuchumi wawachague tu ni kama ya Mugabe hata kama alikuwa sawa lakini hali ilikuwa hairuhusu ila yeye alikuwa na target moja tu ku win election ndio kuja kuwapokonya mashamba sio wawekezaji ila wazimbabwe wachache matokeo akapata umaarufu sana lakini matokeo tuliona pesa yao tu wakawa wanaikimbia. kitu kimoja usimuamini mwana siasa anaweza kufanya lolote ili abaki kutawala hiyo ndio primary target. haya makampuni ya nje yako stock market lazima yaweke kila kitu wazi ukidanganya tu penalty yake sio mchezo ni kama yale ya kampuni ya Siemen kutoa hongo balaa lake fine 5 Billion$ ndio maana sitaki kuamini ACCACIA wafiche mapato maana ni pesa za watu hizo stock exchange. TZ wakacheck income ya jamaa halafu wacheck walilipa ngapi suala la 4% hilo ni ujinga wetu sio wao.
 
Hata mimi nimemzikiliza msomi Gasper na kwa kweli amesema kile kile ambacho wenye akili zetu tumesema miaka nenda miaka rudi na kabudi anakifahamu.
 
Kitu ambacho JMP anafanya ni kujiandalia DOWANS nyingine na figusu figusu za aina hiyo ... yote mikataba alishiriki kuipitisha halafu leo anaunda jopo... unafiki mtupu...na hivyo vipengere anavijua sana na bado anataka kupambana ngangari...si watuwekee basi hiyo mikataba wazi ili tuwaambie cha kufanya.. tunajdiri tu kwa kutokujua kilichomo kwenye mikataba hiyo ...
 
Mr. President ana nia nzuri na inaumiza sn Kwa mtu yoyote kuona rasilimali zetu zinatumiwa na wageni watakavyo huku tukiendelea kula hasara.

Tatizo ni kwamba Mr. President yeye hafuati taratibu zakimkataba. Hili litatukula sana maana hawa mabwana kwenye sheria hawana msalimie mtume.

Hapo ndio wengi tunapishana na maamuzi ya Mr. President. Kuliwa tumeliwa miaka nenda rudi, then tuwalipe tena gharama kubwa ya kukiuka mkataba hapo ni lazma tupaangalie vizuri
 
Kupitia kipindi cha Tuongee asubuhui na mada ikiwa ni Uzalendo kwa Maslahi ya Taifa, mwanasheria wa kujitegemea,Gaspar Mwanalyela amerejea taarifa ya Policy Forum kuhusu mikataba/sheria zetu za madini na kunukuu clause mbili mojawapo ikitamka wazi kuwa, "wawekezaji wanaruhusiwa kufanya uchimbaji kadri wanavyoona inafaa."

Akasoma na kifungu kingine kinachosema kuwa hatuwezi kutaifisha mali za wawekezaji hawa.

Chanzo:Star tv

Hata pale mjengoni huwa tunaona kiti kinavyoweza kufanya maamuzi kadri ya aliekikalia anavyoona inafaa na madhara yake tunayajua na hata yule wa magogoni nae anaweza kuamua kari anavyoona inafaa na tumeyaona matokeo yake.

Naungana na mwanasheria huyu pale anaposema mikataba hii ni mikataba ya "kimangungu".
Hicho kifungu walikwambia kipo kwenye chapter gani katika hiyo sheria. Sheria huwa haisomwi kwa kudonoa hivyo ikiwa inafanya kazi iliyokusudiwa. Hudonoliwa hivyo wakati wa kudanganya mafurafura kama wewe humu jf.
Nyote nyie na wanasheria wengine kwa hili hamna wa kusikilizwa kwa sasa. Kamati ya wanasheria na wachumi ipo kazini nayo itakuja na matokeo na kumshauri rais nini cha kufanya. Ikimshauri kuomba radhi sawa. Ikimshauri kujadiliana na wawwekezaji sawa. Ikishauri kuvunja mkataba sawa. Hivyo nyie wavimba macho tukae kimya mpaka wanaume wa shoka waje watupe cha kusema.
 
Tokeni huko leo ndio mnashituka!Nyi mnafaa kunyongwa kabisa.
 
It is a pity Kabudi hawezi kumweleza Rais kuwa Mh. sheria na taratibu ziko hivi, tufanye hivi na hivi! Lisu hatasikilizwa, kisa mpinzani!
Mh. Rais kweli hawa wote ukimwacha Lisu ambaye ni upinzani, hawakutaki au hawaitakii mema nchi yetu?
Tatizo sheria ilisomwa na third class students Tatizo ni kudanganya kiasi cha dhahabu ili kulipa royalty kidogo
 
Sa si useme tu tujue Maftaha kasema nini iki wote tujifunze kitu?
Courtesy group la telegram
===
Tumsome maftaa Mbunge kanena kisheria zaidi.

MBUNGE MAKINI WA MTWARA MJINI MAFTAH NACHUMA (Cuf) .

Imeandikwa na Maftah Nachuma (MB)
Mikataba yoote ya kimataifa huongozwa na wajibu wa aina mbili. Wajibu ulioandikwa(express obligation) na wajibu ambao haukuandikwa(im
plied obligation).
Wajibu ulioandikwa ni masharti yote ya mkataba yaliyo katika maandishi ambayo wahusika husoma na kuridhia, wakati wajibu usioandikwa ni masharti ya mkataba ambayo hayakuandikwa katika mkataba lakini yapo kwa asili au yapo kwakuwa tayari yalishasemwa na sheria na hivyo si lazima kuyaandika ktk mkataba.
Mathalan, mfanyakazi wako wa duka hawezi kukuibia halafu akasema kwenye mkataba wangu wa ajira hakuna sharti la uaminifu. Laa hasha uaminifu ni sharti la asili "implied obligation" kwa hiyo liandikwe au lisiandikwe bado lipo tu.
Kwenye mikataba ya kimataifa kama ile ya kwetu na makampuni ya madini masharti yafuatayo ni ya asili na hayahitaji kuwa yameandikwa ili kuyatekeleza :
1. Wajibu wa kuanika taarifa zote muhimu kuhusu shughuli inayotekelezwa katika mkataba( Implied covenant to disclose all necessary information over the subject matter).
2. Wajibu wa kutekeleza na kutenda kwa nia njema(Implied covenant to act in good faith and fair dealing).
3. Wajibu wa kila mhusika katika mkataba kuwa mkweli . Hili huwa ni katazo la udanganyifu(Fra
ud).
Haya yawe yameandikwa kwenye mkataba au hayakuandikwa yakikiukwa tafsiri yake ni kukiuka masharti ya mkataba.
Matendo kama kulaghai kuhusu uzito wa madini yanayochukuliwa, kulaghai kuwa unachukua dhahabu huku ukijua unachukua zaidi ya dhahabu, kulaghai kuhusu bei , kutotoa taarifa sahihi za kipi unapata na kipi hupati,nk ni kukiuka wajibu na masharti ya mkataba jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Na ikiwa wamekiuka mkataba kwa misingi hiyo basi Tanzania inaweza kufanya yafuatayo;
1. Kuendelea na mkataba lakini kwa sharti la kurudisha kile chote kilichopotea kwa mda wote( specific performance).
2. Kutoendelea na mkataba na kudai fidia, hasara tuliyopata,pamoja na riba zake kwa kipindi chote(
breach of contract).
Ndugu zangu, wajibu wa kutekeleza na kutenda kwa nia njema (implied covenant to act in good faith and fair dealing), kuwa mwaminifu na kutoa taarifa sahihi katika utekelezaji mikataba ni matakwa ya lazima duniani kote.
Sheria ya biashara ya Amerika Uniform Commercial Code vifungu vya 1 - 12 habari hii imeelezwa kwa upana.
Sheria ya biashara ya Ufaransa na Ujerumani The German Civil Code(BGB) na Civil Code of France zimeeleza vitu hivi.
Pia mahakama kuu ya Uingereza katika kesi ya Yam Seng PTE vs International Trade Co. Ltd (2013) EWHC 111 ( QB) iliamua kuwa masuala ya uaminifu na kutoa taarifa sahihi katika kutekeleza mikataba ni wajibu ambao upo hata Kama haukuandikwa kwenye mkataba.
Halikadhalika sheria yetu ya Mikataba, Sura ya 345 vifungu vya 18 na 13 vimeyafanya masuala ya udanganyifu na kutoa taarifa zisizo sahihi kama mambo ambayo ni makosa na yanayobatilisha mkataba.
Kamati ya Profesa Mruma imebaini upotevu wa Bilioni 829.4 x Miezi 12 kwa miaka 18 = Trilioni 829.4. Hizi ni pesa nyingi mno. Tunayo kesi nzuri ya madai na uhakika wa kurejesha fedha tulizopoteza. Ni vema mda huu pamoja na mambo mengine, nguvu nyingi ikatumika kuona ni namna gani tunapata hii fedha. Makosa yapo na yametendwa na hilo halina Shaka. Iko wapi haja kukhofu, hakika haipo.
Yumkini haitakuwa rahisi kutokana na aina ya mabepari ambao tunashughulika nao. Ni mabepari hatari wenye mtandao mkubwa wa kisiasa na nchi wafadhili pamoja na taasisi kubwa kama IMF, WB, UN nk.
Hata hivyo tumeshasema hii ni vita na vita sharti ipiganwe ili waliosiginwa wawe huru. Tunaweza kuumia kwa mda ila mwisho wa maumivu hayo itakuwa ni neema kubwa na ya milele.
Ni wakati sasa watanzania wote bila kujali Itikadi za vyama au Dini kuungana pamoja kupigania haki yetu.
Prof Ibrahimu Lipumba alionya jambo hili miaka kumi wakati wa utawala wa awamu ya tatu lakini serikali haikuchukua hatua za msingi.
Mungu ibariki Tanzania na mbariki rais kwa pamoja tushinde vita hii.
MAFTAH NACHUMA Mbunge Mtwara mjini.
 
It is a pity Kabudi hawezi kumweleza Rais kuwa Mh. sheria na taratibu ziko hivi, tufanye hivi na hivi! Lisu hatasikilizwa, kisa mpinzani!
Mh. Rais kweli hawa wote ukimwacha Lisu ambaye ni upinzani, hawakutaki au hawaitakii mema nchi yetu?
It is not his job as he is not his principal adviser regarding matters of law.... it is the job of his attornery general to advise the president and the cabinet about the matters pertaining law and all resolutions if they are at per with the existing contracts and all bilateral agreement we are member
 
Come on, one of the responsibilities of the Minister is to advise the President on matters pertaining to law of the country, among others , while the AG is responsible , among , to advise the President on legal technicalities.........
 
kwan
It is a pity Kabudi hawezi kumweleza Rais kuwa Mh. sheria na taratibu ziko hivi, tufanye hivi na hivi! Lisu hatasikilizwa, kisa mpinzani!
Mh. Rais kweli hawa wote ukimwacha Lisu ambaye ni upinzani, hawakutaki au hawaitakii mema nchi yetu?
kwan rais
Kitu ambacho JMP anafanya ni kujiandalia DOWANS nyingine na figusu figusu za aina hiyo ... yote mikataba alishiriki kuipitisha halafu leo anaunda jopo... unafiki mtupu...na hivyo vipengere anavijua sana na bado anataka kupambana ngangari...si watuwekee basi hiyo mikataba wazi ili tuwaambie cha kufanya.. tunajdiri tu kwa kutokujua kilichomo kwenye mikataba hiyo ...

Kwan JPM kasema anavunja mikataba? Mbona kama mnabadilisha lengo la ripoti
 
Back
Top Bottom