Kampuni ya uchimbaji madini ya Uingereza, Resources Indiana kuishitaki Serikali ya Tanzania kwa ukiukwaji wa mikataba

The Assassin

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
4,355
17,321
Kampuni ya uchimbaji madini ya Indina Resources kutoka Uingereza imeitaarifu serikali ya Tanzania nia yake ya kuishitaki kwenye mabaraza ya usuluhishi kwa ukiukwaji wa mikataba ya uwekezaji kati ya Tanzania na Uingereza.

Kampuni inaituhumu Tanzania kwa kukiuka kitu kinaitwa protection and promotion of investments and international law on project hasa baada ya serikali kufanya marekebisho ya sheria ya madini ya mwaka 2010 na sheria yya haki za madini(mineral rights and regulations 2018) ambayo ilifuta na kuondoa haki za kimkataba zilizoingiwa huko nyuma bila kufuata utaratibu.

Indiana imemuandikia barua rasmi na kumkabidhi Mheshimiwa Rais, Msuluhishi mkuu wa serikali na wizara ya madini.

Kwenye hii notice yao wanasema kuna leseni zaidi ya 10 za makampuni ambayo serikali imevunja mikataba yao ya uwekezaji.

Mkurugenzi wao anaonya kua kuwekeza Tanzania ni hatari sana kwa sbaabu pesa yako inaweza kutaifishwa na serikali wakati wowote. Anaonya kua Tanzania sio salama kwa uwekezaji, haitaki wawekezaji.

Soma mwenyewe hapa.
 
Attachments

  • 20200115-IDA-Ntaka-Hill-Government-Action.pdf
    485.3 KB · Views: 3
Aanze na waliitia saini kwenye mikataba isiyo na manufaa kwa taifa. Waeleze kwanini wasifunguliwe msshitaka ya matumizi mabaya ya ofisi huku mshsuri mkuu kisheria , wa serikali akivimbiana minyamanyama ofisini na kusahau kushughulikia maswala haya muhimu.
 
Juzi ilikuwa Winshear ya Canada Leo tena hawa, sifahamu kesho atakuwa nani?

Labda Palamagamba aliliona hili alipokuwa anabadili mikataba na akaona gharama za hizi kesi ni ndogo kuliko faida ya kubadili mikataba.
Palamagamba hana uwezo wa kuona hayo, yule jamaa brain yake ilishakua contaminated, ni mtu wa kujipendekeza zaidi kuliko kawaida.
 
Daah kama ni kweli ina maana hii ni kampuni nyingine tena!!?
Kampuni ziko nyingi tu zinafuata. Kuna mahala tulikosea, kubadili sheria na kufuta mikataba tuliyoingia huko nyuma bila kufuata utaratibu. Mikataba tuliingia wenyewe tena kwa kushangilia, wazee wa ndiyooo kila siku, sasa tumehsingia mkenge ndio tunashtuka kuivunja bila kufuata utaratibu.

Baadae tunaweza kuja kujikuta tuna mashitaka mengi sana kwenye mabaraza ya usuluhishi.
 
Ndio matokeo ya watu kutenda bila ya kufikiria. Tundu Lissu alisema haya lakini watu toka mtaa wa Lumumba wakamkejeli vilivyo. Ndio maana Mchungaji Peter Msigwa aliwaambia kuwa ccm wanachukua muda mrefu sana kuelewa vitu wanavyoambiwa kwa muda huo.
Asipobadilisha hizo sheria na akakaidi hukumu za arbitrators tusubiri vikwazo vya uchumi.
 
Kampuni ziko nyingi tu zinafuata. Kuna mahala tulikosea, kubadili sheria na kufuta mikataba tuliyoingia huko nyuma bila kufuata utaratibu. Mikataba tuliingia wenyewe tena kwa kushangia, wazee wa ndiyooo kila siku, sass tumehsingia mkenge ndio tunashtuka kuivunja bila kufuata utaratibu.

Baadae tunaweza kuja kujikuta tuna mashitaka mengi sana kwenye mabaraza ya usuluhishi.

Wakamate BUNDI WOTE YAISHE
 
Nakumbuka Tundu Lissu alishauri njia sahihi za kuvunja mikataba zifuatwe; aliongelea sana hii kitu na akatahadharisha utaratibu sahihi usipozingatiwa nchi itashtakiwa. Naona yale yote aliyoongea yanaanza kutimia moja baada ya jingine. Kuna watu huko mbele ya safari watatakiwa kunyongwa ili iwe fundisho kwa wengine maana hasara waliyoliingiza taifa haina mfano. Yetu macho!
 
Mawakili wetu kama nawaona vile... Wanapiga jalamba mkao wa kula na kwenda kusafisha macho ughaibuni...

Jr
... halafu watarudi mikono mitupu maana kitakachowapeleka huko is not of their interest!
 
Kampuni ziko nyingi tu zinafuata. Kuna mahala tulikosea, kubadili sheria na kufuta mikataba tuliyoingia huko nyuma bila kufuata utaratibu. Mikataba tuliingia wenyewe tena kwa kushangia, wazee wa ndiyooo kila siku, sass tumehsingia mkenge ndio tunashtuka kuivunja bila kufuata utaratibu.

Baadae tunaweza kuja kujikuta tuna mashitaka mengi sana kwenye mabaraza ya usuluhishi.
Magufuli hana nia njema kwa taifa hili. Anatuyumbisha sana!
 
Back
Top Bottom