Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar aliyefukuzwa kuwa Mgombea Mwenza

simplemind

JF-Expert Member
Apr 10, 2009
16,409
9,183
Hatimaye, Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa atua Chadema baada ya kukubaliana rasmi katika kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kilichomalizika saa 8 usiku kuamkia leo.

Kamati Kuu ya CHADEMA, ilikutana jana katika kikao cha dharura kwenye hoteli ya Bahari Beach, Kunduchi Dar es Salaam, na kufikia uamuzi wa kumpokea Lowassa.

Atatangazwa rasmi kesho Jumanne, Bahari Beach Hotel Dar es Salaam kwa tukio ambalo litarushwa live na ITV, saa 10 jioni. Mamia ya watanzania watashuhudia kupitia kwenye tv zao.

Lowassa alikuwa miongoni mwa wanaCCM 38, waliyotia nia kugombea urais wa Tanzania kwa mwenvuli wa chama hicho. Alikatwa katika hatua ya awali na Kamati ya Maadili ya CCM.

Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar na kutimuliwa baada ya Bunge la Katiba, Othman Masoud ametajwa kuwa Mgombea Mwenza wa Edward Lowassa.

Mwanasheria huyo aliyebobea ndani ya taaluma hiyo, kesho atachukua kadi ya CHADEMA na kuwa mwanachama kamili ili kuweza kukidhi taratibu, kanuni na sharia za Tanzania za mfumo wa vyama vingi na za uchaguzi.

Aidha, kuna tetesi kuwa Othman Masoud, anaandaliwa kuwa mgombea urais kwa mwaka 2020 ama kwa nafasi ya Muungano au Zanzibar.

Othman Masoud ni Mwanasheria wa Kwanza kujitokeza wazi wazi kuitetea Zanzibar, bila kutanguliza maslahi yake. Othman Masoud kwa sasa si mwanachama wa chama chochote cha siasa..
 
Huyu Othman ni mume wake Batilda Burian..

Nakumbuka alijitoa muhanga kutetea katiba ya Wananchi..(warioba)
 
Kama ni huyu Othuman sina wasiwasi naye, nakumbuka kwenye bunge la katiba aliletwa kupiga kura chini ya ulinzi mkali lakini bila hofu akapiga kura ya wazi ya HAPANA.
 
UKAWA nimewapenda bure! Hizi mbinu ni za kuua mtu! Safari hii sangara (CCM) anajikaanga kwa mafuta yake mwenyewe! CCM wanasambaratishwa kwa silaha za wenyewe!
 
Yaani masaa hayaendi huo muda ufike kamanda Lowassa apokelewe rasmi...RIP CCM!
 
nimekubali sasa kuna watu wanajua kufikiri wanangu acheni kabisa maana angalia lowasa na mwanasheria mkuu af kompea magufuli na yule mama yetu kuweni wakweli. CCM kwa heri wellcom ukawa magufuli hana jinsi aliuingia mkenge
 
Jamani UKAWA Noooooooomaaaaaa.....CCM huku wamepatwa na ganzi ya macho....


hali ni tete...wanasubiri ubabe wa mkapa...mtaisoma namba............
 
Baada ya UKAWA kumsimamisha lowasa kuwa mgombea urais kwa tikeki ya UKAWA, pia umoja huo umemteu aliekuwa mwanasheria mkuu wa serekali ya Zanzibar mh Othman masoud kuwa mgombea mwenza wa ukawa kesho panapo majaaliwa mh Othman masoud atachukuwa kadi ya chadema ili awe mwanachama ili apate kugombea.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom