Mwanasheria mkuu wa marekani hatiani

marveljt

JF-Expert Member
Jan 11, 2017
1,503
1,479
Mwanasheria mkuu wa Donald Trump amehutumiwa kuwa alifanya mawasiliano na balozi wa urusi wakati wa kampeni. Hivyo ameombwa kujiweka pembeni ili uchunguzi dhidi yake ufanyike. Je ,hapa kwetu nani yuko radhi kupisha uchunguzi? Ingawaje bado hajajiuzulu ni dhahiri kuwa atafanya hivyo.
 
Trump asije maliza miaka yake yote minne kwa matukio kama huku kwetu bila maendeleo yoyote ila visa kila siku
.
.
.
Kyenekyaka mkighanile une
 
Trump asifaye makosa ya kukubalii mteule wake mwingine ku-resign - ashirikiane na chama chake ambacho kinaongoza Bunge ili kiweze kukomesha upuuzi huu ambao unaonekana umeanza kuota mizizi.

Trump akiendelea kuwa sloppy basi wapinzani/maadui wake wataendelea kutafuta mbinu za kumuondoa Madarakani, akiwakomalia mapema wataanza kufikiria mara mbili kabla hawaja attempt mbinu mpya.
 
Kosa kubwa alilofanya ni kuwa aliulizwa na Senate kama aliwahi kukutana na Balozi wa Urusi Wakati wa kampeni za Uchaguzi wa Rais, akakataa kata kata Wakati FBI walishajua kitambo ukweli wa mambo. Hivyo alisema uongo chini ya kiapo na hilo kwa wenzetu ni kosa kubwa sana. Kwetu tungesema "Jamani ni binadamu alisahau na ingeishia hapo".
 
Kwa mwendo wa trump unaelekea kama wa sizonje. Juzi alitoa taarifa kuhusu kazi,viwanda vya us kama jamaa wa viwanda. Mwezi uliopita mtu aliyemteua alijiuzulu,leo tena huyu mwanasheria. Yeye atakuwa ni mtu wa kuteua mda wote. Alizuia baadhi ya mataifa kuingia us ila mahakama ikazuia tamko lake. Yaani hata kwenye nchi ya wadanganyika nadhani pangekuwa na mahakama bora na viongozi wa upinzani wenye uelewa hata zonje angekuwa kwenye shida sana
 
Bwana Jeff sessions ana kazi ngumu....ila naona Speaker Ryan ashaanza mkingia kifua.
 
Bado watu wanateuliwa na kupanguliwa.

I wonder where the adm is, in terms of the schedule.
 
Trump asije maliza miaka yake yote minne kwa matukio kama huku kwetu bila maendeleo yoyote ila visa kila siku
.
.
.
Kyenekyaka mkighanile une
Obama na wenzake ndo wanahaha.

Katika mwezi mmoja tu kapunguza deni la taifa kwa USD 18 Billion, wakati Obama katika mwezi mmoja alipandisha deni kwa USD 222 Billion.

Jamaa anapiga mzigo taratibu, baada ya muda kazi yake itaonekana na watashikwa na aibu hao akina Obama.
 
Breaking News: U.S. Attorney General Sessions recuses himself from Russia investigations!

Hatimaye Mwanasheria Mkuu (AG) wa Serikali ya Donald Trump, Jeff Sessions, asalimu amri na kutangaza kujiweka kando (recuse himself) katika uchunguzi unaotarajiwa kufanyika kuhusu tuhuma za Urusi kuingilia mchakato wa uchaguzi wa Marekani. Kabla ya kutangaza uamuzi huo bosi wake, akijibu swali aliloulizwa, alisema bado ana imani kubwa naye na kwamba hakuwa na taarifa yoyote kuhusu madai ya mkutano wa AG wake na balozi wa Urusi. Je huu ndio mwisho au kuna zaidi? Tuzidi kuvuta subira...!
 
Trump asifaye makosa ya kukubalii mteule wake mwingine ku-resign - ashirikiane na chama chake ambacho kinaongoza Bunge ili kiweze kukomesha upuuzi huu ambao unaonekana umeanza kuota mizizi.

Trump akiendelea kuwa sloppy basi wapinzani/maadui wake wataendelea kutafuta mbinu za kumuondoa Madarakani, akiwakomalia mapema wataanza kufikiria mara mbili kabla hawaja attempt mbinu mpya.
Huu upuzi wako ungewezekana hapa Tanzania tu, nchi isiyostaarabika inayowakumbatia viongozi wa hovyo wasio na weledi, hekima wala busara wakitegemea kung'ang'ania kubaki madarakani kwa kutumia vyombo vya dola. Pia kumbuka katika maswala yanayogusa maslahi ya taifa tofauti za kichama huwekwa pembeni na badala yake utaifa ndio hupewa kipaumbele.
 
Trump asifaye makosa ya kukubalii mteule wake mwingine ku-resign - ashirikiane na chama chake ambacho kinaongoza Bunge ili kiweze kukomesha upuuzi huu ambao unaonekana umeanza kuota mizizi.

.
Trump hana option. Kitu kizuri kuhusu US ni kwamba Institutions za kule zinafanya kazi inavyopaswa kwa kiasi kikubwa sana. So, jamaa akichunguzwa na kuthibitishwa kuwa alifanya mawasiliano yasiyokubalika na Urusi, itabidi aachie ngazi tu.
 
Huu upuzi wako ungewezekana hapa mcb me tu, nchi isiyostaarabika inayalwal$alqhehPafafzowakumbatia viongozi wa hovyo wasio na weledi, hekima wala busara wakitegemea kung'ang'ania kjiiijiaubaki madarakani kwa kutumia vyombo vya dola. Pia kumbuka katika maswala yanayogusa maslahi ya taifa tofauti za kichama huwekwa pembeni na badala yake utaifa ndio hupewa kipaumbele.

Mag3!! Kitu cha kwanza ujifunze kuheshimu binadamu wenzako hata kama mnatofautiana kimsimamo/maoni - mwanzo nilikuwa naku-ignore ulipokuwa una qoute comments zangu na anazijibu kwa kutumia an abbrasive language, hivi sasa naona umeanza kuwa carried away kwa kufikiri unaweza kuwajibu jibu watu kwa kutimia lugha za vijiweni na sisi uwezo huo tunao sana ila tunajiheshimu na kuheshimu binadamu wenzetu hata am@ gatukubakiani na,maoni yao.

Once again nakupa onyo la mwisho
 
Huu utawala wa Bwana Trump haujatulia kabisa
Donald Trump anahujumiwa kutokana na tabia yake. Sidhani kama utawala wake utamaliza salama ingawa wakati wa khutba ya bunge jumanne iliyopita alionekana kuongea kwa tahadhari sana.
 
Back
Top Bottom