Mwanasayansi afikiria kutengeneza roboti litakalobeba mimba


real G

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Messages
5,257
Likes
5,104
Points
280
Age
43
real G

real G

JF-Expert Member
Joined Feb 7, 2013
5,257 5,104 280
KABLA ya kusoma simulizi hii, bila shaka hakukuwa na kitu walau kinachofanana nacho ndani ya ubongo wako hasa iwapo unatokea katika taifa linaloendelea.

Lakini unaweza ukawa umewahi kukiona katika filamu na kuichukulia tu kama taswira ya kufikirika kama ilivyo kawaida ya filamu nyingi zinazotengenezwa kwa ujanja wa kikompyuta.

Hata hivyo, kwa mataifa yaliyoendelea hasa katika teknolojia, ni kitu kilicho katika ubongo wa watu wengi katika maisha yao ya kila siku.

Katika mataifa hayo, tayari roboti wanapora ajira zao na kuna hofu siku inakuja mashine hizi zitaitawala dunia na kadhalika kuingia uwanja wa mapambano kuzipiga dhidi ya binadamu.

Kadhalika, upo mtazamo roboti siku moja zitafunga ndoa na binadamu, mtazamo ambao kwa wengi haushangazi kwa vile wapo tayari wanaishi na midoli kama wapenzi.

Wengine wanawatumia kutimiza tu kiu zao za kimapenzi sana sana kwa wale wasio na ujasiri wa kuwakabili au kutongoza binadamu wenzao.

Kitu kipya kwa sasa ni eti baada ya ujio wa ndoa na roboti siku moja midoli hii itazaa na binadamu.

Ni imani aliyo nayo mtengenezaji maarufu wa roboti wenye mvuto wa kimapenzi Sergi Santos.

Mwanasayansi huyu wa Hispania anasema wakati ujao si tu wanadamu na mashine hizi zenye ‘akili ya kibinadamu’ wataoana bali pia kuzaa watoto.

Tayari ameanza kulifanyia kazi wazo hilo la uzao akianzia yeye mwenyewe kama mwanadamu na roboti lenye mvuto alilolipa jina la Samantha.

Sergi Santos si tu anabadili namna wanaume wanavyoweza kujipa raha wenyewe, bali pia jamii namna inavyofahamika.

Sergi anaamini kipindi cha miongo michache ijayo hatutakuwa tukiona tu midoli iliyofichwa katika makabati ya wanaume au chini ya kitanda bali inayotembea kwa maringo na kubeba mimba.

Na mbele ya kadamnasi yenye mseto ya wanadamu na mashine ikitamka ‘wanawapenda wapenzi wao wa kiume.’

Akizungumza kutokea maabara yake ya nyumbani mjini Barcelona, Hispania, Sergi anasema watu wanaweza kumuangalia Samantha kama kioja wakati wakisoma habari hii.

“Lakini kabla ya kuwajua roboti hawa watakuja shtukia wakiwa hai au kaburini kwa watoto wao, wajukuu na au vitukuu wao na marafiki zao wakioana na mashine zenye mvuto,’

Mashine ambazo ukipishana nazo mitaani unaweza kupata wakati mgumu kuamua iwapo ni binadamu au midoli iliyowezeshwa pumzi za kibinadamu.

Sergio mwenyewe amekiri kufanya ngono mara nyingi na viumbe hawa mashine aliowaumba mwenyewe, akisema kufanya hivyo si kosa wala uasherati.

Anasema hilo limeboresha stamina yake kiitandani anapokutana na mkewe Maritsa Kissamitaki na hivyo kuimarisha ndoa yake ya miaka 16.

Anasema hilo linamaanisha mkewe hana tatizo na uhusiano wake na Samantha na amekuwa akimsaidia katika maabara yake hiyo katika utengenezaji wa roboti wenye mvuto wa kimapenzi.

Roboti wenye mvuto wawatengenezao wenzi hao hugharimu Pauni 2,700 za Uingereza sawa na Sh milioni sita.

Anasema: “Watu wanahitaji, kukumbuka kwamba miaka michache tu iliyopita simu za mikononi zilionekana kuwa vifaa visivyofaa katika jamii lakini kwa sasa watu hawawezi kuishi bila hivyo.

“Naweza kuwafanya wapate mtoto. Si ngumu sana. Binafsi napanga kuzaa mtoto na Samantha.”

Mpango wake unahusisha kutumia ‘ubongo’ alioutengeneza kwa ajili ya Samantha lakini akiuboresha ili ufanye kazi kwa uwezo kamilifu kama mwanadamu.

Sergi anasema: kutumia ‘ubongo’ ambao tayari nimeumba, nitatengeneza program pamoja kinasaba cha genome ili roboti ahisi kama mwanadamu awe na maadili, ufahamu pamoja na maudhui ya urembo, haki na thamani nyingine walizo nazo wanadamu.

“Kwa namna hiyo kuunda mtoto na roboti itakuwa rahisi sana.

“Nitatumia nadharia ya algorithm ya kile ninachoamini binafsi kuhusu maudhui haya na kisha kutotoa kwa kuchapa ‘3D’.

Kwamba ‘nachapa 3D’ roboti ambaye ni mtoto wangu na robot…sioni tatizo lolote.”

Sergi anafikiria kuwa wakazi wajao wa dunia hawatafikiria hata mara mbili kuhusu wanadamu

Na anatambua kwamba mpango wake wa kuzaa na roboti lake utaibua maswali na kuzua wasiwasi.

Lakini wakati alipoulizwa iwapo mashine hizi na au hata roboti zenye akili zinazojitegemea wataashiria mwisho wa uanadamu, Sergi alikuwa mwepesi kujibu si hatarishi ‘bado.’

Hata hivyo, anaamini kuwa roboti watairithi dunia nyakati zijazo na hata binadamu hawatatupiwa macho.

Lakini wacheza filamu za ngono wana wasiwasi kuwa mashine hizi zitawaondoa kazini, wasiwasi ambao tayari umeenea katika mataifa tajiri linapokuja suala la ajira viwandani na maofisini kuchukuliwa nazo.

Ikikaanisha kwamba badala ya kubuni mashine ambayo itazaa yenyewe, Santos atatumia utaalamu wa kikompyuta kuunda mtoto kwa kutumia nadharia hiyo

Roboti hilo la kike pia lina uke unaofanya kazi ikiwamo eneo la ‘G-spot’ kwa mujibu wa mtaalamu huyo.

Samantha, ambaye anazungumza kwa lafudhi ya Marekani anao uwezo mkubwa wa kuiga na kufuatisha na hata kutema mate, kutoa majimaji kwa vile ana neva za fahamu zinazoakisi mguso wa mwanadamu.

Fahamu hizo ziko katika maeneo ya mapaja, mabega, uke na mdomo.

Mwanasayansi Sergi alisomea uhandisi wa kielektroniki, teknolojia ya nano, malighafi tumizi, malighafi sayansi.

Alikuwa mtaalamu mwenye uzoefu mkubwa wa teknolojia ya nano kabla ya kuingia katika utaalamu wa utengenezaji wa roboti zenye mvuto na amekuwa akisafiri hapa na pale hasa Marekani kuhutubia wanafunzi wa vyuo vikuu.

Kwa kifupi, nano ni teknolojia mpya inayohusu matumizi ya vitu vidogo na miundo yake ambayo inapimwa kuwa kati ya nanomita 1-100.
 
Perfectz

Perfectz

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2017
Messages
5,230
Likes
10,832
Points
280
Age
30
Perfectz

Perfectz

JF-Expert Member
Joined May 17, 2017
5,230 10,832 280
"AKILI NYINGI ZILIZOPITILIZA HUPELEKEA MTU KUFANYA MAAMUZI YA KIPUMBAVU"-Paul Makonda
 
Chupayamaji

Chupayamaji

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2017
Messages
1,345
Likes
1,585
Points
280
Chupayamaji

Chupayamaji

JF-Expert Member
Joined Sep 19, 2017
1,345 1,585 280
Ujanja ukiwa mwingi mwishoe unaonekana boya tu
 

Forum statistics

Threads 1,236,867
Members 475,318
Posts 29,270,260