Mwanao na Mtumizi ya Mtandao

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Kutakuwa na mkutano katikati ya mwezi huu huko Makao makuu ya ITU Nchini Uswizi , Moja ya mada itakayojadiliwa kwenye kikao hicho Ni Masuala ya Mtoto na Mtandao – Usalama Wake , Hii haiwezi kupita bila kuziangalia nchi zetu zilizo chini ya chini ya jangwa la sahara , Kama Tanzania , Malawi , Msumbiji , Zambia na zingine nyingi ila nimeamua kutaja hizo chache kama mfano kwa sababu nchi hizo hazijafanya hatua za kutosha katika kuhakikisha watoto na vijana wao wanakuwa salama zaidi pindi wanapotumia mitandao .

Kwangu mimi nafikiri kuna vikwazo 3 vikuu katika kudhoofisha jitihada za kupambana na uhalifu dhidi ya watoto kwenye mitandao na hii sio kwa nchi hizi chini ya jangwa la sahara tu hata kwa nchi zingine ambazo hazijakuwa sana kwenye masuala ya teknohama .

Suala la kwanza limeonekana ni lugha watoto wengi sana wanajiunga kwenye mitandao ya jamii kama facebook na mengine ambayo wanaweza kujifungulia anuani za barua pepe au kujipatia huduma zingine yale maelezo yanayotolewa kwenye tovuti hizo ni kwa lugha ya kiingereza inakuwa ngumu kwa watu wengi kusoma na kuelewa kile kinachotakiwa kutekelezwa na wasimamizi wa watoto hao au watoto wenyewe ni vizuri mitandao ya jamii kama facebook na mengine mingi ili na uwezo wa lugha nyingi zaidi na nyepesi kwa ajili ya watu kuweza kuelewa vizuri .

Pili ni masuala mengine ya kijamii mfano kwa afrika watoto wengi sio wawazi kwa wazazi wao au hata wazazi hawana mawasiliano ya karibu na watoto wao na kuweza kujua au kuhadidhiana masuala yanayoendelea kwenye mitandao haswa hiyo ya jamii , hii inaweka watoto wengi mbali na wazazi wanashindwa kufuatilia kwa sasa kwa mfano ni rahisi kukuta mtoto anawasiliana na mtu kupitia mtandao wa facebook na kubadilishana nae mawasiliano bila mzazi kujua chochote .

Tatu ni mifumo yetu ya kisheria haijakaa sawa katika kuhakikisha mtoto mdogo anapewa haki zake kwenye masuala kadhaa ya mawasiliano hata nchi nyingi zilizofanikiwa kuwa na taasisi zinazohusika na masuala ya teknohama hazina vitengo au sehemu zinazozungumzia masuala ya watoto na mitandao hili limekuwa pigo kubwa sana sio kwa nchi za chini ya jangwa la sahara tu ni maeneo mengi sana .

Hayo ni masuala machache ambayo yalijadiliwa kwenye kikao hicho Ahsanteni watu wa afrika ya mashariki ambao walishiriki kwenye kikao hicho kwa njia ya mtandao naamini mawazo haya na mengine mengi yatafikishwa kwenye jumuiya zenu na sehemu zingine za kikazi ili kuweza kumkomboa mtoto wa kiafrika na mambo yanayoweza kutokea huko mbeleni kama hali ikiendelea kuwa hivi .

Mafunzo na masomo haya ya kumkomboa mtoto kwanza yanzie mashuleni , majumbani iwe kama utamaduni kisha ndio watu sasa waanze kuzoea na kuwa na utamaduni huu , binafsi nilishangaa nilipotembelea shule moja ya kimataifa na kukuta watoto wanaachiwa kutumia komputa zilizounganishwa na mtandao wenyewe bila msaada wala usimamizi wowote wanaruhusiwa kufanya chochote wanachotaka .

Na zaidi ya yote nilishangaa sana tu nilipomwa mdogo wangu wa miaka 10 ameniomba urafiki kwenye anuani yake ya mtandao jamii nilishtuka sana nilipochunguza niligundua alitengeneza anuani hiyo kupitia shuleni kwao .

Hapa kwetu Tanzania tuliwapi kuipa wiki moja nzima kwa ajili ya usalama wa watoto kwenye mitandao , lakini hatukuelezwa kwa maandishi ni nini kiliendelea baada ya hapo serikali na wadau mbalimbali haswa wanaoendesha huduma za mawasiliano kwa njia ya simu na komputa wamejipanga vipi ni miaka sasa imepita .

Mwisho na kupendekeza mpango wa Kampuni zinazotoa huduma ya mawasiliano ya Internet Afrika Mashariki kuanzisha vitengo vya kusaidia watoto na ushauri kwa wazazi kwa lugha ambazo zinazungumzwa , pia wawe na mafunzo ya mara kwa mara kwenye mashule na maeneo mengine ambapo watoto wanatumia sana mtandao ili kuweza kwenda sawa na dunia ya sasa , vyombo vya usalama kujiweka sawa na mabadiliko haya .

Pamoja tutafika .
 
Back
Top Bottom