Mwanangu wa miezi sita (6) anaumwa mafua hatari.

Abdul Mganyizi

JF-Expert Member
Oct 28, 2019
1,044
1,996
Ndugu zanguni habari za wakati huu,mwanangu wa miezi sita (6) anaumwa mafua mpaka huruma .Naomba anaejua dawa gani naweza nunua itakayomsaidia huyu mtoto.Nitashukuru kwa majibu matakayonipa
 
Mpeleke hospitali anaweza akawa anatatizo lingine ndani yake Kama huwa anapata hilo tatizo mara kwa mara, watoto huwa wanatibiwa kwa uamgalifu sana. Huwezi ambiwa dawa hapa mtandaoni.
 
Kama ni mafua ya muda mrefu na hayaponi Basi jaribu kumpeleka hospitali yawezekana anasumbuliwa na nyama za puani,..kwa sasa inasumbua Sana watoto wengi...
 
Mtandao ndio sehemu ya mwisho unayopaswa kutafuta tiba ya mtoto.
Kimbilio lako la kwanza ni hospitali. Kuna mtu kaandika hapo juu, watoto huwa wanatibiwa kwa uangalifu sana. Huwezi kujijaribia midawa tu ya mtandaoni.
 
Inategemea ameanza lini. Kama yana muda mfupi mnyonyeshe sanaa,na mvishe masweta. Ukiona hayaponi basi nenda hospital. Hali ya hewa ya sasa tunaelekea kipupwe,watoto wengi wanaathiriwa.

Maziwa yanamwongezea mtoto kinga mwili(body immunity) kwa kiwango kikubwa sana.
 
Tatizo la mafua limetamalaki ghafla na watoto wengi kwasasa wanasumbuliwa na shida hii.
Waweza mnunulia Abnal yenye Sodium Chloride, kisha mwekee 2 drops kwenye kila tundu la pua na kwauwezo wa Mungu pua zitazibuka.
Kama akizidiwa mpeleke kwa wataalamu wa magojwa ya watoto.
 
Mpeleke hospitali wadau mshaurini hivi bhas inatosha apelekwe hospital huyu mtoto kazaliwa na mzaz mpumbavu anatafuta tiba mitandaoni
 
Peleka Hospitali mtoto.

Muweke mazingira Safi yasiyo na vumbi, hakikisha baridi haimpati hasa ya usiku.

Mnyonyeshe vyakutosha
 
Peleka mtoto Kwa daktari wa watoto, siyo kila daktari anaelewa matatizo ya watoto!

Utapata ushauri na tiba sahihi,
Pole sana, wengi tunakuona ni uzembe. Humu utapata kila Aina ya ushauri, mpige nyungu, mpe juice ya pilipili kichaa, n.k, peleka mtoto hospital!
 
Chukua mafuta ya samli(mafuta ya maziwa ya ng'ombe) mpake kutwa x 3 mwanzoni mwa mapua yake
 
Back
Top Bottom