DOKEZO Mwanangu ameuawa kwa kupigwa na Mwalimu lakini kesi inazungushwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Naitwa Janeth Shayo, mkazi wa Uru, Moshi. Naomba unisaidie kupaza sauti mwanangu Jonathan Makanyaga (07) mwanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi Mrupanga, ameuawa kwa kupigwa na Mwalimu lakini kesi inataka kupindishwa.

Tar.28/02/2024 mwanangu alienda shuleni akiwa mzima. Alipofika aliadhibiwa kwa kuchelewa "namba". Alipoingia darasani alianza kutokwa damu puani na mdomoni. Akarudishwa nyumbani. Nilipomkagua nikamkuta na majeraha yaliyovilia damu mgongoni, kwenye mbavu na mguuni.

Kesho yake nikaenda nae shuleni kutaka kuoneshwa mwalimu aliyemfanyia ukatili mwanangu. Lakini Mwalimu mkuu akaomba nibaki nje. Akaingia na mwanangu ofisi ya walimu na kumtaka amtambue Mwalimu aliyemuadhibu. Mwanangu akamtanbua. Mwalimu Mkuu akaniambia wameshamfahamu ni mwalimu wa "Field" hivyo atazungumza nae.

Wakanipa 20,000/= za matibabu. Nikampeleka mwanangu zahanati. Kesho yake akazidi kutoka damu, na kulalamikia maumivu sehemu za mbavu. Nikampeleka hospitali ya masista. Daktari akaniambia bandama imejeruhika ndio sababu ya kutoka damu mdomoni. Mtoto alidai pamoja na viboko alivyochapwa, Mwalimu pia alimpiga ngumi tumboni. Huenda ndiyo iliyopasua bandama.

Hali yake ilizidi kuwa mbaya tukapewa rufaa kwenda KCMC. Akatakiwa kufanyiwa upasuaji. Gharama 350,000/= lakini sikuwa nayo. Nikapiga simu shuleni wakasema tuombe afanyiwe halafu watalipa baadae. Hata hivyo kabla hajafanyiwa hali yake ikazidi kuzorota, akashindwa kupumua, akawekwa kwenye Oxygen. Akashindwa kula, akawekewa mpira wa chakula. Baada ya siku chache akafariki 😭.

Lakini ripoti ya hospitali inasema mwanangu amekufa kwa kansa ya damu. Kansa gani ya damu inayomuua mtoto kwa wiki mbili? Na kwanini hiyo kansa itokee baada ya kuadhibiwa shuleni? Kwanini Mwalimu aliyemuadhibu mwanangu anafichwa, na sipewi haki ya kumfahamu?

Nalazimishwa nichukue maiti nikazike lakini nimekataa. Nataka uchunguzi huru. Nimeenda dawati la jinsia kulalamika nikapuuzwa. Nimepiga simu kwa Waziri Dkt. Gwajima D akanipa namba ya mtu wa kunisaidia. Nilipopiga kumbe ni yuleyule Mkuu wa dawati la jinsia aliyenipuuza. Nikamrudia Gwajima akasema niwasiliane nae huyohuyo. Nimekosa pa kulilia haki ya mwanangu Jonathan
Sheria mkononi ihusike hapo.. wanakijiji vipi huko?
 
Huyo mwalimu wa field ana nini cha kumpooza huyo mama ajikwamnue kiuchumi?
ndo ujiulize huyo mama sasa hv anataka nini iwapo mwanae hatupo nae duniani ? na majibu ya daktari yanasema NI KANSA YA DAMU , je kwann haamini haya majibu ? tuanzie hapo ndo tuje kwenye ana nini cha kumpooza huyo mama

Sent from my HUAWEI NXT-L29 using JamiiForums mobile app
 
Bado haujasema, kituo cha afya nacho kina watu wenye taaluma sawa na wa KCMC kinachotofautisha ni hadhi ya sehemu husika na vifaa
sasa Heshimuni majibu ya KCMC , huyo mama kama anagomea majibu na anataka majibu yake kuwa mwl ndo kamuua mwanae bas aje na vipimo vyake

HAWA WAZAZ WAKIPOTEZA WATOTO WAO PENDWA BASI LOLOTE LINALOWEZEKANA KULIFANYA LIWE SABABU HULISIMAMIA MPK MWISHO

Sent from my HUAWEI NXT-L29 using JamiiForums mobile app
 
ndo ujiulize huyo mama sasa hv anataka nini iwapo mwanae hatupo nae duniani ? na majibu ya daktari yanasema NI KANSA YA DAMU , je kwann haamini haya majibu ? tuanzie hapo ndo tuje kwenye ana nini cha kumpooza huyo mama

Sent from my HUAWEI NXT-L29 using JamiiForums mobile app
Suala sio kumpooza huyo mama suala ni iwapo kuna mwalimu anafanya ukatili kwa watoto anafichwa.
 
Majibu ya dakAtari mwenye D MBILI hayawezi kuheshimiwa.

Yamepimwa katika uzani na kuonekana ni majibu ya kanjanja yasiyo na uzito wowote wa kitabibu.

Huyo daktari akamatwe na anyang'anywe leseni yake kwa kosa la kuwa na vigezo duni vya kitaaluma na kudhihirisha ukanjanja mahala pa kazi.

Sijui ilikuwaje huyu mwizi wa vyeti akakoswa na rungu la Magufuli. I wonder my dear.

Cc Lamomy
hahahaa ila we jamaa ni sufuriii

Sent from my HUAWEI NXT-L29 using JamiiForums mobile app
 
Yani mtu unakuwa na stress hadi unampiga ngumi mtoto wa darasa la kwanza ngumi? Aiseee hii ni mbwa sio mwalimu!
Hayo ni matokeo ya uongozi mbovu katika shule....walimu wanashindwa kusimamiana na kuchunguzana kila mmoja anafanya atakavyo
 
ndo ujiulize huyo mama sasa hv anataka nini iwapo mwanae hatupo nae duniani ? na majibu ya daktari yanasema NI KANSA YA DAMU , je kwann haamini haya majibu ? tuanzie hapo ndo tuje kwenye ana nini cha kumpooza huyo mama

Sent from my HUAWEI NXT-L29 using JamiiForums mobile app
Anataka majibu yasiyo na shaka. Yeye kaona majeraha ya fimbo, hospital ya kwanza wamesema mtoto bandama limepasuka na mtoto kasema alipigwa ngumi. anataka kujua ukweli. Hivi wewe angekuwa mwanao ungetoa majibu mepesi kama haya?
 
Ujinga ujinga tu na kupuuza mambo. Vaa viatu vya huyo mzazi halafu ujiulize kama iwapo ungeona ni sawa kutokusikia maelezo ya huyo mwalimu. UJINGA. We unaona ni sawa huyo mwalimu kutokuhojiwa?
mtatuzi wa mwisho ilikuwa majibu ya hospitali , je majibu kuanzia hatua ya kwanza yalisemaj mpk anafika kcmc ? majibu ya awali ni kuwa bandama ineharibika na alipofika kcmc wakamwambia ana KANSA YA DAMU ambapo dalili yake pia ni bandama kuharibika , lkn huyo mama anabishana na majibu ya kote huko na kwa maelezo ya huyo mama alipewa ela tu wala hawakundikiza hospitalini ili wakafodge majibu vzr , sasa huyo mwalimu alikuwa anaenda kuedit majibu au vp ?


KIFO KINAKUJA MUDA WOWOTE , HII ILIPASWA IWE FUNDISHO KWENU , PIMENI AFYA ZENU NA SIO KUSUBIR KUJA KUWASHUSHIA LAWAMA WENGINE

Sent from my HUAWEI NXT-L29 using JamiiForums mobile app
 
hahahaaa we jamaa kichwan mtupu kama mwijaku

Sent from my HUAWEI NXT-L29 using JamiiForums mobile app
Hehehe. Nyie madktari wenye D MBILI ni vituko, hamjafuzu umahiri wa kitabibu ndio maana mgonjwa wa majeraha ya mwili anaambiwa ana KANSA!

Full ukanjanja na kupiga ramli kama magoigoi ya kichawi. Uwezo duni wa kikazi na vigezo hafifu vya kitaaluma.

Mtu ana D MBILI ataweza wapi udaktari zaidi ya kubambia bambia tu na kutoa majibu feki ya kikanjanja! Hehehe 😹😹😹😹
 
kupiga ngumi na kuchapa vinafanana ? hoja ya mama bandama imeharibika kisa kapigwa ngumi na michirizi mgongoni , je WEWE UNAWEZA mpiga ngumi mtoto wa drs la kwanza NGUMI ? Ebu onesha utimamu wako

Sent from my HUAWEI NXT-L29 using JamiiForums mobile app
Uliwahi kuona ile video ya mtoto anapigwa na house maid Uganda? Mtoto wa miaka 2 au 3 hivi? Anapigwa mangumi na mateke kama mwizi? Kama kitu hujawahi kuona usiseme hakiwezekani. Dunia imejaa makatili ambao mtoto wako kwao ni kama paka tu wanaweza kumpiga hata panga akafie mbali.
 
Mwalimu anasemaje? Maelezo yake kuhusu hizo tuhuma. Alimpiga mtoto hakumpiga? Kwanini alifichwa hata kabla mtoto hajafariki?
mwl hakufichwa ndio maana aliingia ofisini na mtoto na kutaka kumjuwa mwl aliyefanya hivyo na kitaaluma mwl mkuu alifanya jambo jema sana , kibaya ni kuwa mwl.mkuu hakujuwa ukubwa wa ttzo , ila sio kila jambo lzm umseme.mwl mbele ya mzaz kwanza unaua CONFIDENCE pili unamweka MACHINJIONI kwa wazazi yaani kumuweka wazi mbele ya mzaz ni htr kiuslama hata kwa mwl husika akiwa kwenye makaz ya raia , huyo mwl mkuu katumia akili nyingi sana kukuzidi ww .

INGAWAJE HATA HIYO ELF 20 UKUTE KATOA MWL MKUU KUPUNGUZA MAKELELE

PIMENI AFYA ZENU ILI KUEPUKA KUWAPA WATU LAWAMA

Sent from my HUAWEI NXT-L29 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom