DOKEZO Mwanangu ameuawa kwa kupigwa na Mwalimu lakini kesi inazungushwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
DED anahojiwa anakuambia amefuatilia mpaka shuleni kabisa amejiridhisha bila shaka mtoto amefariki kwasababu ya cancer aisee!!
Record kutoka hospital ya mtoto kua na cancer ipo au hiyo cancer imekuja one onekana baada ya kifo cha mtoto!? Upelelezi uanzia hapo, ukiwahusisha na team ya wataalamu wa afya hadi wale wa forensic!!
 
Hivi inaingia akilini mtoto wa miaka saba kupigwa eti amechelewa shule? Hivi kwa umri huo yeye ndiye anapaswa kujua saa ya kuamka, kujitarisha na kwenda shule? Huoni huyo mwalimu ni mshenzi wa mwisho? Kwa nini asiwasiliane na wazazi kuhusu kuchelewa? Mambo mengine ni kujitakia na siwezi kumuonea huruma.
mbon kama umeamini maneno ya mama bia ushahidi ? na mm kesho nkijisema yangu tu juu ya walimu utaamini pia , walimu mnawapa presha sana , ndio maana wanatoa maboko sana siku hz sabab hawana waranty na kaz yao , mtoto kapigana anajich kesho anamsingizia mwl

Sent from my HUAWEI NXT-L29 using JamiiForums mobile app
 
kwan dalili za magonjwa zina muda maalumu ?

NLIWAI KUTANA NA MAMA MMOJA ALIKUWA ANAINGIA KWENYE KESI INAITWA PRESBYOPIA ( mabadiliko ya ukuaji kuanzia miaka 40yrs unaanza poteza ufanisi kwenye kusoma maandishi madogo mpk uwepo mwanga wa kutosha au urudishe nyuma kidg ) kisha akapata ajali na nlipo kuja kumuona akawa anaamini ajali ndo imemsababishia lile ttzo though jicho halikuathiriwa vyoyvyote na hiyo ajali il psychology ndo ilikuwa imekuwa distorted na ajali , ILA ALIBISHA MPK NAMRUHUSU AENDE

DALILI ZA MATATIZO HAZIMA , HUO NI MFANO TU

Sent from my HUAWEI NXT-L29 using JamiiForums mobile app
Hiki kifo kinahitaji uchunguzi huru. Hata hiyo hospital aliyotibiwa mpaka kufariki haiwezi kutoa majibu sahihi kwa sababu inaonekana walizembea kumpa matibabu haraka kwa sababu ya kudai fedha. Kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa kuwa mtoto alifariki kwa sababu ya kukosa huduma ya haraka, hivyo madaktari wanataka wasionekane kuwa walifanya uzembe.
 
Record kutoka hospital ya mtoto kua na cancer ipo au hiyo cancer imekuja one onekana baada ya kifo cha mtoto!? Upelelezi uanzia hapo, ukiwahusisha na team ya wataalamu wa afya hadi wale wa forensic!!
utajulikanaje una CANCER kama huna utaratibu ea kupima ?

walimu mnawapa presha sana , n inaonekana hamjui athari za mnayoyafanya

Sent from my HUAWEI NXT-L29 using JamiiForums mobile app
 
mbon kama umeamini maneno ya mama bia ushahidi ? na mm kesho nkijisema yangu tu juu ya walimu utaamini pia , walimu mnawapa presha sana , ndio maana wanatoa maboko sana siku hz sabab hawana waranty na kaz yao , mtoto kapigana anajich kesho anamsingizia mwl

Sent from my HUAWEI NXT-L29 using JamiiForums mobile app
Naamini kwa sababu shule za Tanzania waalim kuchapa/kupiga wanafunzi siyo jambo geni. Huu umekuwa kama utamaduni na waalim wanakuwa na visirani sana. Knachotakiwa kufanywa hapa ni postmortem ya uhakika. Ifanywe na dr wasiofungamana na hiyo hospital aliyotibiwa kwa sababu inaonekana kuwa walizembea kwa kuchelewa kumtibu ndiyo akafariki.
 
Poleni sana kwa msiba. Lakini kifo heshima ya yake ni mazishi. Imetokea zika. Kingine walimu ni vichaa sana walimu wengi shule za msingi za serikali ni walevi na wanavuta bangi na utoto. Ndio hao wakiwa wanakunywa chai wanaongea ujinga ujinga wa kuchapa watoto. Haki ya maiti ni maziko tu mengine ni usumbufu
 
Kama ripoti ya Daktari inaonesha mwanao alikuwa na Kansa ya Damu ( dalili zote unazoelezea zinaendana) kwanini unalazimisha ionekane Mwalimu ndio kamuua mwanao?

Kuchapwa viboko kungekuwa kunaua tungeshakufa wengi sana tuliosoma zamani. Mnataka kutengeneza kizazi gani cha watoto wasiochapwa?

Kwanini mnataka kuleta malezi ya Kizungu watoto wa Kitanzania wenye mazingira na tamaduni tofauti katika malezi na makuzi?

All in all may His Soul Rest in Eternal Peace. Amen. Kuendeleza hii kesi ni kumkosea Marehemu kwa kulazimisha kitu kisichokuwepo.
Mkuu vitoto vya siku hizi ni vidogo sana fimbo ya mgongo unaweza vunja mbavu
 
Naitwa Janeth Shayo, mkazi wa Uru, Moshi. Naomba unisaidie kupaza sauti mwanangu Jonathan Makanyaga (07) mwanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi Mrupanga, ameuawa kwa kupigwa na Mwalimu lakini kesi inataka kupindishwa.

Tar.28/02/2024 mwanangu alienda shuleni akiwa mzima. Alipofika aliadhibiwa kwa kuchelewa "namba". Alipoingia darasani alianza kutokwa damu puani na mdomoni. Akarudishwa nyumbani. Nilipomkagua nikamkuta na majeraha yaliyovilia damu mgongoni, kwenye mbavu na mguuni.

Kesho yake nikaenda nae shuleni kutaka kuoneshwa mwalimu aliyemfanyia ukatili mwanangu. Lakini Mwalimu mkuu akaomba nibaki nje. Akaingia na mwanangu ofisi ya walimu na kumtaka amtambue Mwalimu aliyemuadhibu. Mwanangu akamtanbua. Mwalimu Mkuu akaniambia wameshamfahamu ni mwalimu wa "Field" hivyo atazungumza nae.

Wakanipa 20,000/= za matibabu. Nikampeleka mwanangu zahanati. Kesho yake akazidi kutoka damu, na kulalamikia maumivu sehemu za mbavu. Nikampeleka hospitali ya masista. Daktari akaniambia bandama imejeruhika ndio sababu ya kutoka damu mdomoni. Mtoto alidai pamoja na viboko alivyochapwa, Mwalimu pia alimpiga ngumi tumboni. Huenda ndiyo iliyopasua bandama.

Hali yake ilizidi kuwa mbaya tukapewa rufaa kwenda KCMC. Akatakiwa kufanyiwa upasuaji. Gharama 350,000/= lakini sikuwa nayo. Nikapiga simu shuleni wakasema tuombe afanyiwe halafu watalipa baadae. Hata hivyo kabla hajafanyiwa hali yake ikazidi kuzorota, akashindwa kupumua, akawekwa kwenye Oxygen. Akashindwa kula, akawekewa mpira wa chakula. Baada ya siku chache akafariki 😭.

Lakini ripoti ya hospitali inasema mwanangu amekufa kwa kansa ya damu. Kansa gani ya damu inayomuua mtoto kwa wiki mbili? Na kwanini hiyo kansa itokee baada ya kuadhibiwa shuleni? Kwanini Mwalimu aliyemuadhibu mwanangu anafichwa, na sipewi haki ya kumfahamu?

Nalazimishwa nichukue maiti nikazike lakini nimekataa. Nataka uchunguzi huru. Nimeenda dawati la jinsia kulalamika nikapuuzwa. Nimepiga simu kwa Waziri Dkt. Gwajima D akanipa namba ya mtu wa kunisaidia. Nilipopiga kumbe ni yuleyule Mkuu wa dawati la jinsia aliyenipuuza. Nikamrudia Gwajima akasema niwasiliane nae huyohuyo. Nimekosa pa kulilia haki ya mwanangu Jonathan
Polee sana dada!!!! Mungu akufanyie wepesi.....
 
mna ushahidi sio mnabeba maneno ya mama aliyechanganywa na msiba anatafuta pa kutulizia akili zake

Sent from my HUAWEI NXT-L29 using JamiiForums mobile app
Tulisoma kwenye hayo mashule tunajua nini ni nini ...tunajua mtoto.mdogo anaweza kuchapwa kisa hana viatu je swala la viatu ni kosa la mtoto ? Mtoto kuchapwa kisa uniform zimechaka je ni kosa la mtoto ...walimu ni wapumbavu haswa
 
Record kutoka hospital ya mtoto kua na cancer ipo au hiyo cancer imekuja one onekana baada ya kifo cha mtoto!? Upelelezi uanzia hapo, ukiwahusisha na team ya wataalamu wa afya hadi wale wa forensic!!
Dalili za cancer zimejitokeza baada ya kipigo.
 
siipend ccmu ila ktk hili HESHIMU MAJIBU YA DAKTARI

Sent from my HUAWEI NXT-L29 using JamiiForums mobile app
Swali je ukimkuta mtu yupo maututi ukampiga ngumi akafa ina maana hauja ua ? Kwa sababu huyo mtu alikuwa mgonjwa ? Hiyo inaitwa kummalizia ....mfano mtoto ana ugonjwa wa pumu wewe ukampa mfuko wa simenti abebe kwa lazima akifa kwa kubanwa na pumu wewe unausika au hauhusiki
 
Hivi inaingia akilini mtoto wa miaka saba kupigwa eti amechelewa shule? Hivi kwa umri huo yeye ndiye anapaswa kujua saa ya kuamka, kujitarisha na kwenda shule? Huoni huyo mwalimu ni mshenzi wa mwisho? Kwa nini asiwasiliane na wazazi kuhusu kuchelewa? Mambo mengine ni kujitakia na siwezi kumuonea huruma.
Ukakasi ni mkubwa kwanza kwa psychology haiingi MWALIMU kumchapa mtoto wa chekechea drs la 1&2 tena Kwa kosa la kuchelewa namba mm ntakua mtu wa mwisho kuamini hili

Pili kumpiga ngumi achilia mbali fimbo ambayo kiuharisia haifai kutumika kwa hayo madarasa kwa sababu Ndio anaanza kupenda shule fimbo itamfanya achukie shule Ndio maana Kama ni mfuatiliaji wa makuzi ya mtoto madarasa haya sehemu kubwa ya masomo yao ni kucheza

Hii kesi inamkanganyiko mwingi zaidi ya unavyo fikia Ndio maana from beginning dawati ambalo linashughulikia hii kesi limetupilia mbali hii shauri kuna some sort of ukweli umekosekana kwenye maelezo
 
Shida ya MADAKTARI MAKANJANJA, unaona kabisa mtoto ameshambiliwa mwili mpaka amedhurika, lakini unaandika CANCER kwenye ripoti! 🤓

Is cancer the cause or a co-existing condition? (which is not a causation).

Mtu akiwa na malaria mwilini, kisha akakakatwa panga akafa, utasema amekufa kwa malaria?

Hizi shule zinazofundisha hawa MAKANJANJA zimesajiliwa kweli kihalali au zinafundishaje?

Hawa ndio wanaotushindilia MACHANJO YENYE MERCURY kutoka Marekani.

Nakuagiza Dkt. Gwajima D ulifuatilie hili swala haraka sana na uwawajibishe wahusika kwa mujibu wa sheria, la sivyo nitakuja hapo ofisini kwako kwa namna ambayo hautaielewa.

Cc Lamomy & DR Mambo Jambo
Wizo siku hizo unatoa maagizo kwa waziri umetisha 🤣🤣🤣🤣
 
kwahiyo ulitaka kansa isubir siku mbili tatu zipite ili isionekane ni mwl ? ndo hoja yako hii ?

Sent from my HUAWEI NXT-L29 using JamiiForums mobile app

kwahiyo ulitaka kansa isubir siku mbili tatu zipite ili isionekane ni mwl ? ndo hoja yako hii ?

Sent from my HUAWEI NXT-L29 using JamiiForums mobile app
Mtoto alikuwa mzima hadi alipopata adhabu,baada ya kupata adhabu ya kuchapwa/na kupigwa na kupoteza maisha ndo inasemekana ni cancer,hapa ndo nashindwa kuelewa
 
Back
Top Bottom