Mwananchi: Tusidanganyike, hili ndilo bunge tunalotaka!

Mwananchi: Tusidanganyike, hili ndilo bunge tunalotaka!

Kuna haja na sisi tuulizwe juu ya msimamo wetu tunapo-compare bune hili na lililopita au yaliyopita
Misisngi aliyoiweka Sitta ni mizuri japo wanataka kuibomoa
...Tatizo mkuu watu bado wana ule uoga wa kudhanii kuwa ukikosoa serikali ni dhambi. Lakini mimi nina imani hii hali itazoeleka na kule mjengoni usishangae siku moja ukakuta wabunge wanazichapa kavu kavu hiyo ndio ya kudumisha demokrasi mazeee sio bora liende tu unasaini posho akina Steven Wassira kila siku wanachapa usingizi tu kule ni aibu kabisa. Kwa kweli mi nina uhakika ingekuwa Spika wa bunge hili angeendelea kuwa Samuel Sitta mle mambo yangenoga zaidi hata kama angeona mbunge/waziri amekunjwa suti kwa kuwa mbunge ametoa majibu ya kitoto akinyamaza tu sio huyu mama anayeendeshwa kwa remote kwa masilahi ya mafisadi.
 
Hili ndilo bunge tunalolitaka! Wabunge wasipangiwe aina ya maswali ya kumuuliza waziri mkuu! Waulize maswali ya papo kwa papo hata kama si ya kisera!
 
kwani uongo? juzi kuna gazeti moja limemnukuu mmoja wa viongozi wastaafu akisema kuwa wabunge wanajua sheria moja tu ya namba 68 ya kuomba mwongozo wa spika...haaaaaaahaaa kweli bana nimesikiliza bunge japo kwa kujilizimisha kama nameza quinine vile nikakuta yaani kila saa sheria namba 68 naomba mwongozo wa spika.....................leo Mwanahalisi amendika pia kuhusu bunge kuwa la mashemeji na wakwe....sasa kweli hapo tuna bunge au genge la majambazi???
Unapoombwa mwongozo ni pale ukweli unapotoshwa na au jamaa wanamwaga uozo wao. Au neno mwongozo wewe unalitafsiri vip?
 
Naturaly watu wana akili ya utambuzi, tukiwa nje tunaona na kutambua!ya makinda, ndugai na mwagama pamoja na foilikonjombe tunayaona tunayapima , tunayatafakari na kupata majibu yake,

ya zito, mnyika, kafulila, wenje, lissu. Lema, mbowe, regina,sugu, mdee ect, nayo tunayaona na kuyapima mwisho tunasema! Soon liberation will be on place!
 
wala ulidhani mie nina ugomvi nalo....hata kidogo,mi nilishadhulumiwa hadi maisha yangu Mpwa, nangoja siku na mimi nilipize kisasi.
Unapoombwa mwongozo ni pale ukweli unapotoshwa na au jamaa wanamwaga uozo wao. Au neno mwongozo wewe unalitafsiri vip?
 
Wabunge wetu wapiganaji kwa hii mada naomba mtuelewe mtizamo wetu sie wananchi,kwa vile wahuni wanaona umuhimu wa kuwahoji wahuni wenzao na kutuacha sie wananchi pembeni basi maoni yetu tutapitisha hapa jf na tunaomba myasome na muelewe huo ndo msimamo wa wananchi ya kwamba songeni mbele bunge linavuta hisia na linatusaidia sana katika kuisimamia serikali vyema,huo ndo upinzani halisi na hiyo ndo kazi ya vyama vingi,tunataka 2015 moto uwe mkali zaidi na hilo tutalifanya kwani kura zenu tutawapa na tutakuwa tayari kuzilinda mpaka kieleweke
 
Kwanza kabisa nichukue fursa hii kumshukuru sana mama shelukindo kwa kutufungua macho juu ya yale yaliyofanyika wizara ya nishati na madini chini ya mwanna william, sina uhakika saana naka muheshimiwa mukulu na mkuu wa wizara hii hawajui kilichokuwa kinaendelea juu ya hili na kwa rtaalifa ni kwamba hako kamchezo kamefanyika kwa takribani miaka 4 na jairo kashiriki mara 2. najiuliza sana je watanzania ipo siku watakuwa wazalendo wa nchi yao kama haya mambo yanatokea na bado mkulu jhasemi chochote hata ka suala lipo chibni ya uchunguzi?????ha ha ha ah! tanzania, ni mambo mengi yamefukiwa tukidanganywa na uchunguzi mara tume mara michakato na tuvute subira lakini mwisho hakuna kinachoendelea! sio kwamba watanzania hawajui, no! tunajua sana! rai yangu kwa watawala!amani tunaichezea na itatughalimu ka hatutakuwa makini na kutibu madudu yanayoonekana bayana na yasiyoonekana!

TUNAOMBA HAKI ITENDEKE JUU YA SUALA LA RUSHWA NISHATI NA MADINI!
 
mimi kama kijana bunge hili limenivutia sana, wachana na mazee ka p. msekwa, na yale yaliyogopa kasi yakapumzika mali ya umma ingeendelea kupotea, wanaobeza upinzani bora tu wafe wote maana wamekunywa maji yabendela sana sana mengi yamezaliwa 1967 lakin kuanzia 1975 madudu haya hawayataki kabisa, upinzna ani umeokoa hela nyingi hata serikali inashangaa na kushutuka, ndio maana hata Pinda anawakubali
 
Duu umenikumbusha mbali kidogo hii redio nilikuwa naisikiliza kipindi cha nyuma kidogo baadaye nikaachana nayo kabisa, Ngoja siku moja nita-tune nimsikie kidogo Gadner habash na Masudi kipanya

Duh!kweli mkuu hujasikiliza hii redio kwa siku nyingi,hao jamaa kwenye red ishabaki historia kwenye radio hiyo.
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]Tusidanganyike, hili ndilo Bunge tunalolitaka[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Imekuwa fasheni siku hizi kwa watu mbalimbali kuwabeza wabunge wa Bunge hili la Kumi linaloendelea na mkutano wake wa nne, mjini Dodoma. Fasheni hiyo ilianza taratibu wiki kadhaa zilizopita wakati Spika, Anne Makinda aliposema kwamba heshima ya Bunge ilikuwa imeanza kupotea kutokana na mijadala mikali aliyosema ilikuwa inaligeuza Bunge kuwa kama Kariakoo.

Baada ya kauli hiyo ya Spika, watu kadhaa, wakiwamo baadhi ya wabunge wa chama tawala na viongozi wengine ambao ni wafuasi wa chama hicho walitoa kauli mbalimbali na kunukuliwa na vyombo vya habari wakirudia kauli ya Spika kwamba mijadala na minyukano mikali ya hoja inayoendelea bungeni imepoteza hadhi ya Bunge na kuharibu taswira ya chombo hicho cha kutunga sheria.

Lakini kwa upande mwingine, wabunge na wafuasi wa vyama vya upinzani walipinga msimamo wa Spika na baadhi ya wafuasi wa chama chake na kusema kwamba, hali hiyo ni kielelezo kizuri cha kushamiri kwa demokrasia ya vyama vingi katika nchi yetu na kuimarika kwa uhuru wa wabunge kutoa mawazo yao pasipo kufungwa midomo kinyume na ilivyokuwa wakati wa Bunge la chama kimoja.

Hata hivyo, pamoja na ufafanuzi huo, kejeli zimeendelea kuelekezwa kwa wabunge wa Kambi ya Upinzani, hasa wa Chadema na NCCR na baadhi ya wabunge wa chama tawala ambao wakati mwingine wamekuwa wakiikosoa Serikali bungeni, kwamba wabunge hao wanafanya mambo ya kitoto ambayo hawakutumwa na wananchi.

Sisi tunadhani kwamba madai ya kupungua kwa nidhamu ya wabunge na hadhi ya Bunge siyo ya kweli. Tunadhani madai hayo yanatolewa na watu wanaoshindwa kuimudu kasi ya Bunge la Kumi ambalo lina wabunge wengi vijana na wasomi ambao wanahoji mambo ya msingi ambayo huko nyuma yalikuwa yanafichwa chini ya zulia kwa lengo la kutetea serikali iliyo madarakani badala ya kuisimamia na kuiwajibisha pale ilipokosea.

Inawezekana kwamba upo udhaifu wa hapa na pale kwa baadhi ya wabunge kuvunja kanuni hii au ile kwa makusudi au vinginevyo. Tunachopinga hapa ni madai ya jumlajumla yanayoelekezwa kwa wabunge, hasa wa Kambi ya Upinzani kwamba wanapotoa hoja au kuuliza maswali magumu yanayoibana Serikali wanalidhalilisha Bunge. Mfano ni pale wabunge wanapokatazwa kumuuliza Waziri Mkuu maswali ya hapo kwa hapo ambayo siyo ya kisera, eti kwa sababu maswali hayo yanahitaji muda mrefu wa kufanyiwa utafiti.

Kwa hiyo, lazima tukiri kwamba wengi wa wabunge wa Kambi ya Upinzani katika Bunge hili la Kumi ni wabunge makini, ingawa Bunge la Tisa lililokuwa chini ya Spika Samwel Sitta ndilo lilikuwa anzilishi la mijadala mikali kutokana na kiongozi huyo kusimamia vyema kanuni za Bunge na kutoa haki sawa kwa wabunge wote bila upendeleo . Yaliyompata Spika Sitta sasa ni historia, lakini ni vyema tu tukasema kwamba kiongozi huyo alirudisha imani ya wananchi kwa Bunge.

Tunachokiona katika Bunge la Kumi ni juhudi za makusudi au vinginevyo za uongozi wa Bunge kupunguza kasi ya uhuru wa wabunge wa kuhoji na kuiwajibisha Serikali. Kambi ya Upinzani katika Bunge hili imeimarika maradufu na wabunge wake vijana wameonekana kujizatiti kwa kusoma na kuzielewa Kanuni za Bunge na kutoa hoja za msingi ambazo mara nyingi zinapingwa na kuzimwa na wabunge wa upande wa pili kwa kutumia wingi wao bungeni.

Hali hiyo imeleta hofu kwa sababu wananchi sasa wanaiona mijadala hiyo katika luninga na wanafuatilia na kuguswa sana na mijadala hiyo yenye msisimko mkubwa. Hili ni Bunge la hoja, siyo la staha au la kuendeleza dhana ya kulindana. Ni Bunge lenye vijana wenye uwezo wa kuchambua miswada inayoletwa bungeni. Ni kwa sababu hiyo wananchi wamefurahia hali hiyo ambapo Bunge siyo tena mhuri wa kupitisha mambo ya Serikali pasipo kuhoji. Ndiyo maana tunasema hili ndilo Bunge ambalo wananchi wanalitaka.

Mwananchi
 
Uchambuzi katika makala hii ambao umefanywa na mwandishi katika gazeti la Mwananchi nimeridhika nao. Tanzania tu wageni mno na mfumo wa vyama vingi, na wengi wa wabunge wa chama kinachoongoza serikali cha CCM wanachofikiria upinzani ni kupinga tu hata kwenye hoja zenye manufaa kwa taifa. Ni dhahiri kila chama kina sera zake lakini si kila sera inatekelezeka au kukubalika na umma. Kwa wabunge wetu wawe makini katika jambo hili isijetokea wanakuja kutemwa na wananchi katika uchaguzi ujao kwa kutetea uozo uliopo serikalini.
 
Back
Top Bottom