Mwananchi: Tusidanganyike, hili ndilo bunge tunalotaka! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwananchi: Tusidanganyike, hili ndilo bunge tunalotaka!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ecolizer baba, Aug 3, 2011.

 1. e

  ecolizer baba Member

  #1
  Aug 3, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 77
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 40
  Imekuwa fasheni siku hizi kwa watu mbalimbali kuwabeza wabunge wa Bunge hili la Kumi linaloendelea na mkutano wake wa nne, mjini Dodoma. Fasheni hiyo ilianza taratibu wiki kadhaa zilizopita wakati Spika, Anne Makinda aliposema kwamba heshima ya Bunge ilikuwa imeanza kupotea kutokana na mijadala mikali aliyosema ilikuwa inaligeuza Bunge kuwa kama Kariakoo.

  Baada ya kauli hiyo ya Spika, watu kadhaa, wakiwamo baadhi ya wabunge wa chama tawala na viongozi wengine ambao ni wafuasi wa chama hicho walitoa kauli mbalimbali na kunukuliwa na vyombo vya habari wakirudia kauli ya Spika kwamba mijadala na minyukano mikali ya hoja inayoendelea bungeni imepoteza hadhi ya Bunge na kuharibu taswira ya chombo hicho cha kutunga sheria.

  Lakini kwa upande mwingine, wabunge na wafuasi wa vyama vya upinzani walipinga msimamo wa Spika na baadhi ya wafuasi wa chama chake na kusema kwamba, hali hiyo ni kielelezo kizuri cha kushamiri kwa demokrasia ya vyama vingi katika nchi yetu na kuimarika kwa uhuru wa wabunge kutoa mawazo yao pasipo kufungwa midomo kinyume na ilivyokuwa wakati wa Bunge la chama kimoja.

  Hata hivyo, pamoja na ufafanuzi huo, kejeli zimeendelea kuelekezwa kwa wabunge wa Kambi ya Upinzani, hasa wa Chadema na NCCR na baadhi ya wabunge wa chama tawala ambao wakati mwingine wamekuwa wakiikosoa Serikali bungeni, kwamba wabunge hao wanafanya mambo ya kitoto ambayo hawakutumwa na wananchi.

  Sisi tunadhani kwamba madai ya kupungua kwa nidhamu ya wabunge na hadhi ya Bunge siyo ya kweli. Tunadhani madai hayo yanatolewa na watu wanaoshindwa kuimudu kasi ya Bunge la Kumi ambalo lina wabunge wengi vijana na wasomi ambao wanahoji mambo ya msingi ambayo huko nyuma yalikuwa yanafichwa chini ya zulia kwa lengo la kutetea serikali iliyo madarakani badala ya kuisimamia na kuiwajibisha pale ilipokosea.

  Inawezekana kwamba upo udhaifu wa hapa na pale kwa baadhi ya wabunge kuvunja kanuni hii au ile kwa makusudi au vinginevyo. Tunachopinga hapa ni madai ya jumlajumla yanayoelekezwa kwa wabunge, hasa wa Kambi ya Upinzani kwamba wanapotoa hoja au kuuliza maswali magumu yanayoibana Serikali wanalidhalilisha Bunge. Mfano ni pale wabunge wanapokatazwa kumuuliza Waziri Mkuu maswali ya hapo kwa hapo ambayo siyo ya kisera, eti kwa sababu maswali hayo yanahitaji muda mrefu wa kufanyiwa utafiti.

  Kwa hiyo, lazima tukiri kwamba wengi wa wabunge wa Kambi ya Upinzani katika Bunge hili la Kumi ni wabunge makini, ingawa Bunge la Tisa lililokuwa chini ya Spika Samwel Sitta ndilo lilikuwa anzilishi la mijadala mikali kutokana na kiongozi huyo kusimamia vyema kanuni za Bunge na kutoa haki sawa kwa wabunge wote bila upendeleo . Yaliyompata Spika Sitta sasa ni historia, lakini ni vyema tu tukasema kwamba kiongozi huyo alirudisha imani ya wananchi kwa Bunge.

  Tunachokiona katika Bunge la Kumi ni juhudi za makusudi au vinginevyo za uongozi wa Bunge kupunguza kasi ya uhuru wa wabunge wa kuhoji na kuiwajibisha Serikali. Kambi ya Upinzani katika Bunge hili imeimarika maradufu na wabunge wake vijana wameonekana kujizatiti kwa kusoma na kuzielewa Kanuni za Bunge na kutoa hoja za msingi ambazo mara nyingi zinapingwa na kuzimwa na wabunge wa upande wa pili kwa kutumia wingi wao bungeni.

  Hali hiyo imeleta hofu kwa sababu wananchi sasa wanaiona mijadala hiyo katika luninga na wanafuatilia na kuguswa sana na mijadala hiyo yenye msisimko mkubwa. Hili ni Bunge la hoja, siyo la staha au la kuendeleza dhana ya kulindana. Ni Bunge lenye vijana wenye uwezo wa kuchambua miswada inayoletwa bungeni. Ni kwa sababu hiyo wananchi wamefurahia hali hiyo ambapo Bunge siyo tena mhuri wa kupitisha mambo ya Serikali pasipo kuhoji. Ndiyo maana tunasema hili ndilo Bunge ambalo wananchi wanalitaka.
   
 2. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,135
  Trophy Points: 280
  kwani uongo? juzi kuna gazeti moja limemnukuu mmoja wa viongozi wastaafu akisema kuwa wabunge wanajua sheria moja tu ya namba 68 ya kuomba mwongozo wa spika...haaaaaaahaaa kweli bana nimesikiliza bunge japo kwa kujilizimisha kama nameza quinine vile nikakuta yaani kila saa sheria namba 68 naomba mwongozo wa spika.....................leo Mwanahalisi amendika pia kuhusu bunge kuwa la mashemeji na wakwe....sasa kweli hapo tuna bunge au genge la majambazi???
   
 3. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #3
  Aug 3, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Mhe Willima Lukuvi anayehusika na msuala ya kibunge kwa upande wa serikali ndiye aliyewafunza wabunge wa CCM mambo ya kihuni kama vile kuomba miongozo na kuzomea ili kuwazuia wabunge wa upinzani kumudu kujenga hoja ipasavyo. Hivyo wabunge wa upinzani walipogundua mbinu hizo nao wakaiga na kuwafanya wabunge wa CCM na mawaziri nao kushindwa kujenga hoja zao ipasavyo. Ndio faida ya kuwa wa wabunge vijana wanajifunza mbinu za wapinzani haraka. Mwishowe njam za CCM zimeshindwa imebidi watafute hifadhi katika kanuni za bunge. Swali kwanini Mhe W Lukuvi alimaua kuwafunza wabunge wa CCM kuvunja kanuni? Na kwanini Spika na Naibu na wenyeviti waliachia jambo hilo? Jibu ni moja kuwa kuipendelea CCM
   
 4. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #4
  Aug 3, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wananchi walio wengi wanajua kuwa Bunge hili liko makini sana. Wale wanaolibeza ni wale wachache wasiojua kazi ya Mbunge, wajibu na majukumu yake. Pia, ni wale wanaotoka kwenye familia za MAFISADI. Otherwise, wengine tuko vizuri tunasubiri uchaguzi tu, CCM iangushwe kama mti wa mgomba au majani ya kiangazi.
   
 5. HAZOLE

  HAZOLE JF-Expert Member

  #5
  Aug 3, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,332
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  clouds fm ndo wanabeza sana kupitia kipindi chao cha power breakfast......... bunge kama kariakoo mtaa wa kongo duh. DEMOKRASIA OYEEE
   
 6. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #6
  Aug 3, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Hili bunge kwangu mimi naona bado sana, Ninalolitaka mimi ni Bunge la 50% kwa 50% kwa sasa magamba bado wanatawala, ndo maana ujinga unakuwa mwingi sana! NATAMANI SERIKALI YA MAGAMBA IDONDOKE HATA SASA! NIMECHOKA NA USANIII WA MAGAMBAAA'S
   
 7. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #7
  Aug 3, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Daa hawa jamaa wamewashika kweli kwani redio zingine hazipo?
   
 8. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #8
  Aug 3, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Mabunge yaliyipita kimsingi ndio yaliyowakosea wananchi heshima.
  Yalishindwa kuihoji na kuiwajibisha serikali pale ilipohitajika.
  Wabunge waliligeuza bunge kijiwe cha wastaafu na mahala pa kuchapia usingizi.
  HATA HIVYO;
  Wabunge waliozoea ujinga wa zamani wanaona WAMEINGILIWA.
  Wanaona WAMEVAMIWA na wapinzani ambao sasa wanalifanyisha bunge kazi yake ya msingi.
  Wabunge wa upinzani ni faraja sana kwa wananchi(WASIO WANAFKI) na ni mwiba kwa serikali dhalimu na watu wake.
   
 9. olele

  olele JF-Expert Member

  #9
  Aug 3, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 814
  Likes Received: 339
  Trophy Points: 80
  at least tunaweza kusema bunge ndo limeanza kuwa la kidemokrasia, watu (hasa viongozi wa serikali) walishazoea "bunge poa" yaani wazr anaenda na bajeti ya hovyo inapitishwa kwa asilimia mia, mi nadhani bunge linapitia kipindi cha mageuzi makubwa na wananchi ndo wanalitaka, watu wavumilie tu wenzetu walishapitia huku tena sisi tumechelewa. Hili ndo bunge tunalolita.
   
 10. u

  utantambua JF-Expert Member

  #10
  Aug 3, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Muanzisha thread upo sahihi. Hilo ndio bunge tunalotaka. Sio bunge lisilo na misigano ya hoja, unadhani kwa jinsi bunge hili lilivyo kuna waziri anayeweza kupresent mambo bila kujiandaa? Wakifanya hivyo ndo pale unapoona cdm wanafanya kazi yao hadi kusingiziwa ati wanashusha hadhi ya bunge. Kiukweli ningependa kuona speed inakolea zaidi na zaidi ya hapa
   
 11. MANI

  MANI Platinum Member

  #11
  Aug 3, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,410
  Likes Received: 1,863
  Trophy Points: 280
  Uko sahihi mkuu bila ya hivyo hivi vituko havitaisha!
   
 12. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #12
  Aug 3, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Kusema w/mkuu muongo wakati kweli kadanganya ni kutokuwa na nidhamu?waziri kudanganya pia aachwe?speake na naibu wake kuibana kambi ya upinzani pia lisisemwe?kwa nini ccm watudanganye nac tukubali?kijana gani wasasa asiyelipenda bunge?bunge zuri sana haya yanayotokea mi changamoto kwa speaker na mawaziri watupe tunacho hitaji.
   
 13. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #13
  Aug 3, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Wana JF,

  Me nashangaaa ni vyombo vya habari vimekalia kushadadia na kuwapa nafasi viongozi wa juu kutoa maoni yao mbona hawajaenda mitaani na kuwauliza wananchi wa lika tofauti wasikie kama kweli Bunge limekosa adabu kweli, Nadhani mbinu hapa ya serikali inatumia kujikosha maana wameishaona mwelekeo sio wananchi wamestukia sasa wanatafuta jinsi ya kuwapotosha wananchi na wananchi wako makini siku hizi hawadanganyiki kabisa.

  Wabunge mko mjengoni sio kuitetea serikali bali ni kuipa majukumu na kuiuliza utekelezaji ulivyo fanyika kama ni kweli wataipa hongera na kama serikali imechemka itaambiwa hapo performance ni zero sasa sielewi kwanini wabunge wengiune wana taka kujifanya wao ni part ya serikali. nyie wabunge endeleeni 2015 ndio mtihani mtaukuta pale jimboni kwenu kurudi shida itakuwa
   
 14. Erick G. Mkinga

  Erick G. Mkinga Member

  #14
  Aug 3, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naomba Mwongozo.
   
 15. mbogo31

  mbogo31 JF-Expert Member

  #15
  Aug 3, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 687
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Mimi naona Bunge halijafikia tunapopataka ila angalau sasa linaanza kuwa Bunge, kuna mmoja amesema anataka bunge la 50% by 50%, ni kweli kabisa na hapo ndipo nchi itasonga mbele kimaendeleo na sio huu usani unaoendelea nchini.

  Shukrani kwa wabunge machachari hasa Lema, Wenje na Kafulila na angalau Kilango.
   
 16. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #16
  Aug 3, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Watu wameathirika na ule utendani wa kikondoo wa mabunge yaliyopita, na hii propaganda inaletwa na CCM kwamba watu wanaona bunge la sasa halina tija, lkn sie wananchi tena wa KAWAIDA km wanavyotuita tunalipenda sana bunge la sasa hasa wabunge wa upinzani
   
 17. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #17
  Aug 3, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Duu umenikumbusha mbali kidogo hii redio nilikuwa naisikiliza kipindi cha nyuma kidogo baadaye nikaachana nayo kabisa, Ngoja siku moja nita-tune nimsikie kidogo Gadner habash na Masudi kipanya
   
 18. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #18
  Aug 3, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kuna haja na sisi tuulizwe juu ya msimamo wetu tunapo-compare bune hili na lililopita au yaliyopita
  Misisngi aliyoiweka Sitta ni mizuri japo wanataka kuibomoa
   
 19. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #19
  Aug 3, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  Hakika bunge hili liko makini sana.
   
 20. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #20
  Aug 3, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  .....Ukichunguza sana utagundua wale akina Gerald Hando na Babra Hassan wa Couds fm na Michael Baruti na Zembwela kule EAT fm wote uelewa wao wa mambo ni mdogo sana na ndio maana hurusha hewani vile vipande vya mivutano ya wabunge na kisha kuanza kuponda. lakini wanasahau kuwa hizi zama za kulala na kuburuzana watu wako makini na issues za maana zenye maslahi kwa taifa. Mi kwa upande wangu nawapongeza sana wabunge wote wanaotoa hoja za moto na kali kabisa kwa serikali hii chovu bila kujali kama ni upinzani au wale wa sisiem. Huwezi kuamini ingekuwa zile enzi za giza ukute eti mbunge wa chama tawala aibue kashfa nzito kama ile ya akina David Jairo...................I really like this...
   
Loading...