Mwananchi Njombe: Tangu nizaliwe sijawahi kunywa maji ya Bomba

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Wananchi wa Kijiji cha Luponde wamemshukuru Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini, Deodatus Mwanyika, kwa kuchukua hatua za kufanikisha upatikanaji wa maji safi katika Kijiji hicho kwa kuwapatia tenki la Maji lenye Ujazo wa Lita 10,000, huku mmoja wa Wananchi, Castory Mlelwa akisema "tangia nizaliwe, sijawahi kunywa maji ya bomba"

Mbunge Mwanyika amewakabidhi wakazi hao tanki lenye ujazo wa Lita Elfu Kumi, huku akithibitisha kupokea ombi lao la kupata mipira ya kusambazia maji ili maji yafikie Mitaani.

Mbunge amesema, “Wananchi wamejitoa na kuchangia kiasi cha Shilingi Milioni 10 kwa ajili ya mradi wa maji. Nimepokea ombi lao la kupata mipira na nitahakikisha linafanikiwa.”

Mwenyekiti wa Kijiji hicho, ndugu Legnibeti Kilumile, ameeleza kuwa Wananchi wameonyesha jitihada za kushirikiana kwa kutoa maji kutoka mtoni na kuyafikisha Kijijini, lakini kutokana na changamoto za bajeti, haikuwezekana kuendelea na usambazaji wa maji katika Mitaa yote.

Aidha, Wakazi wa Kijiji cha Luponde wameendelea kuiomba Serikali na wadau wa maendeleo kuhakikisha mipira ya kusambazia maji inapatikana, ili kuondoa kero ya kufuata maji yasiyo salama mtoni.
 
Ila Africa maisha yetu Mungu anajua. Wengine hawajawahi kunywa maji ya bomba by choice.
 
Nchi ya kusadikika
 
Back
Top Bottom