Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,310
- 4,538
MWANASIASA NA MWANANCHI
MWANASIASA
1) Ndugu zangu wananchi,mimi wenu kiongozi,
Liyepigania nchi,na kuleta ukombozi,
Mimi aula siwafichi,nipitishe uchaguzi,
Sio bora uongozi,uwe bora uongozi.
MWANANCHI.
2)Napenda uweke wazi,zote ulotuahidi.
Yaliyo bora makazi,ni moja yako miadi
Pamoja tule andazi,la nchi kuifaidi.
Mwananchi nakilio,kukisema natamani.
MWANASIASA.
3) Epukana lalamizi,nilotenda ni bayana,
Mtu aliye maozi,haambiwa bwana ona,
Barabara ni wazi,yapitika kwa matwana,
So bora uongozi,uongozi uwe bora
MWANANCHI.
4)Barabara zote mbovu,zipi ulozitengeza.
Maisha watia kovu,aibu kuieleza.
Ahadi zote uovu,najua utanibeza.
Mwananchi na kilio,kusema nakitamani.
MWANASIASA
Shida yenu binadamu,hamuwezi kutosheka,
Ninasema maadamu,ninapaswa kutukuka,
Mliponipa jukumu,nikafanya lowezeka,
Si bora uongozi,uongozi uwe bora
MWANANCHI
5)Hospitali zi wapi,mbona mimi silalami
Nacho lalama ni kipi,wakti waua uchumi.
Umetufanya makapi,nakufunga zetu ndimi.
Mwananchi na kilio,kusema nakitamani.
MWANANCHI
6)Mbona tele zahanati,losheheni kila dawa,
Usizue hatihati,u mithili ya ngalawa,
Uongozi kwangu uti,sikwambii ni kipawa,
So bora uongozi,uongozi uwe bora.
MWANANCHI.
7)Hivi pesa ulitaka,ama nchi kuongoza.
Mbona unatajirika,kwako pazidi pendeza.
Wananchi twajizika,nchi ushaimaliza.
Mwananchi na kilio,kusema nakitamani.
MWANASIASA
8)Uonapo gari zetu,hayatiliwi asali,
Hicho sicho kiatu,inatiliwa petroli,
Kweli wewe ni kurutu,alopatwa kwa ajali,
si bora uongozi,uongozi uwe bora.
MWANANCHI.
9)Hapa sina kiongozi,kura nilishapoteza.
Kukupa we mlanguzi,jambo hilo laniliza.
Umekuwa mchuuzi,taifa kulichuuza ?
Mwananchi na kilio,kusema nakitamani
MWANASIASA
10)Bila mimi wewe nani,uso haya wala baya,
Nastahiki kwenye fani,utafanya yangu niya,
Tasalia u mneni,huku tumbo kiumiya,
So bora uongozi,uongozi uwe bora
MWANANCHI.
11)Siku ukiomba kura,mikono ikiwa nyuma.
Leo wahifanya swira,sumu wataka kutema.
Tumeshajua taswira,kiongozi we mnyama.
Mwananchi na kilio,kusema nakitamani.
MWANASIASA.
12)Uchaguzi kiwadia,tumbo zenu zawa mbele,
Chakula nitakitia,mnimine belele,
Kiti nitairukia,niwaache kwa kelele,
Si bora uongozi,uongozi ulo bora.
Shair:MWANANCHI NA MWANASIASA.
Mtunzi:limeandikwa kwa ushirikiano wa Bryan mackungh Rop wa Nakuru Kenya,na Idd Ninga wa Arusha Tanzania.
Bryan Mackungah anapatikana kwa +25472485351 au email ya: braynrop8@gmail.com
Idd ninga anapatikana kwa namba 0765382386,au email ya: iddyallyninga@gmail.com
MWANASIASA
1) Ndugu zangu wananchi,mimi wenu kiongozi,
Liyepigania nchi,na kuleta ukombozi,
Mimi aula siwafichi,nipitishe uchaguzi,
Sio bora uongozi,uwe bora uongozi.
MWANANCHI.
2)Napenda uweke wazi,zote ulotuahidi.
Yaliyo bora makazi,ni moja yako miadi
Pamoja tule andazi,la nchi kuifaidi.
Mwananchi nakilio,kukisema natamani.
MWANASIASA.
3) Epukana lalamizi,nilotenda ni bayana,
Mtu aliye maozi,haambiwa bwana ona,
Barabara ni wazi,yapitika kwa matwana,
So bora uongozi,uongozi uwe bora
MWANANCHI.
4)Barabara zote mbovu,zipi ulozitengeza.
Maisha watia kovu,aibu kuieleza.
Ahadi zote uovu,najua utanibeza.
Mwananchi na kilio,kusema nakitamani.
MWANASIASA
Shida yenu binadamu,hamuwezi kutosheka,
Ninasema maadamu,ninapaswa kutukuka,
Mliponipa jukumu,nikafanya lowezeka,
Si bora uongozi,uongozi uwe bora
MWANANCHI
5)Hospitali zi wapi,mbona mimi silalami
Nacho lalama ni kipi,wakti waua uchumi.
Umetufanya makapi,nakufunga zetu ndimi.
Mwananchi na kilio,kusema nakitamani.
MWANANCHI
6)Mbona tele zahanati,losheheni kila dawa,
Usizue hatihati,u mithili ya ngalawa,
Uongozi kwangu uti,sikwambii ni kipawa,
So bora uongozi,uongozi uwe bora.
MWANANCHI.
7)Hivi pesa ulitaka,ama nchi kuongoza.
Mbona unatajirika,kwako pazidi pendeza.
Wananchi twajizika,nchi ushaimaliza.
Mwananchi na kilio,kusema nakitamani.
MWANASIASA
8)Uonapo gari zetu,hayatiliwi asali,
Hicho sicho kiatu,inatiliwa petroli,
Kweli wewe ni kurutu,alopatwa kwa ajali,
si bora uongozi,uongozi uwe bora.
MWANANCHI.
9)Hapa sina kiongozi,kura nilishapoteza.
Kukupa we mlanguzi,jambo hilo laniliza.
Umekuwa mchuuzi,taifa kulichuuza ?
Mwananchi na kilio,kusema nakitamani
MWANASIASA
10)Bila mimi wewe nani,uso haya wala baya,
Nastahiki kwenye fani,utafanya yangu niya,
Tasalia u mneni,huku tumbo kiumiya,
So bora uongozi,uongozi uwe bora
MWANANCHI.
11)Siku ukiomba kura,mikono ikiwa nyuma.
Leo wahifanya swira,sumu wataka kutema.
Tumeshajua taswira,kiongozi we mnyama.
Mwananchi na kilio,kusema nakitamani.
MWANASIASA.
12)Uchaguzi kiwadia,tumbo zenu zawa mbele,
Chakula nitakitia,mnimine belele,
Kiti nitairukia,niwaache kwa kelele,
Si bora uongozi,uongozi ulo bora.
Shair:MWANANCHI NA MWANASIASA.
Mtunzi:limeandikwa kwa ushirikiano wa Bryan mackungh Rop wa Nakuru Kenya,na Idd Ninga wa Arusha Tanzania.
Bryan Mackungah anapatikana kwa +25472485351 au email ya: braynrop8@gmail.com
Idd ninga anapatikana kwa namba 0765382386,au email ya: iddyallyninga@gmail.com