DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Madereva bodaboda wanaofanya shughuli zao katika eneo la Ujiji, Kigoma, wamelalamikia changamoto ya mikataba inayowakabili, ikiwemo kulazimika kurejesha Sh10,000 kila siku kwa muda wa miezi 18, hali inayokuwa ngumu zaidi wanapopata ajali na kushindwa kuendelea na kazi.
Wakizungumza na mgombea ubunge jimbo la Kigoma Mjini kupitia ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, walimwomba awawezeshe kupata pikipiki zenye mikopo nafuu ili kuinuka kiuchumi.
Akijibu hoja hizo, Zitto ameahidi kushughulikia changamoto hizo pindi atakapochaguliwa, akibainisha kuwa sekta ya bodaboda ni miongoni mwa zinazogusa maisha ya vijana wengi na inahitaji mikakati ya kweli ya kuondoa kero za kimaisha.