Mwanana iko sokoni.


Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Messages
42,404
Likes
38,581
Points
280
Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined Feb 4, 2009
42,404 38,581 280
KAMPUNI ya vinywaji baridi vya Pepsi na Mirinda, ya SBC imewataka watumiaji wa vinywaji hivyo kuendelea kuburudika navyo huku ikiendelea kubuni vinywaji vipya baada ya jana kuzindua kinywaji cha Mwanana.

Aidha, kampuni hiyo imewataka wanunuzi wa jumla wa bidhaa hiyo kuuza vinywaji hivyo kwa bei inayotolewa kiwandani na si kuuza bei ya juu zaidi kwani wenye kipato cha chini watashindwa kunufaika na bidhaa hiyo.

Meneja Mauzo wa SBC, Rashid Chenja aliyasema hayo mwishoni mwa wiki Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kinywaji kipya cha Mwanana chenye ujazo wa mililita 300.

Chenja alisema kinywaji hicho kitaanza kupatikana katika sehemu zote vinavyopatikana vinywaji vya Mirinda na Pepsi kwa bei ya Sh 350 tu ili kukidhi haja ya wanywaji. Kinywaji cha Mwanana kitaanza kupatikana katika Mkoa wa Dar es Salaam pekee na baadaye kinywaji hicho kitaanza kusambazwa mikoani kwa kuanzia mikoa ya jirani.

Hata hivyo, wateja wa jumla watapata ofa ya kreti kwa kununua kinywaji hicho kwa Sh 8,000.
 

Forum statistics

Threads 1,237,166
Members 475,465
Posts 29,280,118