Mwanamtandao Rostam Aziz kufanya mahojiano maalum leo Septemba 2, 2025 kupitia UTV

Mwanamtandao Rostam Aziz kufanya mahojiano maalum leo Septemba 2, 2025 kupitia UTV

Anaenda kuharibu, anaenda kumpa Pole Pole afunguke zaidi maana atatoa code ambazo Pole atapita nazo,

Anaenda kufanya watu wazidi kutaka kusikia Pole Pole ata counterattack vipi na kuzidi kutoa ya ndani zaidi

Angekaa kimya ilikuwa busara zaidi

Kwa jinsi Pole Pole alivyokandia mitungi ya TAIFA GAS ,nilijua tu huyu tapeli lazima ajitokeze
Na hicho Tu Polepole alikuwa anataka....zile siri za kiapo zitamwagwa nje mchana kweupe kwa kisingizio cha kumjibu Rostam..

Rostam shtuka umetegwa, eti CIA agent, agent gani huwezi kuthibiti hasira na mihemko?
 
Ninaandika kitabu cha ujasiriamali ndipo nilipogundua kwamba kuna vitu navijua vizuri lakini kuna watu huwa wanapotosha kwenye jamii tena hata mishipa huwatoka, (hushupaza shingo) hapo ndiyo patamu nikaanza kutafuta jinsi ya kumuelezea binadamu ambaye unamjua kwamba ana akili na ana elimu ya kimataifa lakini huamua kuidanganya jamii hata kwa jambo unalo lijua vizuri hata humu jf wamo
Sahihi kabisa 👍
 
Tupo kwenye uchumi wa kibepari ( soko huria) yeye na ma Tycoon wenzake mfumo wa soko huria unawabeba ,tunachohitaji walipe Kodi tu, kuwasamehe Kodi hawa tycoons na TRA kukomalia Kodi wachuuzi sio fair ,inasababisha mwenye nacho anapata zaidi na asiyekuwa nacho hata hicho kidogo alichonacho kunyang'anywa , mpasuko mkubwa huo na unaleta chuki ya jamii maskini dhidi ya serikali.

Ubepari tumeuiga kutoka nchi za magharibi ,TU copy pia jinsi mihimili ya utawala inavyoendesha nchi.

USA top tajiris wapo kule hata Elon Mask na utajiri wake no 1 wa Dunia anawekewa mipaka Kuna mstari anacholewa hawezi kuuvuka,je huku Tz tutaweza kufika huko ?

Wenye nacho waachwe wapate zaidi watengeneze Ajira. Hela ya tajiri ikikaa benki, watu wa kawaida wanapata mikopo ya kujiendeleeza kibiashara, kujenga, n.k. Tajiri akiamua kutumia hela yake pia watu wa kawaida wananufaika na Ajira zinaongezeka. Ila matajiri wakionekana kama wahalifu fulani, hela wakificha nje ya nchi badala ya kuizungusha nyumbani, wanakuwa hawaleti faida kiuchumi.
 
Mwekezaji Rostam Aziz anatarajia kufanya mahojiano maalum leo Septemba 2, 2025 kupitia UTV.

Ikumbukwe kwa siku za hivi karibuni Mwanasiasa Humphrey Polepole amekuwa akimshtumu kuhusika kwenye mambo mbalimbali ikiwemo ufusadi.

View attachment 3462173
Hiki kipindi kitakuwa kimeandaliwa maalum na wanamtandao. Azam hawana mtangazaji huru mwenye uwezo wa kuuliza maswali magumu. Ameandaliwa chawa ili wafikie lengo lao
 
Back
Top Bottom