Mwanamke: zijue siri za mwanaume mfujaji katika ndoa………………….. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamke: zijue siri za mwanaume mfujaji katika ndoa…………………..

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Feb 22, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Feb 22, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Wanaume wengi wafujaji au watesaji wa wake zao hujitahidi sana kumtenganisha mke na ndugu zake. Wanapofanikiwa kuwatenganisha, wanaume hao huwa wamejitengenezea wigo mpana zaidi wa kuwadhibiti wake zao. Kama mjuavyo lengo la ufujaji kwenye ndoa ni kudhibiti. Mwanaume anapomkosanisha mkewe na ndugu zake anakuwa na uhakika kwamba, mke huyo hana nafasi ya kuondoka kwake kwa sababu hana pa kwenda.

  Lakini kwa kumgombanisha na ndugu zake, mwanaume anapata nguvu ya kumfanya mkewe ahisi kushtakiwa na dhamirana kuanza kuhisi kwamba, ni yeye mwenye matatizo na siyo mumewe, kwani hata ndugu ameshindana nao. Mume pia humkumbushia kwamba ameshindwa hata kuelewana na ndugu zake, yeye ataweza wapi. ‘Ndugu zako tu wamekushindwa , mimi nitaweza wapi?' anaweza kusema hivyo.

  Kwa mwanaume mfujaji, kumgombanisha mkewe na ndugu zake ni jambo la kawaida sana na hufanywa kwa sura mbalimbali. Kwa mfano, mume anaweza kuwaambia ndugu wa mke kwamba mkewe amebadilika sana kwani amekuwa ni mchoyo na hapendi wageni. Na ili kujenga mazingira ya kuthibitisha hilo anaweza kumkataza mkewe kuwahudumia ndugu zake kwa kinywaji chochote wanapokuja nyumbani kuwatembelea. Kwa hiyo ndugu wanapofika hapo nyumbani wakati mume akiwepo, mume huyo kusubiri hadi kiasi cha nusu saa halafu humwambia mkewe, ‘vipi, wageni hawanywi hata soda?' hapo mkewe atawaletea wageni soda, na wageni hao watakuwa wamethibitisha yale maneno waliyoambiwa na mume wake.

  Njia nyingine ni ile ya mume kusaidia sana ndugu wa mke lakini wakati huo huo akitia sumu mbaya dhidi ya mkewe. Anaweza kumpa fedha shemeji au hata baba au mama mkwe na kusema, 'lakini mwenzangu asijue kwa sababu kidogo mambo ya kusaidia hayapendi sana, lakini msimwambie.'

  Nyingine ni ile ya kuwaambia ndugu mambo mabaya dhidi yao ambayo mkewe alimwambia katika mazungumzo ya kutaka aijue familia yake vizuri. ‘Sasa hayo mambo ya kifamilia mimi ningeyajua vipi?' mwanaume atahoji, na itakuwa ni kweli.

  Kuna njia ya kumwambia mke kuhusu ubaya wa ndugu zake. Anaweza kusema kwamba, dada wa mkewe amemwambia kwamba, zamani huyo mkewe alikuwa muhuni . ‘huna haja ya kumuuliza, kaa naye mbali tu, mwepuke huna haja ya kumpa msaada mtu kama huyo. Amenikera sana.' Anaweza kumuonya mkewe. Kwa sababu mke anamwamini mume na hataki mume huyo akasutana na dada yake, hunyamaza tu. Lakini hujenga chuki dhidi ya dada yake.

  Mwanamke anashauriwa kuwa mwangalifu sana na mwanaume mfujaji, hasa linapokuja suala la kumgombanisha na ndugu zake. Kama mume akimwambia mkewe mambo mabaya kuhusu ndugu wa mke huyo, inabidi uchunguzi ufanyike. Mwanamke hapaswi kuamini kila kitu anachoambiwa na mumewe kuhusu ndugu zake……………………………
   
 2. T

  Tall JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2012
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  1. Ufujaji unatokana na mawenge.....umeoa lakini bado hujiamini.
  2. Mwanamke hadhibitiwi bana,wao hujidhibiti wenyewe wakiamua, hao wafujaji sana sana ni kama wanacheza makida.
   
 3. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,224
  Trophy Points: 280
  mwenye masikio na asikie............
   
 4. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2012
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mfujaji wa pesa au mali?
  Au mfujaji wa duduz kupeleka kwenye mashimo mengine?
   
 5. gango2

  gango2 JF-Expert Member

  #5
  Feb 22, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 1,226
  Likes Received: 446
  Trophy Points: 180
  duu mtambuzi !!! kweli balaa
   
 6. A

  Aisha Adam JF-Expert Member

  #6
  Feb 22, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Da! ama kweli we Mtambuzi, shukran kwa somo.
   
 7. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #7
  Feb 22, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kesho naomba uje na ya mwanamke mfujaji.

  ONYO: Kushindwa kufanya hivi kutapelekea maandamano ya mimi na wanaume wengine wafujaji kupinga upendeleo uliouonesha wa kutusema sisi bila kuwasema wake zetu. Maandamano yataanzia kila kona ya mji mpk kwenye server za JF.
   
 8. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #8
  Feb 22, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Hiyo kwenye Bold, ni kwamba unaweza kuigeuza hiyo maneno ya wanaume wafujaji vise versa......................
   
 9. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #9
  Feb 22, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Heshima yako baba,
  Ni somo zuri sana,
  Nadhan salvado wangu hana hii tabia otherwise ungeona mabadiliko uloyataja hapo.
   
 10. obsesd

  obsesd JF-Expert Member

  #10
  Feb 22, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 1,226
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  haya mtambuzi mie niko kufanya analysis tu yan!
   
 11. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #11
  Feb 22, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Na Mwanaume hapaswi pia kuamini kila kitu anachoambiwa na mkewe kuhusu ndugu zake.........................!

  Mkuu salama?
  Naona jana uliwanadi binti zako kwa Tajiri Mweusi! Vipi haukubahatika hata mmoja, waondoe kiwingu hapo home?
   
 12. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #12
  Feb 22, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Hata mimi ninasubiri hii. Kwa kuheshimu huu uzi mzuri bila ya kuuchakachua, tunasubiri huo uzi wa she mfujaji nikitumai kuwa mbinu zao zitakuwa tafauti.
   
 13. K

  Kayinga junior Senior Member

  #13
  Feb 22, 2012
  Joined: Feb 19, 2012
  Messages: 152
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  nitaunda tume ichunguze
   
 14. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #14
  Feb 22, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Dili lilikataa mkuu, yaani angekuwa ni msaada kwangu kuniongezea mtaji kama angekubali ule mpango wa IVF..................LOL
   
Loading...