Mkare_wenu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2011
- 1,714
- 442
Nina na mahusiano na mwanamke mmoja ambaye anaishi mtaa wa jirani ambapo tumedumu kwenye mahusiano kwa takribani mwaka mmoja na nusu, baada ya kuwa nae kwa miezi kadhaa tukatokea kuaminiana na kuanza kusex bila mpira, akawa amepata mimba na nilikuwa nimeplan akishazaa tuanze kuishi pamoja kwavile nilikuwa nampenda na nilihisi ni mtu sahihi anayefaa kuwa mkewangu, na ndugu wengi walikuwa wameshamfahamu.
Bahati mbaya ni kwamba kipindi tunaanza mahusiano hatukuwahi kuzungumza kuhusu kupima HIV, sasa baada ya yeye kupata mimba nilikuwa najua siku akianza kwenda clinic ni lazima ataniambia twende wote, kwa maana sikuhizi ndivyo clinic wanavyotaka, sasa nilianza kupatwa na wasiwasi baada ya kuona mwenzangu hadi mimba inafikia miezi 6 hakuna siku aliyowahi kuniambia habari hiyo na ananiambiaga anaenda clinic, nikahisi kuna kitu ananificha. Kwavile huwa sipendi kukaa na wasiwasi ikabidi siku1 nijitutumue niende kupima mwenyewe kimyakimya bila kumshirikisha, nashukuru Mungu results zikawa Negative, ila bado nilikuwa na wasiwasi naye hivyo ikabidi nijaribu kumdodosa kupitia msg za simu kama ifuatavyo;
Mimi: Clinic sikuhizi hawapimi HIV?
Yeye: Wanapima, mimi walinipima niko fiti
Mimi: Hongera, je hawakukuuliza mwenza maana nnavyojua sikuhizi wanataka muwe wote
Yeye: Kuuliza lazima, tena siku ya kwanza nilipoenda walinifukuza kabisa na kuniambia nije na mwenzangu, Ila nilipoenda siku ya pili na kusema mwenzangu yuko bize sana na kazi hawezi kupata muda wa kuja ndio wakanikubalia wakanipima pekeyangu
Mimi: Kwanini ulilazimika kutunga uongo huo? Je mimi nina ubize wa namna hiyo? Na kwanini hukunipa hata hiyo taarifa ili hata kama nikikataa walau unakuwa umetimiza wajibu wako?
Yeye: Sikutaka kukusumbua tu
Baada ya charts hizo nilikubali kwa shingo upande, ila bado sikumuamini. Siku moja nikamuomba twende tukapime wote, akatoa sababu za kitoto ilimradi tu asiende na kunilaumu ni kwanini simuamini. Hapo akilini ikanijia kabisa kwamba zile hisia zangu zinaweza kuwa sahihi. Nilichofanya ni kugoma kushiriki naye tendo la ndoa hadi atakapokuwa tayari kufanya hivyo. Tukakaa miezi mitatu bila sex hadi alipojifungua. Baada ya kujifungua wazazi walinishauri nianze kuishi naye ili tulee mtoto pamoja, nikawaomba wanipe muda ndani ya miezi miwili nitafanya hivyo.
Siku moja nilikuwa nimelala naye baada ya kujifungua nikambana kisawasawa kwamba ukweli ni upi kwanini hutaki tukapime kama unajiamini uko sawa? Akaniambia ukipima wewe utapata majibu, nikamweleza sisi tumeshakuwa mwili mmoja hivyo ni muhimu kilamtu ajue majibu ya mwenzake na si lazima majibu yafanane. Ukapita ukimya mrefu baada ya muda akaniuliza, je unataka kujua ukweli? Nikamjibu yes, akaniambia 'mimi ni mgonjwa', baada ya kuniambia hivyo sikuonesha kustuka, nikamwabia tu nashukuru kwa kunipa ukweli. Siku hiyohiyo palipokucha kwakuwa ilikuwa imeshapita miezi mitatu nikaenda kucheck tena kwa mara ya pili, namshukuru Mungu kwa 'miujiza' yake nilikutwa negative tena.
NJIAPANDA niliyonayo hapa ni kwamba zile ndoto zangu za kuja kuwa mke wangu ndo zimefail hapa kwakuwa naamini bila sex hakuna ndoa. Je nitawaeleza vipi wazazi wanielewe kuhusu kutomuoa huyu mwanamke wakati niliwaahidi hivyo? Nitumie maneno yepi yatayofanya wazazi kunielewa pasipo kuanika ukweli wa huyu mzazi mwenzangu kuwa mwathirika? Ushauri wenu ni muhimu sana kwa maana muda niliowaahidi wazazi unaelekea kufika kikomo huku hadi sasa sijajua la kuwaambia...