mahirtwahir
JF-Expert Member
- Jan 12, 2013
- 614
- 322
Mke mwema utulivu, hili halina Ubishi
Anakutoa machovu, ya kazini kama moshi
Hana chembe ya uvivu, kila kitu hash hashi
Mke mwema utulivu, ndio raha ya dunia.
Ni raha juu raha, nyumbani ukibakia
Wala hamna karaha, bashasha hunawiri
Huna haja ya kuhaha, baridi roho hukaa
Mke mwema utulivu, ndio raha ya dunia
Kidogo kwake chatosha, hakuna kudangadanga
Na hakuna mshawasha, hata upande wa kanga
Mahaba hunawirisha, japo kibaba cha unga
Mke mwema ni neema, ndio raha ya dunia
Na munapoambizana, hukaa na kusikia
Hafanyi hata kuguna, ishara ya kuchukia
Nyuso zina ng'ara sana, na watu huulizana
Mke mwema ni neema, ni fahari ya dunia
Na mume awa hakongi, majirani hushangaa
Kwa nini jamaa dingi, a shine na kung'aa
Siri chini ya mtungi, hataki hata umbea
Mke mwema ni neema, ndio pepo ya dunia
Na hapendi vijishoga, mara huku mara kule
Na hana muda wa soga, kila siku yuko mbele
Hapendi kuigaiga, kila kitu kwa sumile
Mke mwema rah a sana, kila mtu alijua
Na hata kwenye kibanda, mutaishi kwa murua
Na japo kupanda punda, msimamo hushikia
Hakuna kupinda pinda, na nyuma kufikiria
Mke mwema ni neema, mola akikujalia
Utulivu huwa moyo, si mali wala magari
Wangapi waliyonayo, kukicha haweshi shari
Asubuhi wenda myayo, usiku kucha ngangari
Mke mwema ni neema, Muume akiwa nayo
Tabia haifundishwi, mtu hujengeka nayo
Na mtu hababishwi, hiyo huwa mwenendoyo
Ni vibaya havipishwi, nafsi huwa na choyo
Mke mwema ni neema, kiumbe ukiwa nayo
Kukicha yananawiri, miaka nenda ishapita
Wala husikii kwiri, hutembea na kunyata
Shamsham bila shari, wajukuu washapata
Maisha huwa matamu, mke mwema kuwa nae.
Na ukipata mkorofi, atakutoa kipara
Kukicha hwishi makofi, na hakuna masikhara
Hugombana na mawifi, ajae humcharara
Mke mwema ni neema, na ni raha ya dunia.