Kitoabu
JF-Expert Member
- Jul 7, 2011
- 11,084
- 12,329
Bandugu habari ya mutwekati? Bana abajambo? Kilebe sene kasunu sinkombwa mundu bandu mpapa mpapa mwee! Leo nimeamua kufungua kilichopo ndani ya mtima wangu. Nimiaka mingi tangu nilipo pata wazo hili nalo silingine bali ni kumuoa Mwana mke wa kimasai kwa gharama zozote. Ikibidi hata kuingia msituni kupambana na Simba ili tu nimuoe Mwanamke wa kimasai. Mimi ni mtu wa Pwani utamaduni wetu ni kilimo na Uvuvi kwetu hatujui kufuga naikiwa kufuga huwa tunafuga Kuku pamoja na Bata. Lakini hilo asijali kwakuwa mimi ndie mwenye shida nipo tayari kufuata mila zote za kwao (Ufugaji na Uwindaji) ikibidi hata jeans nitaweka pembeni nakuanza kuvaa Mashuka pia kutoboa masikio. (ispokua kuvaa shanga kiunoni) Tafadhali kama yupo Mwanamke wa kimasai humu ndani basi ajue mimi nampenda (haijalishi) ikibidi ani PM. Sichagui Elimu wala Umri ninacho taka ni kuoa Mwanamke wa kimasai tu.