Valentina
R I P
- Oct 12, 2013
- 24,688
- 28,850
Somo hili sio langu ila nimeona vema kushare nanyi wanawake wa MMU,najua kila mtu angependa mahusiano yake yawe ya mfano bora wa kuigwa...
Naomba niwapestie kama ifuatavyo linalokufaa chukua ukaboreshe ndoa/mahusiano yako
VYAKULA VITANO MUHIMU KWA MMEO VITAKAVYOMFANYA AKUFANYE MALKIA WAKE ASIYEWEZA KUKUPOTEZA KWA LOLOTE AU YEYOTE.
1. UTII USIO NA SABABU WALA MASWALI.
Waefeso 5:22-24, 1Petro 3:1-6.
Wanawake wengi hata waliookoka, wanataka waume zao WAWAPENDE KWANZA ILI NA WAO NDIPO WAWATII, Lakini hii si kweli!
Timiza wajibu wako, halafu Mungu atakusaidia kuugusa moyo wa mmeo kukupenda!
Usimtii mmeo kwa sababu ya zawadi, outing au kwa sababu ya jema lolote alilokutendea, MTII KWA SABABU NI MMEO, ALIYEKUONDOLEA AIBU YA KUWA MIONGONI MWA WANAWAKE SABA WANAOGOMBANIA MKE MMOJA (Isaya 4:1).
Hilo tu linatosha kukufanya uwe kama Mama yetu Sara, na kukupelekea KUMTII NA KUFIKA MAHALI PA KUMWITA BWANA WAKO UNAYEMTII BILA MASWALI NA UNAFURAHIA HILO (1Petro 3:6).
Kuna kitu kinaitwa UTII BILA SHURUTI.... Mtii mmeo, bila kulazimishwa na bila sababu zaidi ya ukweli ya kuwa ni mmeo, hakika UTAPENDWA NA KUONA MEMA YA NDOA YAKIKUJIA!
2. CHAKULA KIZURI
Kilichompa Yakobo baraka ya Esau, NI MADIKODIKO YA REBEKA.
Haikuwa ISSUE YA KULETA TU NYAMA.
Ilikuwa ni issue ya KULETA NYAMA ILIYOANDALIWA ANAVYOPENDA ISAKA.
Rebeka alimsaidia Yakobo kumuandaa yule mbuzi kwa MAUJUZI YALE YALE YA REBEKA, kumbuka Yakobo alikuwa akikaa jikoni na mama yake, hivyo alijua MAPISHI YA MAMA YAKE YANAYOMPAGAWISHA BABA YAKE!!
Mtumishi wa Mungu Askofu David Oyedepo wa makanisa ya Winners Chapel, anasema, *NJIA YA KUELEKEA KWENYE MOYO WA MWANAUME, IKO TUMBONI MWAKE, UKILIGUSA TUMBO LAKE VIZURI, UMEUPATA MOYO WAKE!*
Pambana kwenye eneo la mapishi, uwe bora mwanamke!
Mpikie vitu ambavyo HAJAWAHI KUVIONA KWA MAMA YAKE.
Mchanganye kwenye eneo hili na afike mahali ASIFIE WAZIWAZI MAPISHI YAKO.
Afikie mahali MKITOKA OUT adharau mapishi ya hotel au mgahawa mliokwenda kwa sababu ya MKONO WAKO WA MAPISHI!!
3. ULIMI WAKO MWANAMKE.
Ukisoma 1Samweli 25, utaona Daudi alikuwa AMEKASIRIKA NA AMEAPA ANAKWENDA KUMUUA NABALI NA FAMILIA YAKE YOTE.
Lakini alipokuja Abigaeli mke wa Nabali, ALITUMIA ULIMI WAKE KUMPAMBA, KUMSIFIA DAUDI, NA KUMPOZA MPAKA AKAGHAIRISHA KUMUUA NABALI.
Abigaeli alifungua mdomo wake kwa hekima mno, hakuruhusu MANENO ILIMRADI MANENO, BALI ALIONGEA ASALI TUPU, DAUDI AKAACHANA NA KUMUUA MMEWE!
Hata Nabali alipokufa, DAUDI ALIISHIA KUMUOA ABIGAELI KWA SABABU YA MATUMIZI MAZURI YA ULIMI.
Mithali 31:26 inasema, *MKE MWEMA HUFUNGUA KINYWA CHAKE KWA HEKIMA, NA SHERIA YA WEMA I KATIKA ULIMI WAKE...*
Ikiwa na maana ya kuwa MWANAMKE ANAYEWEZA KUDHIBITI ULIMI WAKE, NA ASISEME NA MMEWE KAMA ANAZUNGUMZA NA KIJANA YEYOTE, AKAJISHUSHA NA KUTUMIA ULIMI WAKE KUMTAMKIA MEMA MMEWE NA KUUKUNA MOYO WA MMEWE KWA MANENO LAINI, YA KUTIA MOYO, KUMSIFIA, KUMUITA BORA, MTU MKUU, NAKADHALIKA, MWANAMKE WA HIVI ATAMFURAHIA MMEWE NA ATAPENDWA MPAKA UPENDO WENYEWE UONE WIVU!!
Tatizo la wengi ni ndimi zao, wanadharau waume zao, wanajibizana nao kama watoto wadogo, wanawanunia na kuwatusi, halafu wanasema, WANAUME SI LOLOTE SI CHOCHOTE.
Ulimi wako unaweza kuipa uhai ndoa yako au kuiua (Mithali 18:20-21).
Mtumishi wa Mungu mtu wa hekima, MIKE MUDORCK anasema, *"Kila MWANAUME ana upande wa HEKIMA na upande wa UPUMBAVU, unachosema naye kitaamua upande upi utakaouona. Ukisema naye kipumbavu utakutana na upumbavu wake, ukisema naye kwa hekima utakutana na hekima yake..."*
4. KITANDANI
Mme anaupenda mwili wa mkewe.
Naweza kusema mojawapo ya sababu za yeye kukuoa ni ili AWE NA UMILKI WA MWILI WAKO PEKE YAKE!
Linapokuja suala la kitandani, HAKUNA UFUNDI WOWOTE ZAIDI YA KUONGEA KWA UWAZI WEWE NA MMEO.
Maandiko yanasema, *Mme hana utawala juu ya mwili wake bali mke, na mke hana uhalali wa mwili wake isipokuwa mme...*
Hivyo tendo la ndoa ni la muhimu sana kwa mmeo, hakikisha unakuwa huru naye, muambie unachotamani akufanyie, USIWE BUBU CHUMBANI, SEMA WAZIWAZI NA MMEO.
Kikubwa vitu kama ulawiti (mapenzi kinyume na maumbile), HILI LIKATAE LIPINGE, MAANA NI DHAMBI NA NI UHARIBIFU HATA KIAFYA.
Mmeo akitaka tendo la ndoa kinyume na maumbile, KATAA KWA HERUFI KUBWA KABISA!
5. KUIWEKA NYUMBA YAKO KATIKA UTARATIBU.
Mithali 31:15
Suala la kuamka mapema, kuweka mambo ya nyumba yako sawa, kujua kila kitu nyumbani mwako na kukicontrol NI WAJIBU WAKO MWANAMKE.
Na lolote linalokuwa limekuzidi hekima au haliko sawa, lilete kwa mmeo mapema, usisubiri aligundue mwenyewe, maana ataona unamficha au hutambui nafasi yake kama kichwa!
Wewe ndo Waziri mkuu wa nyumba yako, hakikisha kila jambo linakwenda sawa na kwa dharura yoyote mjulishe Rais wako yaani MMEO.
UKIFANYA HAYA KWA UMAKINI, BIDII NA MAOMBI, NDOA YAKO ITAKUWA BORA NA YA FURAHA MNO.
Sent using Jamii Forums mobile app