Mwanamke uliyeolewa jua kuitumia smartphone yako vizuri

Emoj

JF-Expert Member
Oct 9, 2015
837
1,282
Mwanamke aliyeolewa ni msaidizi wa mume wake, kuhakikisha amempikia mumewe,amemfulia, na mumewe akitoka kazini akili zake zote ziwe kwake, amuhudumie kwa kila kitu akisimama katika nafasi yake kama mwanamke aliyeolewa. Pia mwanamke aliyeolewa ni nguzo ya familia yampasa kuwa mtu anayemwomba Mungu kwa Imani yake kila wakati na pia kuwalea watoto vizuri na kuhakikisha usalama wao,

Siku hizi smartphone zinatuponzaa wanawake, kila saa tuko mitandaoni, mara kutafuta umbea, mara kuupload picha zisizo na mantiki et umepita kwa mangi umenunua kachips umepiga picha chaap umepost, mara kuandika status za vijembe watsapp, mara kutukana kwenye mitandao,
mwanamke umeolewa una account 20 insta,magroup yasiyo na maana ndo usiseme, mume karudi kazini wewe huna habari umetundika miguu uko busy na simu housegirl ndo amuhudumie mumeo chakula, we unafanya kuagiza tu nipe hichi mnawishe baba mikono kweli jamani?, smtms hadi unapika chakula kinaungua kisa ukobusy na simu.

Mara umepigiwa simu na mwanaume gani sijui anaongea upuuzi wewe ni kuchekacheka tu .Shost anakupigia simu nusu saa mnaongea tu upuuzi,hadi mwanaume anaboreka akikusubiria umalize kuongea aseme nawe jambo.

watoto wala huna habari nao hujui kwamba wamekula,hujui yupi ana homa, ni housegirl ndo anakuja kukuambia mama, Debora joto lake leo liko juu.mama mtu hujui kama joto la mtoto liko juu ila unajua picha ya mwisho leo wema sepetu kaweka insta kweli???? Halafu unajiita umeolewa wakati hujui majukumu yako kama mke??.

Aisee Wanawake mlioolewa badilikeni, simaanishi kwamba msitumie smartphone ila muwe na kiasi, hii ya mke wa mtu kiiila saa uko mitandaoni pasipo na sababu ya msingi acheni,waachieni single Girls.
 
Upo sawia emoj,wanawake wengine wanatia aibu

Akiamka asubuhi ni kuoga na kutoa maagizo kusepa chupi analoweka za wiki nzima

Akirudi sakumi anajikalisha kochini bze na cm,hana lugha ya kuongea na watoto ye ni kupaza sauti tu na kila kitu housirl...

Kujua mipaka na wajibu ni kitu muhimu sana.
 
Ngoja waje hakika patachimbika ila nawapenda sana wanajua kubadili gia angani hii mada itageuka watazungumzia VIBAMIA na kumaliza within 30 mins itakua ndio hadithi hapa.
Smartphones ni janga kwa kweli na upuuzi wa IG ni kaka wa janga hili kuna jukwaa ukitembelea pia utagundua familia zetu kesho zitakua za aina gani kwangu naamini ni janga la wote ingawa wanawake wameathirika vibaya mno.
 
utawaweza wanawake wanao waza mpo bado kwenye relations za ujana wakati ameshaolewa na kuitwaa mama juu
 
Ngoja waje hakika patachimbika ila nawapenda sana wanajua kubadili gia angani hii mada itageuka watazungumzia VIBAMIA na kumaliza within 30 mins itakua ndio hadithi hapa.
Smartphones ni janga kwa kweli na upuuzi wa IG ni kaka wa janga hili kuna jukwaa ukitembelea pia utagundua familia zetu kesho zitakua za aina gani kwangu naamini ni janga la wote ingawa wanawake wameathirika vibaya mno.
Kama umepiga ikulu kimtindo but ni udhaifu mkubwa sana ila ndo umeisha maliza gia ya angani itatumika hapa.
 
Upo sawia emoj,wanawake wengine wanatia aibu

Akiamka asubuhi ni kuoga na kutoa maagizo kusepa chupi analoweka za wiki nzima

Akirudi sakumi anajikalisha kochini bze na cm,hana lugha ya kuongea na watoto ye ni kupaza sauti tu na kila kitu housirl...

Kujua mipaka na wajibu ni kitu muhimu sana.
Tena sauti kama ya Jecha
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom