Jaguar
JF-Expert Member
- Mar 6, 2011
- 3,440
- 1,029
Hii ilitokea huko wilayani chunya mkoani mbeya.Mke na mume wakitoka shambani mara ghafla chatu mkubwa aliwavamia na kumdaka mwanaume.Wakati chatu anajiandaa kumvunja mbavu na hatimaye ammeze,mwanamke alipiga yowe huku akimrushia chatu mchanga.Chatu hakuachia kirahisi mpaka pale mwanamke alipovua khanga na kumfunga kichwa yule chatu kiujasiri.Mara baada ya chatu kumwachia mwanaume,ile khanga ilinasa kwenye kisiki na ikamvuka.Chatu hakufanya ajizi,faster alimdaka mwanamke safari hii.Mwanamke alipiga kelele kuomba msaada lakini mumewe alikuwa busy na mbin za nyika akijaribu kuvunja record ya mjamaica usain bolt.Mungu mkubwa,walitokea wasamaria wema wakamwokoa yuke mwanamke kutoka himaya ya yule chatu.Je ungekuwa wewe ndo huyo mwanamke,ungechukua uamuzi upi?kumrudia mume au la?