Kwanza kabisa niwasalimu vijana wenzangu tunaowaza kujikwamua katika umaskini.
Kumekuwa na dhana ambayo mm kwangu naiona ni kama chachu ya maendeleo kwa vijana wa kisasa, dhana hii ni juu ya kushare na mpenzi au mke kile unachokipata hata kama sio kwa 100% namaanisha mshahara au kipato.
Hapa ni pale wanasema za kuambiwa changanya na zako ujijibu, katika kukua kwangu nilikuwa nikisikia wazee kwakisema Mwanamke haoneshwi wala hatakiwi kujua kipato cha mpenzi au mume wake lakini niliiga kwa familia moja ya ndugu yangu wao walikuwa wanashare kile wanachokipata na japo kilikuwa kidogo ila walifanikiwa sana.
Sasa na mm baada ya kufikia hatua ya kuishi na mwenzangu nikaamua niwe na share nae kipato kwa kumuonesha salary slip na kabla ya kupata mshahara tulikuwa tunakaa chini na kuweka malengo na matumizi na kumbuka mda huo yeye alikuwa hana kazi na elimu yake niya 4m four wakati mm nina bachelor, baada ya mda alipata kazi na alikuwa akipata hela nyingi na hapo ndipo niliona sikukosea kumuonyesha mfano maana baada ya mda mfupi tuliweza kununua kila kitu na hata nyumba tuliyokaa tukahamia kwenye kubwa na tukafanikiwa kujenga na nyumba standard ndani ya mwaka na nusu tuu hapo nikiwa na 27yrz na yeye ana 23yrz only.
Nawashauri vijana wa kiume msiache kushare na wapenzi wenu vipato vyenu na umpe nafasi ya yeye kutoa maoni na ushauri juu ya matumizi ya hicho mnachokipata hata kama hakupata fursa ya kuendelea na masomo na hii itakusaidia kumjua mind set yake
Sijaweka nukta unaweza kudondoka xperience yako katika hili