Mwanamke na Mahusiano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamke na Mahusiano

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by SmithG, Jul 20, 2012.

 1. S

  SmithG Member

  #1
  Jul 20, 2012
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wanawake wote wana uwezo mkubwa sana juu ya wanaume tatizo kubwa wanawake wengi wameshindwa kutumia uwezo wao na ushawishi wao kuhakikisha anamuweka mwanaume sawa na kufanya vile anapenda kwa sababu hawajifahamu, Hapa ninazungumzia kufanya yale ambayo mwanamke anaamini mume wake anazembea kama vile kuweka mahusiano katika mstari sahihi.
  Bottom line ni kwamba, mwanamke anao uwezo mkubwa ktk kuvumbua kilichomo ndani ya mume wake na kwamba mwanamke akitumia uwezo wake ambao Mungu amempa kuhusu mume basi anaweza kujenga mahusiano na ndoa inayoridhisha.
  Wapo wanawake wengi kila kukicha wanalalamika, mume wangu, mume wangu, acha kulalamika, tumia uwezo wako wa kuwa mwanamke kumsaidia mume kuwa mume bora ktk ndoa kwani Mungu amekupa uwezo wa ajabu ndani yako kiasi kwamba mume yeyote anaweza kukubali kile mke anasema pale mke akitumia uwezo wake sawa na Mungu alivyompa.
  Kauli yako ni kitu muhimu sana ktk mustakabali wa kulijenga au kulibomoa penzi lenu.
  {Kuna usemi kwamba: “A man’s wife has more power over him than the stale”
   
 2. Catherine

  Catherine JF-Expert Member

  #2
  Jul 20, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 1,263
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwahiyo wanaume mnanyoosha miguu mkisubiri muambiwe fanya hivi au vile! Hivi hamuwezi kuwa wanaume bora bila wanawake kutumia hiyo power? Mtu mzima tena above 25 unataka uwekwe vipi sawa! Badilikeni wenyewe, msitumalizie nguvu zetu za kike jamani.
   
 3. B

  Bi nyakomba JF-Expert Member

  #3
  Jul 20, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 387
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  hee! makubwa
   
 4. C

  CAY JF-Expert Member

  #4
  Jul 20, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 501
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwenye bold hapo ........... .
   
 5. S

  SmithG Member

  #5
  Jul 20, 2012
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mithali 14:1 " Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe"
  Mithali 12: 15 " Njia ya mpumbavu imenyoka machoni pake mwenyewe: Bali aliye na hekima husikiliza shauri"
   
 6. marrykate

  marrykate JF-Expert Member

  #6
  Jul 20, 2012
  Joined: Mar 4, 2012
  Messages: 589
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  huwa sielewi kwa kweli, hivi mwenye jukumu la kulinda penzi ni mwanamke tu? ndie anaenufaika sana na mapenzi au nini, msituchoshe bana ukiona sio type yako chagua mwingine
   
 7. S

  SmithG Member

  #7
  Jul 20, 2012
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mithali 11: 22 "Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe, Kadhalika mwanamke mzuri asiye na akili"
   
 8. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #8
  Jul 20, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  Afu hakuna hata waganga wa kuongeze nguvu za kike afu mtoa mada anatushauri tuzitumie bure bure

   
 9. S

  SmithG Member

  #9
  Jul 20, 2012
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mithali 15:2 " Ulimi wa mwenye hekima hutamka maarifa mazuri; Bali vinywa vya mpumbavu humwaga upumbavu"
   
 10. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #10
  Jul 20, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,672
  Trophy Points: 280
  Mwanamke ana nguvu kubwa kuilinda ndoa kuliko mwanaume!
   
 11. Bra-joe

  Bra-joe JF-Expert Member

  #11
  Jul 20, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,559
  Likes Received: 510
  Trophy Points: 280
  Mtoa mada kama umeoa, kwa maelezo yako inaonekana mke wako ndiyo kichwa ktk familia na wewe ni mkia.
   
 12. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #12
  Jul 20, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,700
  Likes Received: 12,750
  Trophy Points: 280
  Una wadanganya sana! Hawawezi kulazimisha penzi mwisho wa siku watakwenda kwa waganga na kuwafanya wame zao mazezeta!

  Wasitumie nguvu nyingi bali akili.
   
 13. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #13
  Jul 20, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Whatever happened to 'mwanaume ndio kichwa cha nyumba? Mara hii mnataka kukokotwa, mnaskia uvivu kuwa vichwa? This dot com generation:wacko:
  :loco:
   
 14. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #14
  Jul 20, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  mtoa mada unafurahisha sana unavyomwaga mistari iliyochaguliwa kwa makini ku-highlight consistently dhana ya 'upumbavu'.....
   
 15. S

  SmithG Member

  #15
  Jul 20, 2012
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mithali 18:2 " Mpumbavu hapendezwi na ufahamu; Ila moyo wake udhihirike tu"
   
 16. S

  SmithG Member

  #16
  Jul 20, 2012
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mithali 24:3 " Nyumba hujengwa kwa hekima, Na kwa ufahamu huthibitika"
   
 17. S

  SmithG Member

  #17
  Jul 20, 2012
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mithali 15:2 "Ulimi wa mwenye hekima hutamka maarifa vizuri; Bali vinywa vya wapumbavu humwaga upumbavu"
   
 18. S

  SmithG Member

  #18
  Jul 20, 2012
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mithali 15:21 " Upumbavu ni furaha kwake na aliyepungukiwa na akili, ....................................................................."
   
 19. Catherine

  Catherine JF-Expert Member

  #19
  Jul 20, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 1,263
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  mwanaume mpumbavu nae huifanyaje nyumba yake?
   
 20. Catherine

  Catherine JF-Expert Member

  #20
  Jul 20, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 1,263
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  hapo chacha! Tuzitunze nguvu zetu za kike Kongosho.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...