Mwanamke mwenzangu, Je ni lini mara yako ya mwisho kuangalia utupu wako?

Zinduna

JF-Expert Member
Nov 6, 2011
2,378
3,379
117.jpg


Kwa mwanamke kila mmoja kutokana na malezi au mila na desturi za kabila la kwao ana mtazamo wake linapokuja swala la kuangalia utupu wake iwe ni kwa kuuchunguza au kwa kutaka tu kuangalia tu kama utupu wake umefananaje.

Binafsi katika malezi yangu mama yangu alitufunza mimi na dada zangu kuhusu usafi wa mwili hususan usafi wa sehemu za siri, alikuwa anatukataza kufuga kucha ndefu ili tuweze kusafisha tupu zetu vizuri bila kuogopa kujiumiza na kucha, kwa hiyo kwetu sisi swala la usafi wa sehemu za siri halikuwa na mjadala maana mama alikuwa analisimamia vyema. alitufanya wote kuziona sehemu zetu za siri kama kitu cha kawaida na kutujengea tabia ya kuangalia tupu zetu na kujichunguza ili kuona kama kuna tatizo.

Wapo baadhi ya marafiki zangu wa karibu ambao waliwahi kukiri kwamba hawawezi kuangalia tupu zao. nilipowauliza sababu wapo ambao walidai kwamba hawajisikii vizuri kuangalia tupu zao wapo waliodai waliambiwa na wazazi wao ni vibaya kuangalia sehemu zao za siri na wapo waliodai waliwahi kuambiwa na marafiki zao wakati walipokuwa shuleni wakisoma kwamba tupu zao hazina muonekano mzuri, nikabaki kushangaa, kwamba kwani utupu mzuri unatakiwa ufananeje? Yaani sehemu ya mwili wako ambayo unaisafisha karibu kila siku bado ukose hata fursa ya kuangalia na kujua kama unafananaje!

Labda huenda wapo baadhi ya wanawake wenzangu wanaweza kunishangaa, hebu naomba mnijibu. Je ni lini mara yako ya mwisho kuangalia utupu wako?
 
Sidhani kama kufanya hivyo ni taboo isha, utafanyeje usafi wa sehemu hiyo nyeti pasipo kuikagua ndani ili kujiridhisha ukuwa iko safi?

Sikumaanisha kwamba mtu asijisafishe sehemu zake za siri, i simply said to most people discussing such matters it is a taboo, watu wanaoneana sana aibu talking about their sexuality & well being.
 
Back
Top Bottom