Mwanamke mwenye watoto wawili nani atakutaka!

Huyo mtu hajakosea sana, kama umeondoka kwa mumeo kwa matarajio ya kuolewa tena utakuwa umekosea sana. Kama alivyokwambia huyo mtu kuwa kuolewa na watoto wawili ni vigumu sidhani kama alimaanisha kwa maswala ya kuchujuka na nini, nina imani alimaanisha katika suala la matunzo. Jamani maisha siku hizi si mchezo wewe mwenyewe unamfano halisi wa wanaume wanaopenda kulelewa, nani atakubali aje alee watoto wa mwanaume mwenzie, sana sana atakwambia uache watoto uende peke yako.

Huo ndio unakuwa mwanzo wa kutesa watoto. Yaani kwa tarajio la kuolewa tena, utaishia kupata golikipa mwingine, achana na hiyo mawazo for now..Hawa watu hawatofautiani sana ndugu yangu.
 
Hii sredi inawafaa sana kina mama

Kwa sisi wanaume, nyie wanawake mkiondoka kwenye ndoa tunaoa tena na tena na tena. Bila kujali tuna umri gani na tuna watoto wangapi..

Leo ngoja niwasome zaidi.
 
Hata hapa nimeileta kwa heshima kwani maoni yake yalinipa changamota ambazo niliona ni vizuri kushare, jamii forum is an open forum kufungua akili zaidi. natambua maana ya PM na ndio maana siwezi kumtaja katu, hata hivyo asante kwa kuliangalia hili kwa upande mwingine


nijibu swali langu nililokuuliza......
 
Maswali mazurisana umeuliza kuhusu ndoa,pili,ubora wako hauwjaondolewa kwa kuzaa bali uko palepale,jiamini na ujithamini,kama ndoa inakutesa ondoka,wapo ambao watakuthamini kama ulivyo!
 
Mwambie mtu mzima atishiwi nyau. Yeye anakuona wa nini kuna wengine wanajiuliza watakupata lini. Asijifanye anakusaidia sana kuwa na wewe. Mmeo ana dharau sana; eti watoto wawili atakutaka nani; eeeh presure imepanda hana lolote.

Asanteni sana wadau kwa michango yenu kwenye my last thread titled "I have moved".

My heading is quoted from one of the PM nilizopata kutoka kwa wadau, mdau mwenyewe ni mwanamke.
Namshukuru kwa ushauri wake umenipa changamoto nzuri tu, lakini kutoka katika ushauri wake ambao ananiinstist nisitoke kwenye ndoa, nimeibuka na maswali.
  • Ananiambia ni bora nirudi eti mimi mwanamke wa miaka 32 ndio kwanza mihemko inachanganyia nitaishia kuiba waume wa watu koz sitapata mwanaume aliye single
  • Pili anasema eti nani atanikubali mimi na watoto wangu wawili bora nivumilie
  • Tatu Heshima kwa jamii
sasa wadau nimejiuliza maswali mengi sana na kuona kuwa kweli watu wengi wanaishi maisha ya uongo,

Hivi ni nini hasa msingi wa ndoa??
Je ni Mapenzi??
Je ni Status kwa jamii
Au ni security ( kwa maana huwezi kupendwa tena pindi utakapotoka kwenye ndoa) au nini hasa??
Au kila ndoa ina msingi wake so katika maamuzi yapasa kuconsider msingi wa ndoa hiyo kwanza instead of kugeneralise?

Na je Tunaingia kwenye ndoa ili tuishi ama tunaishi ili tuwe kwenye ndoa? I mean kati ya ndoa na maisha nini kinakuja kwanza?
 
mama mmoja jirani yangu kule mlimani, aliolewa akiwa na watoto wanne, tena wakubwa kabisa.
Kama ipo ipo tu. Kama utaolewa utaolewa tu! Usibabaike.
 
Maswali mazurisana umeuliza kuhusu ndoa,pili,ubora wako hauwjaondolewa kwa kuzaa bali uko palepale,jiamini na ujithamini,kama ndoa inakutesa ondoka,wapo ambao watakuthamini kama ulivyo!
Theoretically uko right, lakini practically ndugu yangu,labda mama awe na uwezo wa kujitegemea mwenyewe kidogo, hivi hivi huu ni mwanzo wa matatizo mengine, society tuliyopo bado haijafikia huko wanakotaka hawa kina mama wengi wa sasa, wanajiita Independent women!
 
watoto si tatizo kwa kuanzisha mahusiano mapya, mapenzi ni mapenzi tu haijalishi yaliyopita. labda tatizo hapa ni je wewe ukianza mapenzi mapya na mtu mpya na mumeo nae hali kadhalika akapata wake, hawa watoto wataenda wapi, je watapataja mapenzi na malezi ya dhati toka kwa wazazi wote wawili?? ila ndo ni mapenzi, jali mapenzi yako na umpendae na si jamii inakutizama vipi?
 
Best ndoa ni mapenzi km hakuna mapenz ndoa ni ndoano kila cku utakutana na mitihan itakayofanya ujihc kwanini haukutoka jna,kwakuwa ndoa icyo na mapenz haina kuhurumiana ni kuumizana 2.
Maisha kwanza kuolewa huko ni probability,na status ya m2 c mara zote inakuzwa kwa kuolewa.
K2 cha mcng km unataka kutoka kwenye ndoa hakikisha utaweza ishi kwa kujiheshm zaid,huku ukizuia mihemko ya mwil ili icwe umetoka then unafanya mambo ya ajb yanayokudhalilish zaid,na pia uweze kuwa2nza watoto wako bla yakumsumbua jamaa km itabd watoto wawe kwako.
 
Back
Top Bottom