Mwanamke Mwenye Mimba ya Watoto Tisa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamke Mwenye Mimba ya Watoto Tisa

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, Apr 30, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [TABLE="width: 491"]
  <tbody>[TR]
  [TD="colspan: 3"][/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #E1E1E1"]
  [TD]
  [​IMG]
  Karla Vanessa Perez, mwanamke mwenye mimba ya watoto 9[/TD]
  [TD]Monday, April 30, 2012 1:53 AM
  Mwanamke mmoja wa nchini Mexico amekuwa gumzo duniani baada ya taarifa kutolewa kwenye televisheni moja ya nchini humo kuwa mwanamke huyo ana mimba ya watoto tisa na anatarajia kujifungua mwishoni mwa mwezi ujao.[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Kwa mujibu wa televisheni maarufu ya nchini Mexico inayojulikana kama Televisa, mwanamke huyo aliyetajwa kwa jina la Karla Vanessa Perez anatarajia kujifungua mwezi ujao watoto sita wa kike na watatu wa kiume.

  Karla ambaye aliwahi kuzaa watoto watatu mapacha, anatoka kwenye mji wa mpakani wa mwa Mexico, Coahuila, unaopakana na jimbo la Texas la nchini Marekani.

  Karla anadai kuwa alifanyiwa matibabu ya kupandikiza mimba kwa njia ya kitaalamu ya IVF kwenye hospitali ya taifa kwenye mji wa Saltillo.

  Karla ambaye umri wake haukutajwa alisema kuwa yeye na mumewe Bernardo walifanyiwa matibabu ya kurutubisha mbegu za kiume na mayai ya uzazi hali iliyopelekea kupata mimba ya watoto wengi.

  Televisheni ya taifa inayoitwa Notimex nayo ilitoa habari ya mimba ya watoto tisa ya mwanamke huyo na kuongeza kuwa Karla anatarajiwa kujifungua watoto wake mnamo tarehe 20 mwezi ujao.

  "Ni mapema sana kuanza kuchagua majina ya watoto" Karla aliiambia televisheni hiyo ya taifa na kuongeza "Kitu cha kwanza tuombe kila kitu kiende vizuri".

  Wakati gumzo likiwa limetanda juu ya mimba ya mwanamke huyo huku mumewe akijivunia mkewe kuwa na mimba ya watoto wengi kiasi hicho, daktari mmoja nchini humo ameibuka na kudai Karla hana mimba ya watoto 9.

  Daktari huyo amedai kuwa alimfanyia ultra-sound Karla na kwenye tumbo lake hakuna hata mimba ya mtoto mmoja.

  Mamlaka ya afya nchini Mexico imetangaza kuwa itafanya uchunguzi kujua kama Karla ni kweli ana mimba ya watoto 9 kama alivyonukuliwa na vyombo vya habari au kama anaongopa.[/TD]
  [/TR]
  </tbody>[/TABLE]

  Mwanamke Mwenye Mimba ya Watoto Tisa
   
 2. SIMBA WA TARANGA

  SIMBA WA TARANGA JF-Expert Member

  #2
  Apr 30, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 992
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nasubiri wazaliwe.
   
Loading...