Si kweli! Si kila mtu anaetaka Mwanamke aliemzidi umri basi ni domo zege au ana mapungufu financially, assumptions za namna hii ni mbovu kwa sababu wasichoelewa wengi ni kuwa mwanamke mtu mzima amepitia vingi, anajua mengi, ana hisia za dhati kama akipenda na si mshamba kama walivyo baadhi ya wanawake wenye umri mdogo au wa kati ambao hawana uzoefu wa maisha.
Mimi nikimpata namchukua na nitamlea mimi na si kwa sababu ni tegemezi ila mapenzi, na nitamlea Mimi coz najimudu; Nimewekeza kwenye Bar kadhaa upande wa jikoni, nina biashara za M-pesa, Tigopesa, Airtel Money, Nina Maduka ya vyombo na nguo, hizo ni baadhi ya biashara nilizonazo ukiacha mali ninazomiliki ambazo sitazitaja na zisizo za biashara, sidhani kama naweza kuwa tegemezi kwa mtu na umri huu.
Kwa hiyo wakuu, hayo ni mawazo ambayo si ya kuyazingatia sana.