mbalisana
Member
- Dec 15, 2011
- 46
- 42
"Mwanamke mpumbavu huvunja nyumba yake kwa mikono yake mweyewe" huu ujumbe nimekutana nao mara nyingi ila kwa siku hizi unanichanganya. Ni upumbavu upi hasa unaotajwa hapa?na je kuna wanaume wanaopelekea nyumba zao kuvunjika? hawa wapo katika kundi gani? inanitatiza nimekutana nayo mazingira mengi mfano mume kasafiri kakutana na mwanamke mwingine kazaa nae,mwaka unaofuata kasafiri tena kikazi kazaa na mwingine mwanamke akitaka kuondoka jamii inamwambia acha upumbavu usiondoke utavunja nyumba yako kisa mahawala wa nje.na hizo safari sio za miaka ikizidi sana miezi miwili. na amekuacha unalea watoto na kutunza nyumba hamuwezi kufuatana kila mahali. hii imekaaje jamani. mwanamke tu ndo wakujenga nyumba na kuvumilia yote?