Mwanamke miaka 35 akamatwa kwa ufuska

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 31, 2016
8,557
2,000
MKAZI wa Mgoweko Wilayani Gairo Mkoani Morogoro Shani Suleymani (35) amekamatwa na Polisi na kufikishwa Mahakamani akidaiwa kufanya shambulio la aibu kwa kijana mwenye umri wa miaka 12, ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi Gairo ‘B’ iliyopo Wilayani humo.

Akizungunza na waandishi wa Habari jana Kamanda wa Polisi Wilbroad Mutafungwa, alisema kuwa tukio hilo lilitokea Januari 13, mwaka huu, majira ya saa 8:00 mchana ambapo alisema mwanamke huyo alikutwa akifanya tendo la ndoa na kijana huyo.

Akitolea ufafanuzi kuhusiana na tukio hilo, Kamanda Mutafungwa alisema kuwa, mwanamke huyo alikuwa akifanya tendo la ndoa na kijana huyo tangu akiwa darasa la tatu hadi hiyo siku aliyokamatwa ambapo alisema kuwa chanzo cha tukio hilo ni tamaa za kimwili.

Kwa mujibu wa kamanda mtuhumiwa alifanikiwa kufanya matukio hayo na kijana huyo kwa muda mrefu kwa kuvizia wazazi wa kijana huyo wakiwa wametoka na kwamba pia aliweza kufanya matendo hayo nyumbani kwake wakati mume wake akiwa amekwenda kwenye shughuli zake za kazi.

Aidha alisema mtuhumiwa huyo alishafikishwa mahakamani katika mahakama ya Kilosa Januari 21 mwaka huu kwa CC/37/2019 na kwamba tarehe 31 mwezi wa kwanza akiwa nje ya dhamana alitenda makosa mawili ikiwemo kufanya shambulio la kudhuru mwili na kutumia lugha ya matusi ambapo alikamatwa tena na kufikishwa katika mahakama ya mwanzo ya gairo CCNO/57/2019.

Alitoa wito kwa wazazi kuangalia mienendo ya watoto wao mara kwa mara huku akiwaonya wanawake wanaofanya vitendo vya kikatili kwa watoto kuacha mara moja, kwani wao ndio walinzi wakuu wa watoto dhidi ya ukatili wa aina yoyote ikiwemo kingono.
 

TOEDSLOTH

JF-Expert Member
Nov 3, 2018
790
1,000
Niliwai kusoma nakala kwenye gazeti la Raia Mwema, lenye maudhui ya tukio kama hili lkn yenyewe ilitokea Marekani, Mwalimu kufanya mapenzi na mwanafunzi wake wa kiume, toka chekechea mpka darasa la6 mpka wakazaa, pmja na Mwalimu kupewa kifungo lkn alisema anampenda sana uyo mwanafunzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 

-KANA-

JF-Expert Member
Apr 17, 2017
3,928
2,000
Niliwai kusoma nakala kwenye gazeti la Raia Mwema, lenye maudhui ya tukio kama hili lkn yenyewe ilitokea Marekani, Mwalimu kufanya mapenzi na mwanafunzi wake wa kiume, toka chekechea mpka darasa la6 mpka wakazaa, pmja na Mwalimu kupewa kifungo lkn alisema anampenda sana uyo mwanafunzi

Sent using Jamii Forums mobile app
Movie..... "That's my boy"

- KANA -
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom